top of page

USIYAKUMBUKE MAMBO YA ZAMANI !

Updated: Aug 30, 2022


Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.” Isaya 43:18 (KJV)


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,


Ukweli ni kwamba hatuwezi kuyasahau yale ya kale tuliyoyapitia kwa maana tumeumbwa kwa namna ambayo tunaweza kukumbuka mambo ya zamani. Mfano; ikiwa hapo nyuma ulikuwa na maisha ya anasa,si rahisi kuyasahau maisha hayo Kwa Sasa maana akili na ufahamu wako unakumbuka vizuri. Na sio vibaya kukumbuka wapi ulipotokea ili kusudi kwa maisha uliyonayo sasa uweze kumpa Mungu utukufu.


Biblia inaposema“ usiyakumbuke mambo ya zamani,tena usiyatafakari” Ina maana usitumie muda wako mwingi katika mambo yaliyopita,na kutamani kubaki katika mambo hayo ya zamani. Au usikae katika mambo ya zamani/ don’t dwell on the past! ( Lakini pia Neno linasema “ ukiwa ndani ya Kristo,ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya! ” 2 Wakorintho 5:17)


Angalia mfano huu;


Israeli baada ya kutolewa Misri Kwa mkono wa Bwana wenye nguvu,ilifika wakati wakaanza kuyakumbuka mambo ya Misri ambayo yalikuwa ni mambo ya zamani kwao. Mara kadhaa walimnungunikia Musa,na Bwana alikasirika na hatimaye aliwaangamiza kwa tabia ya kuyakumbuka tu mambo ya zamani yasiyokuwa na faida kwao. Kwa sababu ya kuyakumbuka na kuyatafakari mambo ya zamani / ya Kimisri wakajikuta wakiingia katika tamaa mbaya iliyowatia hatiani ! 


Kumbe!

tamaa ya mambo ya zamani uliyoyatubia ” uchochewa na namna ya kuyakumbuka na kuyatafakari hayo mambo! Ebu soma katika Hesabu 11:4-5 uone namna ambavyo mkutano wa Israeli uliovyogubikwa na tamaa ya mambo ya zamani wakiwa huko Misri Bwana alikowatoa. Kisha wakaanza kumnungunikia Musa wakikumbuka nyama,samaki,matango ,matikiti maji ,mboga,vitunguu saumu. Lakini vyote hivi vilikuwa vya Misri!!! 


Katika utafiti wangu mdogo nilioufanya nikitafuta kujua kwa nini wapendwa wengi huanguka dhambi au hurudia dhambi zile zile mara Kwa mara. Niligundua kwamba walio wengi huwa na tabia ya kuyakumbuka sana mambo ya zamani tena na kuyatafakari. Kwa kufanya hivyo,wanafungua mlango Kwa adui kuwarudisha Misri/kuwaangusha katika dhambi na makosa yale yale waliyoyatubia!


Mfano;

fikiria mtu ambaye alipokuwa huko Misri/duniani alikuwa ni mzinzi wa kawaida tu! Alafu,akapata Neema ya wokovu. Lakini katika wokovu wake akachukua muda wa kukumbuka namna alivyokuwa anatoka na kwenda uzinzini. Uwe na uhakika mtu huyo hawezi kuchukua muda katika wokovu bila kuanguka katika uzinzi. Sasa huo ni mfano mdogo sana kati ya mifano mingi!


Matokeo ya kuyakumbuka na kuyatafakari mambo ya zamani


01. Kushikwa na tamaa 


Hakuna aliyebaki salama ikiwa kama mtu atayakumbuka mambo ya zamani mara Kwa mara na kuyatafakari hasa pale anapoona mambo ya Sasa hayaendi. Fikiria tena mtu ambaye kabla ya wokovu alikuwa ni mtu wa madili! ( Mtu wa mishemishe za kujipatia Mali Kwa njia ya udanganyifu) alafu akiwa anayatafakari maisha hayo sana na kujilinganisha na Sasa ambapo hakuna michongo ya namna hiyo maana ameokoka,ni rahisi kukamatwa na tamaa ya kurejea katika harakati zake za zamani pamoja na kwamba Yesu ni Bwana!


02. Kusumbuliwa na manung’uniko na malalamiko mara Kwa mara


Moja ya hali mbaya inayokwamisha malengo Yako ni kuishi Kwa malalamiko . Ndio maana leo kuna wapendwa ambapo wanapopitia katika changamoto basi hulalamika na kunung’unika hata wanafikia kusema “ Mungu mbona umeniacha” .

Sasa Swali linakuja amekuacha wapi? Kwani ulikuwa wapi? Bila shaka mtu anayesema hivyo ni yule aliyeyapima maisha yake ya kwanza hata kama alikuwa Misri na kuamua kulinganisha maisha yake ya Sasa akiwa nuruni,alafu anapongundua kwamba hapo mwanzo alikuwa vizuri ndiposa anahitimisha na Neno “ Mungu umeniacha!!!”


03. Kuchochea hasira ya Bwana


Israeli walipokumbuka Misri na kuyatamani ya Kimisri huku wakiwa wamesahau kwamba walishatolewa huko tena hawastahili kubaki Misri hata kama walikula nyama na samaki,siku ile tu walipoanza kuyatafakari na hatimaye kunung’unika Musa,basi hasira ya Bwana iliwaka na kuwateketeza ( Hesabu 11:1-2)

Hivyo,Kwa kuwa Mungu ni yule yule asiyebadilika,kuna hatari Sasa ya kufurikiwa na hasira ya Bwana. Pamoja na wema wa Bwana lakini Bwana Mungu si wakuzoeleka! 


Kumbuka;


Ikiwa mambo ya zamani yalikuwa ni mema na yakumpa sifa Bwana. Basi hayo ni mazuri na yafaa kwa mafundisho. Lakini kama ikiwa mambo Yako ya zamani yalikuwa hayampendezi Mungu basi uwe makini sana hata namna ya kuyasimulia,na tena haifai kubaki au kudumu katika hayo Kwa maana Kwa kufanya hivyo,waweza ukawaharibu wengine wanayoyasikia kama utayasimulia,uwe makini hapo.


Mfano ni huu;

Rafiki yangu mmoja alikuwa akiitwa “niga boy” enzi zake kabla hajaokoka. Alikuwa ni mhuni tu wa kawaida! Kwa Sasa ameokoka tayari,Sasa kuna muda akiwa anawasimulia watu kwamba alikuwa ni mhuni “a.k.a niga boy” na story nyingi za zamani na uchafu aliokuwa akiufanya. Kwa hiyo story zile za maisha ya dhambi zikawakaa waumini sana kuliko hata Neno alilokuwa anafundisha.


Na baada ya neno waumini walianza kumkwepa Kwa maana wengine walisema “nikiombewa na huyu nitapata roho ya uzinzi alivyokuwa nayo kabla ya kuokoka” na wengine walisema hivi hivi!!! Lakini ukumbuke hayo yote yalikuwa ni mambo ya zamani tu! Ila watu waliposikia wakayabeba kana kwamba ni mambo ya sasa! Umeona hatayari hiyo ya kuyakumbuka na kuyatafakari mambo ya zamani!!!!?


Lakini ukiyakumbuka Kwa lengo la kumwinua Bwana mahali alipokutoa,hivyo ni vyema sana. Lakini hata hivyo bado uwe makini sana na Nini unachokumbuka kwa maana si utaratibu wa kiungu huo. 


Songa mbele,angali wito wa Bwana!

Baada ya hayo yote, hakikisha una focus Kwa Bwana pamoja na kwamba ulipitia maisha fulani. Ukiwa na malengo ya kusonga mbele bila kuangalia nyuma ulikotoka ndio shabaha kubwa ya ushindi! 


Ikiwa umebarikiwa nifahamishe kwa +255 683 877 900

What’s app number ni +255 746 446 446


Na Mch. Gasper Madumla


UBARIKIWE.

Recent Posts

See All
JIANDAE NA MAFUNDISHO YAJAYO.

“ Shalom mpendwa… Ninajua ya kwamba umekuwa ukifuatilia masomo mengi katika uwanja huu. Mungu azidi kukubariki na kukuinua. Tulikuwa...

 
 
 

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page