ZINAA NDANI YA KANISA! – 01
- Mch. Gasper Madumla
- Jul 19, 2022
- 2 min read
Updated: Aug 29, 2022

1 Wakorintho 5:1 (KJV) “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.”
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Katika kanisa la Korintho kulikuwa na zinaa ya ajabu sana,Paulo anasikitika kuona uzinzi ukifanyika ndani ya kanisa na tena viongozi wa kanisa wamekaa kimya kana kwamba nao pia hufurahia zinaa hiyo. Habari ya uzinzi na uasherati kutoka kanisani imeenea kiasi kwamba si jambo la kuuliza,kila mmoja anajua kinachoendelea. Lakini cha ajabu kanisa halichukui hatua yoyote ya kusafisha zinaa.
Kwa nini viongozi wa kanisa walikaa kimya?
Ikiwa zinaa iliyokithili katika kanisa halafu viongozi wajapoona bado wapo kimya,basi ujue kuna sababu. Kuna sababu nyingi za kuikumpatia zinaa ndani ya kanisa, miongoni mwa sababu hizo,ni;
01. Msingi mbovu
Jambo lolote linalokusudiwa lisimame vyema linahitaji msingi mzuri. Kanisa nalo lililosimama vyema kiimani na kiimadili linahitaji msingi mzuri. Lakini msingi ukiwa mbovu ni dhahiri nyumba nayo itayumba,itakuwa mbovu tu! Kanisa lenye kuikwepa zinaa hutegemea sana msingi wake uliowekwa na mbeba maono / mwasisi.
Mfano, kiongozi akizoelea “utani” basi ujue washirika watamzoe sana na kushindwa kupokea maelekezo Kwa usahihi wake. Angalia pale kiongozi anapocheka cheka na wana kwaya,au praise team yake.
Hivi unajua,mazoea yakizidi uzaa mizaha na,kupelekea kuvunjikia maadili,hapo ndipo utaona mchungaji akishindwa kukemea uovu,
Kwa maana mchungaji atapata nguvu wapi ya kuwakemea ikiwa wakosaji ni marafiki zake walioshibana kiasi cha kutaniana kama watoto!!!
Viongozi wa kanisa la Korintho nao walikuwa na mazoea makubwa sana na washirika wao hasa katika hali ya kufanya mizaha.
Lakini pia, tunapozungumzia suala la “msingi mbovu” tunahusisha na suala zima la “mfumo wa uongozi mbovu” ambao hutoa mwanya wa uzinzi. Fikiria ikiwa kama kila mtu ndani ya kanisa ana uhuru wa kumwona mchungaji ofisini moja kwa moja kwa moja kisha kukaa huko ofisini kwa muda mrefu,
Je huo sio mlango wa kumwangusha mchungaji?
Kwa maana akina Yezebeli wanaweza kumtega huko huko ndani maana mchungaji yupo peke yake na Yezebeli mwindaji! Hili ni suala la kiuongozi tu,namna ya kupanga vizuri! Hivyo yapo mambo mengi yakikosewa kupangwa mwanzoni katika msingi,ujue lazima zinaa itakuwepo.
02. Viongozi wenyewe ni wazinzi!
Ukweli ni kwamba huwezi kukemea makosa ikiwa wewe mwenyewe ni mkosaji mkubwa. Tambua hili “ mzinzi hawezi kumfukuza mzinzi mwenzake” Viongozi wengi waliokamatwa na “roho za uzinzi “ huambukiza roho hiyo kwa kanisa na hatimaye kanisa linajikuta limebeba wazinzi wa kutosha!
03. Uchanga wa kiroho
Waathirika wakubwa katika kanisa ni “wadada / wanawake “ ambao wanajikuta wakitumiwa kingono labda na viongozi wa kanisa kwa maana wamepotoshwa kimaandiko kwa sababu wao ni wachanga kiroho au wao kwa wao uwakiana tamaa na kushindwa kujizuia kwa sababu hawajakomaa vyema hata kushinda vishawishi .
Mfano yule asiyekomaa vyema kiroho amwonapo binti kavaa vibaya kiasi kwamba maumbile yake yanaonekana,basi ni rahisi kushawishika lakini pia kwa mwanamke mchanga kiroho amwonapo kijana anayeshawishi Kwa kinywa naye ni rahisi kuvutika. Hili ni suala la kukua kiroho tu.
Mtu ambaye amekua kiroho,Hana hisia mbaya za uzinzi hata kama anajaribiwa
ITAENDELEA…
Ikiwa umebarikiwa, nifahamishe na kwa msaada zaidi+255 683 877 900
What’s app +255 746 446 446
Na Mch. Gasper Madumla
UBARIKIWE .
Bình luận