JIANDAE NA MAFUNDISHO YAJAYO.
- Mch. Gasper Madumla
- Sep 29, 2018
- 1 min read
“ Shalom mpendwa…
Ninajua ya kwamba umekuwa ukifuatilia masomo mengi katika uwanja huu. Mungu azidi kukubariki na kukuinua. Tulikuwa mapumziko ya mwezi kama mmoja hivi,lakini sasa tumerudi tena.
Mafundisho yataendelea kurushwa / kuwekwa kuanzia mwezi ujao wa 10 ( siku chache tu). Nimekuwa nikipokea simu nyingi za watu mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi. Labda nikupe mwanga kidogo nikuoneshe wasomaji wazuri kwenye blog hii pendwa.
Nchi zinazoongoza kusoma mahali hapa. Zikishikilia tatu bora,ni hizi hapa;
Tanzania. ( inaongoza mara nyingi,ingawa si kila siku)
Marekani ( ni nchi ya pili kitakwimu inayoongoza katika wasomaji wake wanaotembelea hapa.
Uingereza (london hasa) Hapa pia kuna wasomaji wengi.
Makadirio ya watu 800 hadi 1000 kwa siku ujisomea blogu hii. Kati yao wameokoka kupitia blogu hii. Blog haiokoi mtu,bali blog imekuwa kama daraja la kuwaleta kwa Yesu. Wengine tumeweza kuonana na kufahamiana kupitia hapa,na wengine hatujaonana lakini wamebarikiwa sana. Ukweli ni kwamba ninakupenda wewe ambae huachi kupitia kwenye blogu hii kila siku.
Na sasa tutaendelea hivi punde…”
Comments