top of page

PEMBE NA WAFUA CHUMA.

Updated: Aug 26, 2022




Pembe nne na wafua chuma wanne / Four horns and four craftsmen


“Nami nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, pembe nne. Nami nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Nini hizi? Naye akanijibu, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, na Israeli, na Yerusalemu.

Kisha Bwana akanionyesha wafua chuma wanne.

Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake;

lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.” Zekaria 1:18-21


Tafsiri ya neno “pembe” kibiblia huwakilisha “ utawala wa kimabavu” . Ni utawala wa kuumiza bila kujali. Utawala wa namna hii,hupelekea anayetawaliwa kutolewa katika nafasi yake bila kupenda,ni utawala wa kuua bila huruma hata utu. Ni kama vile utawala wa kidikteta! Mfano wake ni mnyama mwenye pembe imara anavyoweza kumpiga mnyama asiyekuwa na pembe mpaka akamwua bila kujali!!!


Kwa sababu tu mnyama mwenye pembe ameamua kufanya hivyo. Maono ya Zekaria yanatueleza kuhusu “pembe nne” kama tawala mbaya nne. Bila shaka tawala hizi ni Ashuru,Misri,Babeli, Umedi na Uajemi ( Umedi na Uajemi zinawakilisha tawala moja yaani Persia) zilizoinuka juu ya watu wa Mungu kwa kipindi tofauti tofauti kwa lengo baya la “ kutawanya ” utawala wa kimabavu wowote unapoinuka,kazi yake ya kwanza ni;


  • Kutawanya yaani kuleta “matengano / disunity “


Matengano,mafarakano na hali ya kukosa umoja wa watu wa Mungu ni kazi ya kwanza ya adui. Lengo la adui ( shetani) ni kututenganisha na Mungu na kututenga sisi kwa sisi ili kusudi kila mmoja awe peke yake na tukose nguvu kwa maana laiti kama tu pamoja tutakuwa na nguvu – “umoja ni nguvu ” watu wa Yuda walitawanywa na kila mmoja akawa na lake,wakapotezana.Pembe hizo leo zimechukua nafasi kubwa sana kuleta disunity katika utumishi wetu.


  • Kukandamizwa pamoja na utumwa.


Pembe hizo katika maono zilikuwa zinaelezea kuhusu ugandamizwaji wa uhuru pamoja na hali mbaya ya utumwa wa watu wa Mungu.

Pembe kama ya Ashuru alikamata Israeli (ufalme wa kaskazini) na kuhakikisha makabila kumi ya Israeli yanafutika na kupotea kabisa. Pembe hii ilishughulika na “kupoteza kizazi”. Katika ulimwengu wa roho kuna tawala za giza zinazoelekezwa kufuta kizazi/kabila hata kusababisha kabila kupotea kabisa . Hii ni pembe ya Ashuru. Lakini utumwa ulibebwa na pembe ya Misri.

  1. Pamoja na hayo,neema ya Bwana (Zaburi 132:17) , inaonekana katika maono ya Zekaria pale alipoona “wafua chuma wanne ” watakaokuja kushughulikia pembe hizo. Uzuri ni kwamba kila mfua chuma alikabidhiwa pembe yake,hivyo hakukisalia pembe hata moja isiyoshughulikiwa. Wafua chumba ilikuwa nguvu iliyokwenda kinyume na pembe. Bila shaka,wafua chuma waliwakilisha wateule wa Bwana ambao watakuja kushughulikia pembe hizo – 1 Wafalme 22:11


  • Mfua chuma wa kipindi hiki,ni wewe.

Bwana anamtafuta “mfua chuma” atakayesimama na kuziangusha pembe zinazowatawanya watu wa ukoo wako binafsi. Nguvu ya mfua chuma inatokea kwa Bwana,hivyo mfua chuma hana budi kujiungamanisha na Bwana kwa kazi ya kuangusha pembe.

Hivyo inawezekana watu wa kwenu wametawanywa na pembe,au yawezekana bado wapo utumwani / utumwa wa dhambi ( maana kuna koo ambazo wamekataa wokovu,na bado wanaabudu sanamu)

Hali ikiwa hiyo, unahitaji idadi ya wafua chuma iwe na uiano na pembe zilizoinuka. Kwa maana kila mfua chuma ahakikishe anaishughulikia pembe yake ipasavyo.Hii ni sawa na kusema suala la kushughulikia tawala mbaya zinahitaji nguvu kubwa ya umoja.

Ikiwa umebarikiwa, nifahamishe .


Pia kwa msaada zaidi,piga sasa + 255 683 877 900


What’s app +255 746 446 446


Mch. Gasper Madumla


UBARIKIWE

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page