top of page

WALINZI JUU YA KUTA ZAKO ~ 01

Shalom…

Kwa ufupi.

  1. Mlinzi / Walinzi

Ukifanikiwa kwenda bank yoyote ile,kabla ya kuingia,hapo nje utaona mtu aliyevalia mavazi maalumu huku akishikilia bunduki. Tena ukiingia ndani ya bank,utaona mtu mwingine mmoja au zaidi ya mmoja waliojipanga sawa sawa,wenye kubeba silaha wakati wote.Na kama utakaa kihasara hasara,basi ujue utafuatwa na hatimaye utawekwa chini ya ulinzi. Watu wa namna hii walio makini,huku wamebeba silaha kali,huitwa “walinzi” hivyo “ mlinzi” ni mtu mkakamavu mwenye mafunzo / elimu ya kushambulia na kujihami,alindaye mali au fedha.

Siku moja nilimsindikiza rafiki yangu mmoja mchungaji mwenzangu,tulikuwa wachungaji watatu na tulikwenda kupatazama mahali aliponunua shamba mwenzetu. Ili uweze kufuka huko ilitulazimu tupitie kwenye kambi ya Jeshi ( lilikuwa eneo la mlandizi,jeshi la wananchi Ruvu). Na kwa kuwa tulitumia usafiri wa piki piki /boda boda,tulipofika kwenye lango la kuingia kambini,tulisimama tukaguliwe na mijamaa ya jeshi. Dah! “utii bila shuruti ” ndio kauli mbiu iliyoingia ndani yangu. Wale wanajeshi langoni,walitukagua na waliporidhika wakaturuhusu. Nami nikaanza kutafakari jambo hilo,kwa maana walionesha umakini wa hali ya juu kiasi kwamba kama tungeleta maneno yoyote basi nakwambia tungechezea makofi tu! Wanajeshi hao langoni,ni walinzi wa langoni. Lakini tulipoendelea mbele,tuliona wengine kwenye lango la pili,unapoingia ofisini kwao. Hii ni kuonesha wapo makini kwa jinsi gani.

  1. Swali la kujiuliza,kwa nini walinzi?

Nilikuwa na mtoto wangu wa kiroho mmoja ambaye alihajiriwa na mhindi mmoja. Kazi yake aliyoajiriwa ilikuwa ni kazi ya ulinzi. Cha ajabu katika kazi ya ulinzi aliyokuwa akiifanya,ni kulinda jengo lililobomolewa na hapakuwa na mali yoyote,tena katika eneo hilo kulikuwa na uzio wa fensi na geti kali kiasi kwamba hakuna mwizi yoyote angeliweza kuingia ndani,lakini hata hivyo ndani ya uzio huo hakukua na kitu chochote kile cha kukilinda,lakini cha jabu huyo mhindi boss akamwajiri kulinda magofu ya nyumba iliyobomolewa.!!! Hili jambo si la kawaida!!! Bali tunajua mlizi huitajika mahali penye mali au fedha. Lakini mahali pasipo mali au fedha yafaa nini mlinzi kuwepo? Hivyo tunapoona sehemu wamewekwa walinzi,tunatambua kwamba labda kuna mali,fedha au kuna umuhimu wa eneo hilo kulinganisha na maeneo mengine.

  1. Aina za walinzi.

Kuna aina mbali mbali za walinzi kulingana na nini kinacholindwa. Lakini pia katika ulimwengu wa roho wapo walinzi wa aina tofauti tofauti.Kwa mujibu wa biblia tunafahamu malaika ni moja ya kundi la walinzi wa kiroho. Lakini pia kuna walinzi wengine kama;

01. Bwana ni mlinzi.

“ BWANA ndiye mlinzi wako;BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.” Zab.121:5

Biblia inamtaja Bwana Mungu kuwa ndiye mlinzi wa kwanza na wapekee katika maisha yako. Ni yeye ndiye ambaye akulindaye usiku na mchana tena akulinda buree pasipo gharama yoyote ile. Laiti kama ungelijua gharama ya ulinzi japo wa lisaa limoja tu,ungelishangaa. Nenda kawaulize wale watu wa wenye magari wanayoyapaki na kuwakabidhi walinzi magari yao,cheki gharama wanayolipia kwa masaa tena.

Unajua,mimi nilipata neema ya kuwa mfanyakazi kwenye kampuni moja ya usafirishaji ( clearing and forwarding) ,nilipokuwa kule,kuna wakati tulikuwa tukilipia gharama za uhifadhi wa containers ( storage charges) kwa gharama za juu sana kwa siku ( tulikuwa tunalipia kwa dola (payments in terms of dollars). Halafu,sasa ninapoangalia jinsi vile Mungu atulindavyo buree,hatulipii gharama yoyote kwa dola wala kwa tshs,huyu Mungu mwacheni aitwe Mungu jamani. Nataka nikuoneshe kwamba,“Bwana ndiye mlinzi wa kwanza” ukumbuke kwamba “ mlinzi hawezi kulinda kitu kisicho cha thamani” hii inatuonesha kwamba wewe pia ni wa thamani machoni pa Mungu. Ulinzi atupao Mungu ni wa ajabu sana,kiasi kwamba hakuna awezaye kutoa isipokuwa ni yeye Mungu tu.

Wakati mwingine hutambui hata uendako,wala hauoni ni nini kilichopo mbele yako. Wakati mwingine hujui kwamba umetegwa,wabaya wamekuinukia ili wakumalize,lakini katika hayo yote unajikuta umevuka pasipo kudhurika hata katika moja. Lakini ukitafakari kama utapata kujua hata kidogo,utakuta ni mkono wa Bwana umekusaidia ( Zab.118:13)

Ni vyema ukijua kwamba Bwana ndiye akulindaye,wala sio mageti mkubwa nyumbani kwako,wala sio kwa sababu yoyote ile ya kibinadamu. Kwa sababu unalala salama na kuamka salama kwa sababu mkono wa Bwana uko nawe,kwa hivyo hivyo ulivyo tena wakati mwingine na makosa na dhambi zako,lakini bado wema wa Bwana umekuzunguka.

ITAENDELEA…

Kwa msaada zaidi +255 655 111 149/683 877 900/762 414 446.

Na Mch.G.Madumla

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page