top of page

UTAKUWA MBALI NA KUONEWA

Updated: Aug 30, 2022



  • Utakuwa mbali na kuonewa / You will be far from oppression


Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia. ” Isaya 54:14 .


Ni neno la faraja na matumaini  juu ya mtu aliyekuwa akiteswa,na kuonewa. Neno “kuthibitika” lina maana ya “ kuwa imara”,hivyo ukitafakari Neno hilo utagundua kwamba,Bwana ndiye mwenye kumthibitisha/kumfanya mtu awe imara katika haki. Lakini ahadi ya Bwana juu ya anaonewa ni kumpa uhuru /awe mbali na kuonewa. Uonevu huu unozungumziwa katika Isaya 54,ni ile hali ya kugandamizwa katika haki za msingi anazostahili mtu kupata.


Watu wa Mungu walikuwa katika uvuli wa mauti huko Sayuni,wamekosa msaada wa kibinadamu, Hata hivyo jischo la Bwana lilikuwa pamoja nao,hii ina maana Bwana alikuwa hajawaacha wala kuwapungukia. Hali yao ya kimaisha Bwana alikuwa akiijua vizuri,na kwa huruma zake,anaamua kuwainua kutoka katika hali mbaya ya kuonewa. Kumbuka,Bwana ni mwenye huruma juu ya watu wake.


Hata sasa,Bwana anashughulika sana na haki yako. Ni vyema kufahamu kwamba,Bwana anajua uonevu unaopitia na anajua kwamba pasipo Yeye,wewe huwezi kabisa kujiondoa mwenyewe katika mazingira hayo ya kuonewa. Kuna hali ya kugandamizwa / to be oppressed,ambayo haitokani na Bwana Mungu bali inatokana na adui/ibilisi. Ni vyema kufahamu kwamba “hupaswi kuonewa / kugandamizwa ” kwa namna yoyote ile.,ukifahamu ili basi utakuwa na nafasi ya kudai haki /ahadi hii katika maisha yako. Uonevu si fungu lako!!!


  • Uonevu katika ndoa


Watu wengi leo wamejikuta wakilia sana badala ya kufurahi katika ndoa zao. Wengi wanaonewa,wanagandamizwa kiasi kwamba hawajui la kufanya na wanaishia katika kulia tu. Lakini fahamu ya kwamba “kulia” sio solution / ufumbuzi/utatuzi wa hali ya uonevu. Lazima uchukue hatua ili utoke katika kilio hicho cha muda sasa. Ukweli ni kwamba huwezi ukatoka katika kugandamizwa / kulia kwa kupambana kimwili,kwa maana utapigwa tu!!!


Ebu angalia watu waliokuwa wakilia kila siku kwa sababu ya uonevu waliokuwa wakiupata,kisha angalia ni kwa namna gani baadhiyao walifanikiwa kuwa mbali na uonevu huo kupitia njia gani. Moja ya mfano mzuri,ni Taifa la Israeli (Isaya 54 hiyo hiyo),walikuwa na mateso,lakini waligundua kwamba wanamwitaji Bwana awatoe katika mazingira magumu ya uonevu.


Bwana alituma neno kwanza kwa kinywa cha nabii Isaya kuwaambia yatosha sasa,akawaambia “utakuwa mbali na kuonewa” . Hata leo,lipo neno la Bwana linalozungumza nawe katika uonevu unaopitia – Isaya 54:14. Kamata Neno hili,kisha liimbilizie/omba ukisimamia neno hili/mkumbushe Bwana ya kwamba “wewe si wakuonewa” kwa maana Bwana amezungumza na maisha yako. Ukiamini hili nilisemalo kisha ukachukua hatua ya kurejea kwa Bwana kimaombi,kuna kitu kitabadilika katika hali yako.


Hata hivyo wengi wanapitia katika uonevu mbali mbali,lakini majibu yake ni moja tu,kwamba ni Bwana ndiye atakaye kukuthibitisha katika haki. Hivyo kwa yeyote anahisi kwamba anaonewa kwa namna yoyote,anatakiwa kwanza asimame katika haki ili Bwana sasa ampiganiye na uonevu huo.


Inawezekana kabisa kuwa mbali na kuonewa,kwa maana Bwana ajua yote unayopitia,kwa maana Yeye hujua yote – Zab.139:3-4


Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,basi nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja. Lakini inawezekana labda unahitaji MAOMBI kwa maana nawe unapitia changamoto hii,


Basi kwa yote nipigie sasa kwa + 255 683 877 900


What’s app namba ni +255 746 446 446 


Na Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE.

コメント


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page