top of page

UTIMILIFU WA UNABII – 4

Updated: Aug 29, 2022


“nabii tatu zilizotolewa kipindi cha agano la kale na kutimizwa katika Kristo”

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,


Unabii haukuletwa kwa mapenzi ya mwanadamu,bali unabii uliletwa kwa mapenzi ya Mungu ukiongozwa na Roho mtakatifu – 2 Petro 1:21. Ikiwa unabii umetokana na mapenzi ya Mungu,basi ni lazima utimie katika nyakati zilizopangwa na Mungu. Kumbuka hapo Roho mtakatifu husimama kama kiongozi /director wa kila nabii ili kusudi kuleta utimilifu wa nabii zote.


Biblia imefurika nabii nyingi mno zilizotolewa na Bwana katika nyakati tofauti tofauti na hatimaye nabii hizo kukamilika ndani ya muda alioupanga Bwana wakati mwingine akiwatumia watu wake aliowavuvia katika kazi hiyo ya unabii. Katika wingi wa nabii hizo zipo nabii za agano la kale zilizotimizwa katika Kristo kwa sababu biblia yote inamzungumzia Kristo kama kiini / center .


1.Uadui dhidi ya shetani na uzao wa mwanamke.


Mungu mwenyewe aliyeweka uadui kati ya shetani  dhidi ya mwanamke na kati ya uzao wa shetani na uzao wa mwanamke (Mwanzo 3:15). Nataka uone hapo “shetani na uzao wake dhidi ya mwanamke na uzao wake’‘ . Jambo la kwanza unalopaswa kuelewa hapo,ni kwamba shetani ana “uzao” hii ina maana hayupo yeye peke yake bali ana uzao / wafuasi wake aliowazaa au kuwafanya na kuwamiliki,yeye na uzao wake utapambambana na mwanamke na uzao wake. Uzao wa mwanamke ni “ Yesu Kristo’‘ pamoja na uzao wake. Utimilifu wa unabii huu tunauona katika Luka 22:53 “ …hii ndio saa yenu na mamlaka ya giza…” Luka 4:1-13


2. Misihi atadharauliwa na kukataliwa katika mji wake.


Nabii Isaya alitabiri juu ya masihi wa Bwana kwamba atakaliwa,tadharauliwa tena watu watamkimbia hasa hasa wale watu wake mwenyewe – Isaya 53:3 . Unabii kama huu haupendezi lakini ndio unabii ambao ulitimizwa kwa Kristo Masihi wa Bwana. Utimilifu wa unabii huu tunauona sehemu kadha kama vile Mathayo 13:57, Yoh.1:11. Ukumbuke watu walioandikiwa wampokee masihi ndio waliomsulubisha,hii ni kuonesha walimkataa lakini kumbuka – jiwe walilolikataa waashi ndilo limekuwa jiwe kuu la pembeni!


3. Mwana wa Daudi kuwa mponyaji,mkombozi wa ulimwengu.


Katika hali ngumu ya mashutumu,mangaiko ya jamii ya Kiyahudi katika kipindi cha Yeremia,Neno la Bwana likaachiliwa katika kinywa cha Yeremia juu ya uzao wa Daudi kwamba atatoka mtawala mwenye “uwezo wa ajabu wa kuponya”.Unabii katika Yeremia 33:6 33;16 unakuja kutimizwa katika Mathayo 1:21


Hivyo, ni sawa na kusema maisha yote ya Kristo Yesu yalitembea katika unabii ikiwa na maana Yesu hakufanya jambo lolote kwa matakwa ya kibinadamu bali lile tu ambalo Baba wa mbinguni ameliachilia kwake ( Yoh.5:19)


Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.

Na Kwa msaada zaidi unipigie simu Kwa+255 683 877 900


What’s app number +255 746 446 446


Na Mch. Gasper Madumla.


UBARIKIWE

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page