top of page

UTIMILIFU WA NABII – 1.

“ Utimilifu wa unabii uliotolewa na uliotimizwa katika Kristo (Nabii 10 katika agano la kale) ”

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

“Majani yakauka, ua lanyauka;Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.“ Isaya 40:8

Neno la Mungu ni lazima litimie,na kamwe haliwezi kupita bure ( soma pia Isaya 55:10). Hii ni wazi kabisa kwamba katika kila neno lililonenwa na nabii kumhusu Masihi,hakika utimilifu ni lazima. Ujio wa masihi haukuwa gafla bali ni mpango kamili wa Mungu. Mungu aliufunua mpango huu kwa manabii wake,kila nabii alimwelezea masihi na ujio wake. Kuanzia kuzaliwa kwake hadi kufa na kufufuka kwake kulitabiliwa mapema . Hata mahali gani Masihi wa Bwana atatokea,nako kulikwishatabiliwa hii yote ni kuonesha tu kuwa ujio wa masihi Kristo Yesu,ulikuwa ni mpango wa Mungu kuokoa watu wake. Machache ninayokuandikia kati ya mengi niliyonayo,ni kukuonesha nabii chache zilizotolewa kuhusu masihi.

Nini ujumbe mkuu wa Biblia?

“wokovu” ndio ujumbe mkuu wa Biblia kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo wa Yohana. Habari ni moja tu,“ wokovu ulioletwa na Kristo ” ndio kiini haswa cha Biblia. Ni mapenzi ya Mungu kuokoa watu wake,Yeye hupenda kila mtu aokoke ( 2 Petro 3:9,1 Timotheo 2:3-4). Simulizi zote zinamlenga Kristo kama masihi wa Bwana. Moja ya kitu kikubwa cha kujifunza kwenye huduma/utumishi au maish yako ni “ Neno la Mungu lolote linalohubiriwa ni lazima limlenge Kristo / Christ should be the center” ( kama injili inayohubiriwa hayupo Kristo, basi ujue si injili hiyo,kwa maana Kristo ndiye injili yenyewe)

Unabii na utimilifu wake,kwa ufupi.

  1. Uzao wa mwanamke – Mwanzo 3:15 ( Utimilifu : Wagalatia 4:4,Ufunuo 12:5)

  2. Mahali atakapozaliwa,Bethlehemu – Mika 5:2 ( Utimilifu: Mathayo 2:1,Luka 2:4-7)

  3. Atazaliwa na bikira – Isaya 7:4 ( Utimilifu ; Mathayo 1:18)

  4. Katika kuzaliwa kwake,watato wachanga watauwawa – Yeremia 3:15 ( Utimilifu; Mathayo 2:16)

  5. Mwana wa Mungu atakimbilia Misri – Hosea 11:1 ( Utimilifu; Math.2:14)

  6. Atasalitiwa na mtu wa karibu /rafiki – Zab.14:9 ( Utimilifu; Math.26:14-16)

  7. Atanyamaza wakati wa kuhukumiwa/ hatapambana kwa kinywa – Isaya 53:7 ( Utimilifu; Math.26:62-63)

  8. Alibeba dhambi za wakosaji- Isaya 53:12 ( Utimilifu; Math.26:28,Yoh.1:29)

  9. Hataonja uharibifu / atafufuka – Isaya 16:10 ( Utimilifu; Math.28:9)

  10. Atapaa juu,atanyakuliwa – Zab.68:18 ( Utimilifu; Luka 24:50-51)

Hata hivyo,ni nabii nyingi zilizonenwa kwa habari ya masihi nazo zimetimia. Nabii nyingine zilieleza hata namna huduma yake itakavyokuwa,namna atakavyolichunga kundi lake n.k,na hakika ndivyo ilivyokuwa.

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI, piga kwa +255 683 877 900

Whatsapp namba +255 746 446 446

Mch.G.Madumla

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page