top of page

ZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA.

Na Mch.G.Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Tafsiri ya neno “hodari”  ni hali ya kuwa shupavu,imara au shujaa. Uhodari tunaojifunza leo ni uhodari  katika Bwana si uhodari katika mambo maovu,maana inawezekana ukawa hodari wa mabaya!.  Biblia inazungumzia uhodari katika Bwana. Hivyo ni lazima tujue “uhodari katika Bwana” ukoje?

Uhodari katika Bwana;

Ni ile hali ya kukaza kuyafanya mapenzi ya Mungu yote kwa msaada wa Roho mtakatifu. Au ni hali ya kusikiza sauti ya Mungu kwa makini,na bidii;kutunza kuyafanya yote akuagizayo Mungu.  Sasa utagundua suala la kuwa hodari katika Bwana linamuhitaji sana Roho mtakatifu. Lakini swali la kujiuliza leo,kwa nini tuzidi kuwa hodari katika Bwana?

Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:10-12

Neno linakutaka “uzidi” kuwa hodari. Ikiwa na maana kwamba una uhodari fulani ndani yako,lakini sasa unahitajika uzidi katika uhodari huo . ( Ukiona neno hili “uzidi” limetumika,basi ujue lina maana ya kwamba upo kwenye ilo eneo lakini sasa uongeze kasi/uzidi. Uzidi katika uweza wa nguvu zake pia.)

Ukitafakari vizuri andiko hilo,utaona kuna mambo mawili unayoambiwa kuwa hadori nayo;

  1. Hodari katika Bwana

  2. Hodari katika uweza wa nguvu zake

Neno la kwanza “uwe hodari katika Bwana” lina maana uwe jasiri,shupavu,usiyeyumbishwa yote hayo yawe katika Bwana. Ni sawa kabisa na kile ambacho Bwana alichokuwa akimwambia Yoshua (Yoshua 1:9). Lakini jambo la pili,ni kuwa hodari katika nguvu zake Bwana. Hapa kilichobadirika ni neno “Nguvu” ambalo limenogesha sentensi nzima. Kwa nini nguvu? kwa nini asingeliishia kusema uwe hodari tu,ila katafuta neno “nguvu” alitumie hapo? n.k

Bila shaka Neno linakuonesha kwamba suala zima la uhodari hutegemea na kiwango cha nguvu ulichonacho (Kwa maana bila nguvu hakuna uhodari). Unajua Bwana anajua kiasi cha nguvu zetu kwamba kipo chini sana,na anatutaka tuongeze nguvu kwake hali akijua yale yajayo,kwamba bila nguvu zake hatuwezi chochote. Moja ya jambo lilopo kwa kila mtu ni “vita” jambo hili linahitaji nguvu hasa kwa Bwana ili ushinde.

 Tujifunze kwa mfano huu;

Mwanariadha yeyote anapoanza kukimbia mbio ndefu,kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili aweze kushinda. Moja ya jambo muhimu ni kuanza kukimbia kwa taratibu/pole pole bila kasi kwa maana anajua mbio zake ni ndefu. Lakini jambo la pili ni kuona “ushindi” hata kabla hajamaliza mbio. Ni kawaida kabisa kwa mwanariadha kuona hivyo,ili kusidi kukamtie nguvu zaidi ya kukimbia.

Na ndivyo ilivyo Ukristo ni mbio ndefu zinazohitaji mipango mikakati ya namna ya kuanza na kuendelea kukimbia huku moyoni ukiamini kwamba utashinda tu,na kupewa taji.

Unajua,bila kukomaa katika Bwana,kamwe huwezi kushinda hata katika  hilo unalopitia sasa. Mungu hupendezwa na wakomavu katika Yeye,na wala hapendezwi na mkristo mwenye kukata tamaa na kulia lia.

1.Uhodari wa Eliya Mtishbi.

Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi (Yakobo 5:17). Aliyekuwa amekaza mno kwa Bwana hata mwishowe alitwaliwa ( 2 Wafalme 2:11).  Ukitizama uhodari wake pale alipowaua manabii wa baali mia nne na hamsini. Na baada yapo alimwendea Ahabu na kumwambia ainuke,ale na kunywa sababu sasa kuna mvua ( Maana Eliya alisimamisha mvua isishuke  muda wa miaka 3 na nusu). Lakini hapakuwa na mvua bado,kwa sababu alitakiwa azidi kuwa hodari katika Bwana kwenye maombi,imeandikwa;

Basi Ahabu akainuka ili ale na kunywa. Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini.Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akanena, Enenda tena mara saba.Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie. Ikawa, muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanyesha mvua nyingi. Ahabu akapanda garini, akaenda zake Yezreeli.” 1 Wafalme 18:42-45

Eliya akiwa katika maombi,anataharakishwa amwambie mtumishi wake aende akatazame kama kuna mvua,maana yeye Eliya ameiona mvua. Lakini kumbe mvua hajaonekana katika macho ya damu na nyama,mtumishi wake haioni mvua!!!  Na mtumishi wa Eliya anapanda mara mbili kutazama mvua na wala haioni kabisa hata mara ya saba anaona kiwingu kidogo mfano wa mkono wa mtu.

Haikuwa jambo jepesi kama Eliya asinge kuwa shupavu katika maombi. Yamkini angeliomba kidogo tu,alafu mtumishi wake akampa majibu yale yale kwamba hakuna mvua. Basi ni dhahili mvua isingekunya juu ya nchi. Matokeo ya mvua yaliletwa na bidii ya kuomba kwake Eliya akiamini kwamba kuna mvua inakuja,nayo ni mvua kubwa. Tatizo sio mvua kuja bali tatizo ni hali ya uhodari katika Bwana iletayo matokeo ya mvua.

Leo,jiangalie wewe mwenyewe jinsi unavyoenenda kwa Bwana,Je unaenenda katika uhodari?  Je wewe ni shupavu katika Bwana n katika maombi ?  Umeomba mara ngapi juu ya hilo tatizo/shida kiasi cha kutokujibiwa? Mbona umekata tamaa mapema? Au unafikiri kuomba kwako kumetosha,kiasi cha kuacha kuomba? Jifunze kwa Eliya aliomba mara nyingi zaidi ingawa aliona majibu lakini alikaza kuomba hata majibu yakajidhihirisha katika ulimwengu wa mwili.Watu wengi wamekata tamaa!!! Wakidhani ya kwamba Mungu hawasikii,kukata tamaa ni dhambi mbele za Mungu.

02. Uhodari wa Daudi mwana wa Yese.

Habari za Daudi ni habari nzuri za kujifunza siku ya leo,ili zikutie nguvu. Maisha ya Daudi akiwa mtoto wa nane wa mzee Yese yanatofautiana na maisha ya kaka zake akina Eliabu. Kigezo kimoja wapo cha utofauti wao kilikuwa ni kwamba;moyo wa Daudi ulimpendeza Bwana (Matendo 13:22),pia Daudi alikuwa hodari. Tunamuona Daudi akimuua simba na dubu,(mnyama hatari wa polini),akipambana na wanyama wengine. Kama asingelikuwa hodari asingeliweza kupambana namna hiyo.

Daudi alimshinda Goliathi,anasema Daudi “Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.” 1 Samweli 17:36

Hivyo; mambo mengine hayatoki bila ukomavu katika Bwana. Ukiwa jasiri katika Bwana na uweza wa nguvu zake,ujue hakuna jambo litakaloshindikana kwako. Kwa msaada zaidi na maombi nipigie sasa; +255 683 877 900

What’s app number ni +255 746 446 446

Mch.Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page