MELKIZEDEKI MFALME WA SALEMU.
- Mch. Gasper Madumla
- Jul 7, 2022
- 2 min read
Updated: Aug 29, 2022

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Waebrania 7:1 (KJV) “ Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;”
Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, akiwa katika Bonde la shawe, Melkizedeki mfalme wa Salem akamjia pamoja na mkate na divai ( ishara ya meza ya Bwana kwa maana huyo Melkizedeki ni kuhani),Kisha Akambariki Abramu,naye Abramu akamtolea fungu la kumi la nyara alizokuwa nazo.
Ilikuwaje mpaka Ibrahimu kumtolea fungu la kumi Melkizedeki?
Bila shaka Ibrahimu kuna kitu alikiona ndani ya Melkizedeki,naye alishuhudiwa kwamba Melkizedeki hakuwa mtu wa kawaida kiasi kwamba Ibrahimu akajua namna ya kuchota baraka kwake. Kumbuka,Ibrahimu alikuwa mtu wa imani mwenye uwezo mkubwa wa kumsikia Mungu na kuona kiroho.
Alipomwona Melkizedeki alitambua nafasi ya Melkizedeki kama kuhani wa Mungu Aliye juu sana naye akagundua ni amekutana na kuhani mkuu,mkubwa zaidi yake kiroho na ndio maana Melkizedeki alimbariki Ibrahimu ( kwa maana mdogo hubarikiwa na mkubwa- Waebrania 7:7).
Hivyo Ibrahimu alitembea katika kanuni ya unyenyekevu,na kukubali kutoa fungu la kumi Kwa Aliye juu sana zaidi yake.
Nani hasa huyu Melkizedeki?, Ni malaika?
Kusema ukweli ukuhani wa Melkizedeki ni ukuhani wa ajabu sana kutajwa katika maandiko matakatifu kwa sababu ukuhani wake unatajwa kwenye kipindi cha mwanzo sana enzi za Abramu hata kabla ya Abramu hajawa Ibrahimu, kipindi cha kale. Haijawai kutajwa ukuhani wowote katika kipindi hicho isipokuwa Melkizedeki peke yake. Pia biblia haielezi kwamba Melkizedeki ni malaika, lakini tafsiri ya kupitia tafsiri ya jina lake kama ilivyoandikwa katika Waebrania 7:1-3 tunaweza kujifunza machache
∆ Kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
Ukuhani wake Melkizedeki unatajwa ni ukuhani uliotukuka,pia ni ukuhani wa milele – Zab.110:4 sifa hii ya kikuhani ni ya kipekee kabisa kwa maana hakuna kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu kama Yesu Kristo ( Waebrania 4:14). Ukuhani wa Yesu umefananishwa na Melkizedeki.
∆ Mfalme wa Salemu
Maana yake ni mfalme wa amani – Naye Yesu ndiye hasa uweza wa kifalme upo begani mwake,yeye ni mshauri wa ajabu,Mungu mwenye nguvu,Tena huitwa Baba wa milele,na “ Mfalme wa amani“- Isaya 9:6. Ukweli ni kwamba hakuna ambaye mfalme wa amani isipokuwa Yesu Kristo pekee. Hivyo,sifa hii ya Melkizedeki ni sifa maalumu ya Yesu.
∆ Mfalme wa haki.
Hii ni tafsiri nyingine ya Jina la Melkizedeki yenye kueleza moja kwa moja sifa ya Kristo Yesu kwamba ndiye pekee mfalme wa haki. Huitwa “ MUNGU mwenye haki“. Yesu mwenyewe,hivyo Yesu Kristo si tu mwenye haki,Bali Yeye mwenyewe ndio haki na ndio maana ukimpata Yesu umeipata haki.
Pamoja na mfanano huo na Yesu lakini tunaweza kumwona Melkizedeki kama kuhani aliyepata kuwepo bila kuwa na taarifa za msingi za familia yake. Hivyo biblia hakurekodi kizazi cha Melkizedeki kwa sababu hiyo Melkizedeki hana baba wala hana mama,wala hana wazazi.
Haujulikani siku zake hivyo,hana mwanzo wala hana mwisho wa siku zake,naye amefananishwa na Yesu Kristo ambaye hakika hana mwanzo wala hana mwisho wake.
Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.
Na Kwa msaada zaidi unipigie simu Kwa+255 683 877 900
What’s app number +255 746 446 446
Na Mch. Gasper Madumla.
UBARIKIWE .
Kommentare