top of page

WAJIBU MKUU KATIKA NDOA.

Updated: Aug 29, 2022



Unajua wengi hudhani kuwa “tendo la ndoa ” ndio hasa wajibu au kazi kuu katika ndoa. ( Ingawa tendo la ndoa lina nafasi yake muhimu katika ndoa) Lakini kuna wajibu mkuu katika ndoa,ambao Kila mmoja (mwana ndoa) akikaa katika wajibu wake mambo mengine yatatiki. Hivyo;


Katika ndoa kila mwanandoa ana wajibu muhimu kwa mwenzake sawa sawa na maelekezo ya Bwana Mungu kwa sababu ndoa ni taasisi yake Mungu mwenyewe.Wajibu au kazi zipo katika pande mbili kwanza mume ana wajibu mkuu kwa mkewe na mke naye ni vivyo hivyo,ana wajibu mkuu kwa mumewe. Kuna wajibu mkuu ambao kila mmoja Bwana amempa amtimizie mwenzake ili ndoa iwe ndoa kweli kweli.


  1. Mume,ampende mkewe. ( Waefeso 5:25)


Fimbo ya mapenzi alikabidhiwa mwanaume kama sehemu kubwa ya wajibu wake tena wajibu wa kwanza kabisa. Aina maana mke asimpende mumewe,hapana! Kila mmoja anapaswa ampende mwenzake, lakini mume amepewa “kumpenda mkewe “ kama kazi yake ya kwanza kuliko zote.


Katika kitabu cha Waefeso 5:25 – “ mume ampende mkewe kama Kristo alivyolipenda kanisa ” Tafakari vile ambavyo Kristo alivyolipenda kanisa, utagundua kwamba Kristo alikubali ,adharauliwe,asemwe , ateswe mpaka kufa kwa ajili ya kanisa,kwa Nini? Ni kwa sababu alilipenda kanisa. Kumbe ukipenda ! upo tayari kusemwa,kudharauliwa,n.k Kwa maana umependa.


Mume naye amepewa kazi ya kumpenda mkewe hata akubali kusemwa,kudharauliwa na hata kupata mateso kwa ajili ya mke wake. Unajua suala la kupenda ni suala la kiumeni? Maana mwanamke anaweza akawa hampendi kivile mwanaume fulani lakini akubali kuolewa naye ili mradi anapendwa na maisha yakaendelea mbele vyema kwa maana mwenye kutakiwa kupenda kwanza ni mwanaume.


Huo ndio utaratibu wa kiroho, lakini kama mwanamke ndiye apendaye kwanza,si vibaya ila lazima awe mwangalifu kwa maana hiyo nafasi anapaswa awe nayo mwanume kwanza.


  1. Mke,amtii mumewe.(Waefeso 5:22,1 Petro 3:1)


Mke akiwa msaidizi wa karibu kwa mumewe amepewa majukumu mengi kama vile kumpenda mume na watoto – (Tito2:4). Hasa lililo kubwa ni kujitiisha Kwa mumewe kama ishara ya kunyenyekea. Utii wa mke kwa mumewe ndio wajibu namba moja wenye matokeo mema katika ndoa.


mke akiwa mtii kwa mumewe atakula mema yote ya mumewe bila kuulizwa ulizwa. Kwa maana ya mume ni ya kwake pia. Kuna simulizi ya mwanadada aliyejifunga kifungo cha utii kwa mumewe kiasi kwamba mume alimpenda hata mali zake zote akaziandika kwa Jina la mkewe,mpaka akaunti za bank akaweka kitu kinaitwa “ equal power ” katika kuendesha account za kibenki. Si mchezo!! Jamaa kadata katika utii wa mkewe!!!


waswahili husema,mwanamke mtii ndiye anayemtawala mumewe! Hivi unajua hata Sara alikuwa na sauti kwa Ibrahimu kwa sababu tu alikuwa ni mwanamke mtii, maana kuna wakati Ibrahimu alijaribu kumkatalia wazo/ombi la Sara kisha Bwana akasema na Ibrahimu kwamba amsikilize Sara atakayomwambia na ayafanye hivyo hivyo, Je si kibali hicho ???( Mwanzo 21:12) 


But leo imekuwa ni shida,kwa maana wapo wake wamekosa kibali kwa waume zao kwa sababu si watiifu. Yaani imefika wakati mwanamke kama mwanaume, mwanume akipanda na mama/mke anapanda vile vile!!! Kelele mtindo mmoja!!! 

Hakuna jambo muhimu kwa mke kama kumtii mumewe. Utii haumaanishi udhaifu au hali ya kuwa mjinga bali ni kusikia sauti ya mume.


Hata katika maisha tu ya kawaida ukiwa mtii. Ikiwa mume atampenda kwa dhati mkewe na mke akawa mtii na mtulivu kwa mumewe basi matokeo yake ni furaha na amani katika ndoa itatawala. Tena mambo mengine yote yatafanyika katika raha ikiwemo “tendo la ndoa” 

Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.


Na kwa msaada zaidi unipigie simu Kwa+255 683 877 900


What’s app number +255 746 446 446


Na Mch. Gasper Madumla.


UBARIKIWE .

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page