top of page

NINAWEZAJE KUTAMBUA NABII WA UONGO? ~ 01.

Updated: Sep 5, 2022


Moja kati ya changamoto kubwa tuliyonayo katika ulimwengu huu ni namna ya kutambua nabii wa uongo na yule wa ukweli kwa maana wanafanana sana kiasi cha kutuchanganya,na ndio maana unaweza ukasema “yule ndiye wa uongo na kumbe ni wa ukweli” na papo hapo ukasema “yule ni wa ukweli na kumbe huyo ndiye wa uongo “. Kwa kweli inachanganya sana,hata inafika wakati hujui ni yupi umwamini na ni yupi usimwamini!!! Miujiza inayofanywa ni mingi na ya ajabu ajabu,na kubwa zaidi ya yote ni kwamba wote wanaweza kutumia jina la Yesu kama mwamvuli wa kujifichia,ili yule wa uongo asije akatambulika.


  • Lakini kwa nini mpaka ifike wakati utamani kuchunguza kazi wazifanyazo? ( kwa maana kama ni nabii wa uongo au wa kweli, watajuwa wao na Mungu wao,mimi wamenihudumia basi yatosha,niende zangu!)


Wengi wana mtazamo huo wa kutotaka kudadisi kazi ya watumishi wa Mungu,. Watu wa namna hii ndio wale wanaofanya chochote wanachoambiwa na mtu anayeitwa mtumishi wa Mungu. Ni hatari hapo! Tumeshuhudia mengi yakifanywa na watumishi halafu wafuasi wakiyatekeleza bila hata kuhoji uhalisia wake,mfano hivi karibuni tumeshuhudia ;


  1. Waamini wakilishwa nyasi kama ishara ya kumpokea Roho matakatifu ( yeyote atakayetapika,basi huyo amekwisha mpokea,na walikuwa wakitapika wengi,kwa sababu ni majani wanayokula)

  2. Waamini wakinywa jick/sabuni ya kusafishia masinki ya chooni,kama ishara ya kusafisha roho za shetani!

  3. Waamini wakilala chini,kisha mtumishi akitembea juu yao,wapokee upako.

  4. Mtumishi akitembea na wanawake,kuwaingizia upako ( akiingiza uume wake,hapo ndipo mwanamke atasheki sheki/vibrate akipokea upako)

  5. Waamini wanao sumbuliwa na pepo wakibeba kichwani mwao mishumaa mikubwa iwakayo moto,ule moto unawaka mpaka unaunguza nywele zao,kama ishara ya kuunguza mapepo kwenye kichwa.

  6. Wadada kumfulia,kudeki,kumpikia baba mtumishi kisha hubakia nyumbani kwa baba mtumishi, kupata upako!

  7. Dah!!!! Zipo nyingi bhana!,n.k


Bibilia inasema tofauti kabisa na mtazamo huo,kwa maana inasema “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.“ 1 Yohana 4:1. Hivyo kuwa na mtazamo wa kuamini kila roho ya mtumishi, na kumwachia Mungu mwenyewe, sio mtazamo wa kibiblia. Bali Neno linakutaka wewe uzichunguze hizo roho,yaani uzitafiti roho za watumishi wanaoitwa ni watumishi wa Mungu kwa matendo/ishara wazifanyazo! Kazi ya kutafiti sio kazi ya Bwana, bali ni kazi yako wewe. Lakini, Je unawezaje kuzichunguza ikiwa huelewi chochote juu mambo hayo? Yaani hata wa kweli humjui utawezaje kumjua wa uongo???? Unanielewa lakini?


  • Ifike wakati, tumwogope Mungu ndugu zangu!


Wapo watumishi wanaoitwa ni watumishi wa Mungu, lakini kwa kweli si watumishihuyo Mungu kabisa! Ingawa hapo mwanzo walikuwa ni watumishi wa Mungu. Watu ambao wanaweza kuigiza mbele ya madhabahu! Utakuta wamekaa kikao kikubwa cha kupanga kuwadanganya/ kuwapotosha watu. Na wakikubaliana wafanye hivi na wafanye vile,wanapokuwa kwenye ibada ili watu waamini,nao wajipate pesa. Utakuta mmoja akijifanya ni mlemavu,halafu wakati wa ibada mtumishi akijifanya anamwombea kisha “msanii”


huyo akinyanyuka na kutembea kama mtu mzima,na watu hapo wakishangilia na kutoa mapesa mengi wakidhani kuwa wanampa Mungu kumbe wanawachangia wasanii walioigiza!!! Ukweli ni kwamba Mungu anaweza kufanya tena zaidi ya hayo,lakini Mungu anautaratibu wake.


Sasa,hivi kweli watu wamefikia kiasi hiki? Cha kulitumia jina la Yesu katika usanii wa namna hiyo? Na hivi kweli hatusomi maandiko kuyapima mambo haya jamani? Tukumbuke kwamba Mungu hadhiakiwi,chochote apandacho mtu,atavuna tu ( Wagalatia 6:7). Wasanii wa namna hiyo,watavuna hukumu ya moto wa milele,lakini na yule anayejua jambo hilo pasipo kulikemea hawezi kubaki salama,na wale wote wanatafuta kudanganywa nao watatumbukia shimoni.


Hujawahi kuona miujiza ya kutengenezwa na watumishi ambao wasanii? Wapo wengine wasiogopa kabisa,waliobobea katika udanganyifu wakicheza kwenye nafasi za manabii au wachungaji,mitume ila hasa kwenye nafasi ya nabii. Hivyo,bila kumwogopa Mungu, wakitumia maandiko hayo hayo,lakini kwenye tafsiri nyingine na wakitumia unabii ambao kweli ukifuatilizia unakuwa hivyo.


Cha ajabu bila hofu,ndipo husema “ mama nimekusikia shida yako,sasa inakubidi utoe sadaka ya ukombozi,lakini hakikisha sadaka yako iwe nono/pesa nzuri…na utakombolewa” maskini ya Mungu, mama huyo hutoka hapo na kwenda kukopa pesa ya ukombozi!!!

Bila kujiuliza uliza wala nini kwa maana tayari amefungwa tena ameambiwa “ukitaka kupona usichunguze chunguze,fanya kila kitu nikuambiacho” Dah!!


Bila kujua ipo sadaka moja tu ya ukombozi, ambayo ilikwisha kutolewa,na hakuna sadaka ya ukombozi nyingine yoyote itakayokuja. Sadaka ya Kristo pale msalabani ndiyo sadaka halisi ya ukombozi, nayo yatosha kabisa. Lakini watu hawajui hilo,maana wasanii hawasemi hiyo kweli!


  • Nifanyeje nipate kuwajua,wanaonidanganya?


Mambo yafuatayo ni siri,yatakayokupa mwanga wa kutambua mbichi na mbivu,uongo na kweli,kutambua yupo ni mganga anayejiita kuwa ni nabii wa uongo na yupi ni nabii/ mtumishi wa kweli….


ITAENDELEA…


Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa

+255 683 877 900

Whatsapp +255 746 446 446


Na Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE.

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page