UWEZO WA KUFANYIKA MTOTO WA MUNGU
- Mch. Gasper Madumla
- May 9, 2017
- 2 min read

Na Mch.Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi sana;
Imeandikwa ; “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;“Yoh.1:12
Kitendo cha kuokoka ni kitendo cha kuhamishwa kutoka katika utawala wa giza wa shetani na nguvu zake Kisha kuingizwa katika utawala mpya wa MUNGU baba.
Tendo hili ni la ajabu sana Kwa maana saa ile ile aliyeokoka anapewa uwezo mpya wa kufanyika mtoto wa Mungu. Kwa lugha nyingine shetani ananyanganywa na kupata hasara Kisha ufalme wa Mungu unafaidika Kwa ajili yako uliyeokoka.
(Pamoja kwamba kuna tafsiri nyingi katika mstari huo wa Yoh.1:12) Lakini Jambo muhimu la kuelewa ni kwamba kuokoka kunakupa uwezo wa kufanyika mtoto wa Mungu atakayeziridhi ahadi za Mungu. Hakuna njia mbadala wa kupewa uwezo huo isipokuwa ni Kwa kuokoka tu.
Neno “ Uwezo” lina maana ya nguvu,Kwa hiyo pale asemapo“ wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto..” Ina maana aliwapa nguvu ya uwana. Kama ujuavyo kwamba mwana halisi wa baba,yupo tofauti na mtumwa,mwana ni mrithi wa vyote.
Lakini ni vyema kufahamu kwamba,ukamilifu wa uwana hutegemea na kiwango chako cha ukuaji. Kama mwana atakua vyema basi ni dhahiri ataweza kumiliki mapema na katika uzuri na utaratibu.
Lakini kama mwana hataweza kukua na kubaki mchanga,basi ingawa ni mwana hapo hataweza kumiliki Mali ya baba yake. Kumbe ishu si TU kuwa mwana Bali kukua katika uwana. Leo tunashida hii,wengi ni Wana lakini hawana nguvu ya kumiliki Mali zile za baba yao. mfano:
nenda kasome habari za mwana mpotevu ktk kibabu cha Luka 15:31“ … na vyote nilivyonavyo ni vyako.” Biblia inaema kwamba , vyote alinavyo baba ni vya mwana,lakini je mwana anajitambua? Ana uwezo/ nguvu ya kumiliki?
Bila shaka yule mwana aliyebaki nyumbani katika Luka 15:1-32 alikuwa Hana uwezo wa kumiliki Kwa maana alikuwa bado hajajitambua kwamba vya baba yake ni vyake pia! Hivyo,Bwana anategemea aone Kila mtu aliyemwamini anapokea uwezo/nguvu ya uwana Tena na kujitambua.
Hali ukuaji kiroho ni muhimu sana katika uwana ulionao Ili kusudi usiendelee kubaki mchanga wa kiroho. Ukuaji hutegemea mambo machache. Kwanza kanisa ulilopo lina sehemu yake, lakini kikubwa ni bidii Yako binafsi.
Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi,maswali na ushauri. Tafadhali usisite kunipigia
Kwa simu namba +255 683 877 900
What’s app number ni +255 746 446 446.
Na Mch. Gasper Madumla
UBARIKIWE.
Comments