top of page

UTAONA,LAKINI HUTAKULA!!!

Updated: Aug 30, 2022

  1. Utaona kwa macho yako lakini hutakula / “You will see it with your own eyes,” answered Elisha, “but you will not eat any of it!”


Katika kipindi cha mtu wa Mungu Elisha,kulikuwa na njaa huko Samaria kiasi cha kuuza kichwa cha punda kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha. Katika kipindi kigumu kama hiki,mtu wa Mungu Elisha anasimama na kuutangazia uma habari njema asemayo Bwana akisema


“…Lisikieni neno la BWANA; BWANA asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.“ 2 Wafalme 7:1


Elisha mjumbe wa Mungu anasema kile alichoambiwa kusema kwa watu wote. Ili kuonesha kwamba yale ayasemayo si yake bali ni ya Bwana,Elisha anabainisha wazi kwamba ni ni neno la Bwana hilo. Watu wanaambiwa “ walisikie Neno la Bwana ” kwamba wasije kupuuzia,tena waliamini Neno la Bwana.


Kumbuka hapo;Neno la Bwana limekuja kwenye kipindi kigumu cha njaa,kutengua njaa hiyo,lakini ni lazima kwanza kulisikia ( yaani kulipokea katika imani yote). Kumbe hata kipindi kigumu cha siku za leo,bado Mungu analo neno kwa ajili ya watu wake,“kutengua ugumu”Kwa maana Bwana anajua watu wake,naye anajua kwamba hatuwezi kujinasua wenyewe!


Lakini hata hivyo,akida mmoja anayeaminika na mfalme,anasimama na kupingana na Neno la Mungu, akida huyu anaonesha kuwa ni mtu asiyeliamini Neno la Bwana wala kuwaamini watumishi wake,kwa maana akida anasema“ …Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? …” 2 Wafalme 7:2 akida hakubaliani na Neno la Bwana, kwa maana macho yake yamekamatwa na mazingira yaliyopo.


Hata leo kuna watu wengi wanaofanana na akida huyu,watu ambao hawaamini na kupingana na Neno la Bwana kwa kuyaona mazingira waliyokuwa nayo ( kwa maana mazingira aliyokuwa nayo akida ni mazingira ya njaa,magumu,ukame lakini papo hapo lipo Neno la Bwana lisemalo kinyume na mazingira hayo ).


Lakini cheki kile akida asemacho kwa Elisha mtu wa Mungu,akida anapingana na Neno kwamba jambo hilo haliwezekani hata kama Mungu akifungua madirisha ya mbinguni,haliwezekani. Hapo ndipo Elisha alipomwambia “…Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.”. Kuna watu walikula lakini si akida,yeye aliishia kuona tu,hakula kwa kutokuamini kwake na kupingana na Neno la Bwana. Ni rahisi kuwa na tabia kama ya huyu akida,lakini ujue kwamba matokeo yake “ hutakula


Jaribu kufikiria kwamba ni hasara kubwa kiasi gani aliyoipata akida! Na na hasara kubwa kiasi gani kwa mtu anayefanana na akida,yule anayebeza,kukataa,na kutomwamini mtumishi wa Mungu pamoja na kulikataa Neno la Bwana kwenye kizazi hiki. Ni vyema ukajifunza kupitia akida huyo ambaye kuburi chake kilimponza.


Kwako wewe uone,na kula ule.

Wazo mama la ujumbe huu,ni kueleza jinsi ambavyo kutokuamini kunavyoweza kuathili baraka zako. Kwa maana kwa mfano huo wa akida,tunaona kwamba Bwana alikwisha achilia neema ya chakula palipo na ukame,lakini mmoja ( akida) hakuweza kupokea neema hiyo kwa sababu ya kukinganzana na Neno la Bwana Mungu.


Kushindwa kulipokea Neno la nabii ni kushindwa kupokea neno la Bwana kama ikiwa nabii huyo ni nabii wa kweli.


Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900.


Na.Mch. G.Madumla


Whatsapp namba +255 746 446 446


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page