top of page

YESU ANAKUITA JINSI ULIVYO!

Updated: Sep 2, 2022

“ cha pombe ” anaweza akaokoka na kuwa mtu mwingine.



Hivi unajua mtu aachi pombe ndipo aje kwa Yesu,Bali Yesu umwita mtu jinsi alivyo,naye ndiye mwenyewe kumbadilisha” Yesu anakuita vile ulivyo!!!

Duh! Hiyo kali kwa kweli,…Nzuri sana… 🙆🙆👊👆


Je ujawahi kusikia mtumishi akikemea watu au mtu fulani kwamba anatakiwa aache pombe ndipo aje kanisani? Au wakati mwingine waweza kusikia mtumishi akimwambia kwa ukali binti fulani wa kimataifa“kama huwezi kuja kanisani na nguo ndefu,basi baki huko huko bar!!!. ” au hujawahi kuona mtu akilazimishwa aache kitu fulani ambacho kwa kweli ni chukizo kwa Mungu, ili aokoke! Sasa hivyo ndivyo watumishi wengi husema, na Wamesahau kwamba anayemwezesha mtu fulani kuacha dhambi au uovu ni Mungu. Tena watu hawawezi kuacha dhambi kwa akili zao binafsi.

Kama kweli anayekuwezesha kuacha dhambi ni Mungu basi ni dhahiri kabisa unamwitaji kwanza Mungu kisha Mungu akuwezeshe kuacha dhambi. Unajua ukimuhubiria mlevi aache pombe kisha ndipo aje kwa Bwana mimi nataka nikwambie hawezi kuacha pombe na hakika utamkosa huyo mtu kwa sababu si yeye awezaye, bali Roho mtakatifu ndiye awezaye kufanya kazi hiyo isipokuwa mwenye dhambi aoneshe kuhitaji msaada huo ili asaidiwe.

Hata wewe usije ukajisifia kwamba umeacha uchafu wako uliokuwa ukifanya hapo mwanzo kwa sababu ni mjanja sana. Sio kweli!


Bali pale ulipoamua ukaweka nia, Mungu akakusaidia katika hilo. Lakini ujue hata kitendo cha kufanya maamuzi hayo, Mungu alihusika sana. Kumbuka tunaokoka kwa neema kwa njia ya imani katika Kristo Yesu ( Waefeso 2:8).

Kanisa la leo limewakosa watu wengi walio dhambini kwa mafundisho manyonge yanayofundishwa, na matokeo yake tumejikuta tukihubiriana sisi kwa sisi na sio kwa walio nje tuwalete kanisani.


Naikumbuka ile sheria ya dini yangu ya zamani kabla ya kuokoka, kasheria kalikuwa ni kazuri kwa kweli lakini kiroho sheria hakusaidia chochote. Maana kule kanisani kulizuia wanawake wote wenye kuvaa nguo fupi,na ikionekana kama kuna mmoja kavaa nguo fupi basi alikuwa akifunikwa na kikoi/mtandio  👭.


Wanaume nao walitakiwa kuvaa mavazi ya heshima. Hili lilikuwa ni jambo zuri kimwili,kwa maana kwa sehemu fulani jambo hili lilikuwa likifundisha maadili mazuri na kumweshimu Mungu na madhabahu yake. Lakini ukumbuke,tangazo la kuwazuia wote waliovaa ovyo wasiingie kanisani,katazo hili linaweza kutafsiriwa kwamba,


kila mmoja anayetaka kuja kanisani ni lazima awe safi kimavazi,kitu ambacho ni kibaya,kwa maana Yesu hafanyi kazi hivyo,Bali Yesu hutuita sote jinsi tulivyo hivyo hivyo bila kujali mavazi wala tabia zetu. Yesu anakuita jinsi ulivyo,ni Yeye ndiye mwenye kukurekebisha!

Wainjilisti wafanye nini?

Wainjilisti wote wana kazi ya kuwaita watu kwa Yesu jinsi walivyo. Mwaliko huu uwafikie kwa watu wote mahali popote bila kuwepo kwa kipingamizi chochote. Mazingira ya nje yasikwamishe watu kufikiwa au kuletwa kanisani. Hii ina maana hata kama ni mtu mhuni,jambazi n.k anapaswa afikiwe na kuletwa kanisani hivyo hivyo alivyo then Yesu atambadilisha.


Kanisa liwapokee watu wa kila namna kwa maana kanisa ni mahali pa makimbilio ya watu wema na wabaya,tena hasa wabaya wanaohitaji uponyaji. 

💡Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi + 255 683 877 900

Na Mch. G. Madumla.


What’s app ni +255 746 446 446


UBARIKIWE.

Recent Posts

See All
JIANDAE NA MAFUNDISHO YAJAYO.

“ Shalom mpendwa… Ninajua ya kwamba umekuwa ukifuatilia masomo mengi katika uwanja huu. Mungu azidi kukubariki na kukuinua. Tulikuwa...

 
 
 

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page