top of page

YESU NI MUNGU KAMILI NA BINADAMU KAMILI – 01

Updated: Sep 29, 2022



Uungu na ubinadamu wa Kristo Yesu / Christ’s divinity – humanity


a)Uungu /Yesu ni Mungu.


Biblia inamwelezea Kristo Yesu kuwa ni Mungu asilimia mia moja. Moja ya sifa kuu aliyonayo yenye kueleza uungu wake ni sifa ya umilele aliyokuwa nayo ( Yoh.1:1-4,14). Hakuna yeyote mwenye sifa ya umilele isipokuwa Mungu tu,hata shetani hana umilele kwa maana yeye alikuwa ni malaika,na malaika wote waliumbwa na Mungu,kwa hiyo kuna siku moja wote waliumbwa pamoja naye ibilisi. Ni mungu tu ambaye hakuumbwa,Kristo naye anasifa hiyo hiyo kwa maana alikuwepo kabla ya huo Mwanzo (Mwanzo 1:1-3),kwa maana katika huo mwanzo Kristo alikuwepo,huyu ni Mungu hakika. Lakini nikupitishe kwenye vielelezo vya kina,kama ifuatavyo;


i) Maneno yake;

  1. Yeye na Mungu ni mmoja – Yoh.10:30

  2. Ukimjua Yesu ,umemjua na Baba – Yoh.14:7-9

  3. Yeye ni ndani ya Baba na Baba ni ndani yake -Yoh.14:10

  4. Yote aliyonayo Baba ni ya Yesu pia – Yoh.16:15

  5. Soma pia Luka 22:69,70 – Uungu alionao.


ii)Ushahidi wa mitume;

  1. Yeye ni Bwana – Warumi 1:4

  2. Ni Mungu mwenye kuhimidiwa – Warumi 1:5

  3. Ni Mungu,na wa kwanza katika viumbe vyote – Wakolosai 1:15

  4. Yeye ni Mungu mwenye siri zote – Wakolosai 2:2

  5. Utimilifu wote wa Mungu unakaa katika Yeye Kristo – Wakolosai 2:9

  6. Mungu aliyejidhihirisha katika mwili – 1 Timotheo 3:16

  7. Yeye ni mng’ao wa utukufu wa Mungu – Waebrania 1:3

  8. n.k Kama nabii Isaya kaandika mengi kuhusu uungu wa Yesu,soma kitabu cha Isaya.


iii) Roho chafu nazo zilimshuhudia kwamba hakuwa mwanadamu wa kawaida,bali mwana wa Mungu/hakuweza kutofautishwa na Mungu;

  1. Mwenye kuwatesa mapepo na roho chafu – Mathayo 8:29

  2. Yeye ni mtakatifu wa Mungu,mwangamizaji wa roho chafu – Marko 1:24

  3. Hata mapepo yalimtambua – Luka 4:41


iv) Uwepo wake,alikuwepo kabla ya vyote;

  1. Yeye ni wa milele – Mika 5:2,Yoh.1:1

  2. Alikuwepo kabla ya Ibrahimu – Yoh.8:58

  3. Alikuwepo kabla ya Yohana mbatizaji – Yoh.1:15

  4. Alikuwepo kabla ya ulimwengu kuwapo – Yoh.17:5

  5. Ni Kuhani wa milele – Waebrania 7:3

  6. Yeye ni mwanzo na mwisho,wa kwanza na wa mwisho – Ufunuo 22:13

  7. N.k


v) Ni Bwana na mwenye mamlaka.

  1. Mamlaka yote ya mbinguni na duniani ni yake – Mathayo 28:18

  2. Bwana mwenye kutiisha mapepo – Marko 1:27

  3. Hakika ni Bwana – Luka 6:5

  4. Ndiye Kristo na Bwana – Matendo 2:36

  5. N.k


Hata hivyo,Yeye ni mtawala mkuu juu ya kanisa,katika hasili,ulimwengu,mbinguni na kila eneo. Sifa ya utawala wa mahali pote ni sifa ya kiungu pekee,kwa maana hakuna awezaye kutawala kila eneo isipokuwa Mungu tu,Kristo Yesu naye hutawala kila eneo. Ukiweza kuyapitia maandiko hayo hapo juu yenye kumwonesha Kristo kuwa alikuwa 100% Mungu,ufahamu wako utabadilika. Siri ipo hapa; “Bwana Mungu,amelichagua jina la Yesu Kristo,watu wote waombe kwa jina hili,kwa kuwa ndio jina lake Yeye mwenyewe (Waefeso 5:20),Hii ni siri ya ajabu. Hilo ndilo jina linalotuokoa (Matendo 4:12).

ITAENDELEA…


Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900


Na.Mch. G.Madumla


Whatsapp namba +255 746 446 446


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page