KANISA (THE CHURCH) ~ 02
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 16, 2019
- 4 min read

Muundo wa kanisa / The structure of the church.
Muundo wa kanisa ni ngazi ya uongozi kutoka kwa kiongozi mkubwa wa kanisa mfano Bishop /mtume/ mpaka ngazi ya watenda kazi wengine. Kawaida neno “muundo” huwakilisha picha halisi ya kitu, mfano ukisema muundo wa biblia utakuwa ukizungumzia kuhusu agano la kale pamoja na agano jipya kwa maana maagano hayo mawili ndio yanayounda biblia takatifu. Hivyo muundo wa kanisa ni ile namna ambayo tunaona nafasi ya kingazi ya kila mmoja ndani ya kanisa. Je mchungaji wako ana nafasi gani kanisani? Au je askofu ana nafasi gani kanisani?…
Hivyo utagundua unahitaji kujifunza mengi kuhusu kanisa hasa katika eneo la muundo wa kanisa.
Kanisa ni lazima liwe na muundo/mpangilio maalumu wa kiutawala kuanzia namna ya kutengeneza uongozi ulio imara kwa manufaa ya kanisa pamoja na manufaa ya kila mtu ndani ya kanisa. Ingawa biblia haisemi ni muundo gani mzuri unastahili kufuatwa, lakini biblia imeweka wazi kwamba kanisa linahitaji kuwa na viongozi. Katika kila kanisa limejitengenezea taratibu zao za uongozi, lakini taratibu nyingi leo zinasumbua sana kiasi kwamba ni bora hata zisingelikuwepo!😎 Lakini tunawezaje kutembea bila kuwa na taratibu? Haiwezekani, tunahitaji tuwe na taratibu / mpangilio mzuri utakao tuwezesha tusonge mbele vyema.
Kanisa la Bwana duniani limejengwa katika muundo ufuatao. Hata kama wewe ni wa dhehebu gani, lakini utajikuta upo katika moja ya muundo ufuatao;
Ngazi ya kiongozi mmoja ( Episcopal = bishop – led or pastor – led)
Ngazi ya kundi la viongozi (Presbyterian = Elder -led)
Ngazi ya kanisa kama kiongozi (Church -led)
01.Ngazi ya kiongozi mmoja ( Episcopal)
Ni muundo gani huu?
Huu ni muundo ambao kiongozi wake wa juu, huwa ni mmoja akitoa madaraka kutoka kwakwe kwenda kwenye ngazi za chini za uongozi. Mfano ;kiongozi mwenye dhamana anaweza akawa ni askofu mkuu ( arch bishop), sinior pastor, apostor, papa (pope kwa wakatoliki) N. K. Kwa hiyo kama ningeliweza kuchora muundo huu ningelianza na nafasi/ngazi ya kwanza kabisa ingelikuwa ni ngazi ya Mungu >Askofu mkuu > askofu wasaidizi> n. k.
Makanisa mengi hasa makanisa ya kiafrika yanatumia muundo huu. Kwamba yupo kiongozi mkubwa wa juu kama msemaji mkubwa wa kanisa au huduma. Aina hii ya muundo huitwa “Episcopal ” kwa lugha ya kitaalamu. Muundo huu umetokea wapi? Biblia imeeleza aina ya muundo huu;
Waamini kwenye kanisa la zamani ( watu kama Timotheo na Tito) walikuwa na mamlaka juu kusanyiko/ kanisa. Kwa mfano katika Tito 1,Paulo anamwambia Tito achague viongozi. Hii inaonesha Tito alikuwa ana mamlaka ya kikanisa dhidi yao.
Katika Ufunuo 2-3,tunaona neno “Kwa malaika wa.. ” hii ikiwa na maana kwa viongozi wakubwa waliopewa kuongoza na kusimamia kanisa.
Hivyo tunaweza kuona aina hii ya kwanza ya muundo wa kanisa. Ebu angalia muundo wa kanisa lenu upoje? Je mna kiongozi wa juuwengine chini yake ana viongozi wengine? Bila shaka yawezekana ndio mpo na viongozi wengine.
02. Ngazi ya kundi la viongozi. (Presbyterian)
Huu ni muundo wa kanisa ambao unaongozwa na kundi la viongozi waliochaguliwa au kuteuliwa. Kundi la viongozi hawa ndio wenye kufanya maamuzi ya mwisho. Kundi la viongozi /elders linaweza kuwa la viongozi 6 au zaidi ambao ni wenye mamlaka na uongozi mzima wa kanisa ambao chini yao katika muundo wapo viongozi wengine labda 20 au zaidi kisha chini ya hao ndipo mchungaji anafuatia alafu viongozi wengine wanafuatia katika kundi.
Hivyo nafasi ya mchungaji ipo chini kwa maana maamuzi makubwa hufanywa na kundi la viongozi / wazee wa balaza(elders). Kama mchungaji akitaka kutoa maamuzi makubwa ni lazima awaite viongozi wa juu au viongozi wa juu wakae na kutengeneza maamuzi kisha mchungaji ndipo atangaze.
“Presbyterian ” ni neno lenye asili ya kigiriki lililotokana na neno “ presbuteros= elder ” neno hili halina maana ya makanisa ya Presbyterian yaliyopo. Muundo huu utumika kwa baadhi ya makanisa hapa afrika na nje ya nchi pia. Biblia inasema nini katika muundo huu wa kanisa?
Viongozi wa kundi waliongoza makanisa huko Antiokia, Yerusalem, Filipi na Efeso.
Yakobo, Petro, Paulo na Luka wote hawa wameeleza kuhusu viongozi kuongoza makusanyiko. Kwenye Matendo 15,viongozi wa makusanyiko walifanya kazi pamoja na mitume kujibu maswali tatanishi yaliyoulizwa.
03. Ngazi ya kanisa kama kiongozi ( congregation)
Muundo huu ni ule kanisa ndio hutoa maamuzi ya mwisho. Hivyo ngazi ya juu ya kanisa ni watu kisha ngazi inayofuata ni viongozi kisha ngazi inayofuata ni mchungaji. Kama mchungaji akitaka kufanya maamuzi makubwa itambidi apeleke kwanza viongozi wake wa juu, kisha viongozi watawaita watu wa kanisa kisha watu wa kanisa wakisema ni sawa kwa jambo fulani walilolipitisha, ndipo viongozi watamwalifu mchungaji na mchungaji atalitangaza lasmi. Mfumo wa muundo huu hutumika hasa kwa makanisa ya magharibi na huko marekani lakini kwa baadhi ya makanisa.
Hivyo katika muundo huu ni kanisa kwa ujumla utawala kwenye maamuzi makubwa na sio mchungaji au bishop. Kanisa /watu ndio uangalia maendeleo mazima ya kanisa na ukuaji wake na nini kifanyike au nini kisifanyike. Muundo huu umeonekana kwenye baadhi ya maandiko kama vile;
Kanisa la awali/zamani, kanisa lilichagua watumishi 7 ( Matendo 6)
Kanisa la huko Antiokia lilipeleka Barnaba na Sauli (Matendo 13:1-13)
Kanisa lina nguvu ya kuwawajibisha wakosaji ( 2 Wakorintho 2:6, 1 Wakorintho 5:1 na kuendelea)
Katika miundo hii, unafikiri ni muundo gani unaodhani ni muundo mzuri kwako? Hata hivyo katika kila muundo una faida zake na mapungufu yake. Ikiwa kama umepata kitu, nifahamishe. Kwa huduma ya maombi pia piga namba hizi hizi + 255 683 877 900
ITAENDELEA…
What’s namba +255 746 446 446
Na Mch. G. Madumla.
UBARIKIWE.
Comments