top of page

YESU NI MUNGU KAMILI NA MWANADAMU KIMILI ~ 2 ( tamati)

Updated: Sep 29, 2022


…kitendo cha kuitwa “mwana wa Mungu” kinaonesha hali yake ya uungu alionao. Huku uswahili kwetu ( Tz) tunamsemo usemao “mtoto wa nyoka ni nyoka” msemo huu ni wa wahenga ambao walikuwa wakijaribu kusema kwamba mtoto wa nyoka ana tabia sawa na nyoka mkubwa,wanafanana hata tembea yao. Ni sawa na kusema ukimwona mtoto wa nyoka,umemwona nyoka! Kwa maana wote ni nyoka,tofauti yao ni – mmoja ni mkubwa na mwingine ni mdogo. Biblia imemfunua Kristo katika uungu wote aliokuwa nao,kitu ambacho hakuna mwanadamu yeyote aliye na uungu wote kama Kristo Yesu,


hakika huyu ni Mungu kamili. Lakini hata hivyo,biblia inamwelezea kuwa Kristo alikuwa ni mwanadamu kamili.

Tofauti kubwa katika uanadamu alionao Kristo na uanadamu wa kawaida upo katika eneo la asili ya dhambi / nature of sin kwa maana Yeye hakuwa na dhambi,wala hakutenda dhambi / hakuwa na hasili ya dhambi ( 2/Wakorintho 5:21,Waebrania 4:15), bali sisi wengine tumezaliwa ndani ya asili ya dhambi kwa kukosa mtu mmoja ( Adamu).


Hali ya utu / ubinadamu wa Yesu unaanzia kutajwa mwanzo wa injili ya Mathayo,pale tunaposoma ukoo wa Daudi / A record of the genealogy of Jesus Christ,Yesu anatajwa kama “mwana wa Daudi / the son of David” – Mathayo 1:1


Ile namna ya kutajwa kuwa sehemu ya ukoo wa Daudi inamtambuliza kwamba na Yeye Yesu alizaliwa. Hii ndio sehemu ya kwanza ya kumtambulisha Yesu kama mtu aliyezaliwa na mwanamke. ( Soma kuzaliwa kwake Mathayo 1:18-25)


  • Kusudi la Yesu kuzaliwa kama mwanadamu.


Tunaweza kuyaona mengi yaliyo ndani ya Kristo hata kuwa mfano wa mwanadamu, lakini kusudi lilikuwa ni moja tu nalo ni “ukombozi kwa watu wote” Wagalatia 4:4-5. Ujio wake ulilenga kukomboa waliopotea,watu wote walikuwa wamekwisha potea. Yesu akaja kukomboa,hii ina maana kitendo cha kufanyika mwili,ni kuudhihilishia ulimwengu kwamba Yeye ndiye njia,kweli na uzima ( Yoh.14:6),ulimwengu ujue kwamba wokovu una Yeye tu,na upo halisi. Asingelivaa mwili,wokovu usingelipatikana. Yeye amekuja kutafuta na kuokoa kilichopotea ( Luka 19:10)


Shuhuda kumi zinazomweleza Yesu kuwa alikuwa pia ni mwanadamu 100%.(Udhihilisho wa ubinadamu aliokuwa nao) nazo ni;


  1. Alihuzunika / sorrow – Mathayo 26:37

  2. Kuna kipindi aliona njaa – Luka 4:2

  3. Akuna wakati alilia / wept – Yoh. 11:3nk

  4. Alikuwa na mwili wa kawaida, mwenye mikono,miguu n.k – Luka 24:39

  5. Kuna kipindi alikuwa ni mtoto alipozaliwa na akapitia hatua zile zile za ukuaji – Luka 2:40

  6. Kuna kipindi alichoka – Yoh.4:6

  7. Aliteswa,(alidharauliwa na kukataliwa) – Isaya 53:4-5

  8. Alilipa kodi – Mathayo 17:27

  9. Kuna wakati alikwenda harusi – Yoh.2:2

  10. Alikuwa na mama yake mzazi,pamoja na ndugu zake wa damu na nyama – Marko 3:31


Pamoja na hizo kuna shuhuda nyingi zinazomdhihilisha Yesu kuwa alikuwa mwanadamu. Yesu anaitwa “ mpatanishi” ,Yeye ni mwanadamu Kristo Yesu ( 1 Timotheo 2:5). Hivyo ukija kusoma / ku – study habari za Kristo Yesu, utagundua / uta – observe kwamba Yesu alikuwa 100% Mungu na 100% mwanadamu. Ili Mungu atufundishe stadi za maisha alitufundisha kupitia Kristo Yesu, vile alivyoishi ndio mfano halisi wa mtu wa Mungu anapaswa awe.


UBARIKIWE.


Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900


Na.Mch. G.Madumla


Whatsapp namba +255 746 446 446


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page