top of page

NINAWEZAJE KUTAMBUA NABII WA UONGO? ~02

Updated: Sep 2, 2022


01. Utambulisho wao./Kupenda- kujiinua,sifa.


Hili ni jambo la kwanza linaloweza kukupa maarifa ya haraka katika kumtambua nabii wa uongo. Kila nabii wa uongo ana tabia inayofanana na manabii wengine wa uongo. Moja ya tabia ya mtumishi wa uongo ipo kwenye eneo la kujitambulisha/ semi zao. Wengi wa manabii wa uongo wanapenda kujitambulisha sio kutambulishwa, na katika kujitambulisha ndipo hutumia maneno matamu matamu kujisifu.


Maneno kama“ Mimi ni —-,ninaona kila kitu kinachotokea duniani maana mimi ni nabii,….njoo nikuponye wewe mwenye mateso….njoo nikufutie mateso yako….mimi ndio alfa na omega… Usicheze na moto huu,sina haja ya kukuombea kwa jina la Yesu, jina langu tu ni dawa…” N.K ukichunguza maneno hayo, utajua mtumishi huyo si wa kweli kwa maana yeyote anayeweza kufanya maombi nje ya Jina kuu la Yesu, anapata wapi nguvu kama sio kwa shetani? Lakini;


Kumbuka; kujitambulisha sio kubaya,wala sio dhambi,kwa maana kila mmoja hujitambulisha pale anapoulizwa au anapopata nafasi ya kujieleza. Ubaya ni kile kinachomtoka mtu,hata kuacha maswali mioyoni mwa watu,“ Je sifa hizi zote ni za kweli? Je sifa hizi zote ni za mtu au Mungu? “ . Kwa mujibu wa biblia “Bwana ndiye aliye mkuu,Na mwenye kusifiwa sana.” Zab.48:1. Sasa,swali la kujiuliza kwa nini mpenda sifa kuitwa ni nabii wa uongo? Mbona ni hali ya kawaida kabisa!!!


  1. Mtumishi yeyote anayependa sifa,ni lazima awe mwongo kwa sehemu kubwa.


Ikiwa mtumishi wa Mungu akafikia wakati wa kujiweka kwenye nafasi ya Mungu kwa namna yoyote ile hasa katika maneno ya kinywa chake,ujue mara nyingi atakuwa akisema uongo hali akijua kwamba anasema uongo. Lengo kuu linakuwa yeye aonekane yupo juu kuliko anavyoonekana. Fikiria asemapo “njoo nikuponye,…mimi ni nabii wa Bwana hapana chezea kwanza siumwi,sifi leo wala kesho,….


nilikuwa nazungumza na Mungu jana,leo kaniambia….”

Katika maneno hayo tu ambayo tumeyasikia yakitamkwa na watumishi wa namna hiyo mara nyingi,ambayo kwa kweli hakuna ukweli ndani yake. Kwa maana Mungu ndiye aponyaye bali anaweza kumtumia tu kama chombo,lakini yule aponyaye ni Mungu,ni Yesu. Tena hivi ni kweli unaweza kuishi hapa duniani bila kuumwa hata mafua? Tena hivi ni kweli utaishi milele? U Mungu?….Unaona hapo!!! Maneno hayo machache yanamtambulisha nabii huyo ni nabii wa namna gani!!!


Siku moja nilikuwa kwenye Bajaj,ndani ya ile Bajaj radio ilikuwa imefunguliwa na mtumishi mmoja alikuwa kwenye kipindi, na ilikuwa kipindi cha kupokea simu kwa wagonjwa ( maana alikwisha fundisha inavyoonekana,tulikutia kipindi mwisho mwisho) mama mmoja akapiga simu,ajaanza kujieleza chochote juu ya shida yake,basi mtumishi aliyekuwepo radioni akamwambia “mama umelogwa na jirani yako,….”


yule mama akawa anashangaa kwa maana inaonekana kana kwamba ni kweli hivi,lakini hajaanza kusema gafla mtumishi hapo hapo akamtafutia ufumbuzi“…mama…nina maji ya upako ninayo kwa bei poa,….” sasa hapo meona namna mambo yalivyokuwa!!!

Lakini pia katika eneo la “ utambulisho” si lazima mtumishi awe na mambo hayo yote,lakini mtumishi yeyote akiwa nje ya Yesu,huyo ni wa uongo moja kwa moja. Biblia inasemaje? “ Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.” Kutoka7:11-12


Andiko hili linatupa picha za watu wa aina mbili waliofanya miujiza. Mmoja ni mtu upande wa Mungu na mwingine ni wa upande wa shetani( mchawi). Lakini cha ajabu wote wawili wamefanya ishara,yaani Musa alifanya kwa msaada wa Mungu aliyemtuma na wachawi nao walifanya kwa msaada wa nguvu za giza. Miujiza yao inafanana – fanana,( lakini kamwe muujiza wa Mungu utabaki kuwa ni muujiza wa pekee)

Andiko hilo linatufundisha mambo mawili ya msingi;


  1. Wachawi nao wanaweza kufanya ishara.

  2. Ishara ya Bwana ni kuu kuliko ya mchawi ndio maana nyoka za wachawi zilimezwa


Hivyo,kwa neno hilo,watumishi wa farao waliofanya ishara walikuwa ni “wachawi“. Ni rahisi kutambua kwamba ishara zao ilikuwa imetokana na nguvu za giza,kwa maana wao wenyewe ni wachawi. Hata leo,wapo watu ambao si wa Kristo nao wanafanya ishara na miujiza kwa kutumia vitabu vyao na mambo mengine. Watu wa namna hiyo wote ni manabii wa uongo/ wadanganyifu/watumishi wa shetani.


Katika hili,wala huitaji kufunga na kuomba ili uone kwamba wanatumia nguvu za Mungu au za giza? Kwani hujawahi kusikia kwenye matangazo watu wanaojitambulisha moja kwa moja kuwa hutumia majini kuponya magonjwa!! Sasa watu kama hawa unahitaji kufunuliwa ili uwatambue? Hivyo yeyote aliye nje ya Kristo, muujiza wake si wa kweli….


ITAENDELEA…


Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900


Whatsapp .+255 746 446 446


Na Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE.

Komentarze


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page