UKOMBOZI WA KIFIKRA – 02 ( tamati)
- Mch. Gasper Madumla
- Mar 27, 2020
- 2 min read
Updated: Aug 30, 2022

02. Mtazamo usiofaa
Mtu aliyefungwa akili/fikra zake,kawaida hutazama vitu tofauti na uhalisia wa vitu hivyo. Hata maamuzi yake ni ya kushangaza,kwa sababu ndivyo aonavyo nafsini mwake. Kumbuka; Waisraeli nao walikuwa na mtazamo usiofaa,kinyume kabisa na alivyokuwa akiona Bwana,kwa maana bado walikuwa na utumwa katika akili zao kiasi kwamba hawakuweza kuwa chanya katika mtazamo wao.
Na hii ni moja ya silaha kubwa anayoitumia adui,ili afanikiwe atakayo juu wa watoto wa Mungu. Ebu cheki mfano mmoja pale ambapo Musa alipowatuma wapelelezi 12,kuipeleleza nchi ya ahadi,biblia inasema wapelelezi 2 tu (Kalebu na Yoshua) miongoni mwa wale 12,walikuwa na mtazamo sahihi,lakini waliobakia 10 walikuwa na mtazamo usiofaa,hivyo wakawatisha watu kwa taarifa zao walizotoa (Soma Hesabu 13 yote)
03. Kushindwa kuona mbali.
Mara nyingi watu waliofungwa fikra zao hawawezi kuona mbali,bali huyatazama mambo ya sasa tu. Ni kweli sio wote wanaoshindwa kuona mbali watakuwa wamefungwa kiakili bali sehemu kubwa ya watu wanakuwa na shida ya kufungwa akili zao. Na kutoka kwao ni mpaka wakombolewa kiakili!!!! Imekuwa ajabu kwamba leo waliookoka ndio kundi kubwa la watu waliofungwa fikra zao,kiasi kwamba hawaoni mambo mengine isipokuwa wanaona sana ya kiroho tu. Kuona mbali ni tofauti na “malengo’‘ kwa maana unaweza ukawa na malengo lakini pia ukashindwa kuona mbali.
Nani awafungaye watu fikra zao?
Biblia inatupa sababu chache ambazo kwa hizo mtu hata ufungwa fikra zake. Moja ya kitu/sababu ya kufungwa ni ile ya shetani ambaye huitwa “mungu wa dunia hii”,yeye mara zote huakikisha anafunga akili na fahamu,usije ukaamini – 2 Wakorintho 4:4.
Pili sababu nyingine zinatokana na mtu binafsi,mfano “kukosa maarifa” ni sababu kubwa sana ya kufungia fikra zako. Wengine wamejikuta wakiwa hawawezi kutoka kiakili kwa sababu si watu wa maarifa kabisa. Maarifa ? yanatokea wapi? Maarifa ni habari / elimu juu ya kitu/mambo/maisha. Kuna maarifa ya kwanza ni yale ya kiroho,na ya pili ni ya kimwili / elimu dunia juu ya vitu na mambo mbali mbali.
Sasa utagundua kwamba si wengi ni watu wa maarifa ya Neno la Mungu,lakini pia si wengi wenye maarifa za mambo mengine. Kwa kukosa tu maarifa muhimu,basi umekosa habari muhimu na hatimaye kuna mambo hujayajua na kwa hayo yamekwamisha akili/fikra zako kwenye eneo moja.
Wapendwa wengi tunachangamoto ya kuwa mbali na vitabu,bali tunapenda biblia tu. Na hatimaye tumekuwa si wasomaji wa vitabu vingine,kwa kufanya hivyo tu,huwezi kuelewa zaidi na hatimaye utakuwa umefungwa usielewe mengi. Biblia inatuambia hata Danieli kwa kuvisoma vitabu (Danieli 9:2).
Alipata maarifa yaliyofungua akili na ufahamu wake,kisha akatambua mambo mengi,na kuchukua hatua mara moja ya kutoka mahali alipo. Wewe je,unasoma vitabu? Ni kwa namna gani unasoma vitabu? Ni vitabu vingapi umejiwekea ratiba ya kuvisoma? n.kBahati mbaya;Wengine hata biblia kitamu mama kinachowahusu,hawajawahi kukisoma na kukimaliza mpaka leo tangu aokoke miaka mingi iliyopita.
Sasa unategemea utafungukaje? Je hujui kuna mambo huwezi kuyaelewa mpaka usome?
Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,basi nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja.
Lakini inawezekana labda unahitaji MAOMBI kwa maana nawe unapitia changamoto hii,Basi kwa yote nipigie sasa kwa + 255 683 877 900
What’s app namba ni +255 746 446 446
Na Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comentários