USINIPUNGUZIE MWENDO,NISIPOKUAMBIA.
- Mch. Gasper Madumla
- Jun 11, 2018
- 3 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
” Usinipunguzie mwendo,nisipokuambia” ni maneno ya mama mwenye haraka kumuendea mtumishi wa Mungu kwa sababu amefikwa na msiba wa mwanae. Ni Mwanamke Mshunami aliyechua hatua ya imani ya kumkimbilia Elisha mtumishi wa Mungu akitazamia kuona uzima wa mwanae. Mzigo aliokuwa nao mwanamke huyu Mshunami ulikuwa ni wa kipekee kwa maana hata mumewe hakuwa na mzigo huu,na kwa sababu hiyo hakuwa tayari kumsikia mtu mwingine isipokuwa Elisha mtumishi wa Bwana ambaye kwa yeye alipata muujiza wa mtoto. Vile alivyokuwa akimkimbilia Elisha haikuwa mwendo wa kawaida,maana hakutaka kumbunguziwa mwendo! Mwanamke Mshunami ananifundisha mambo mengi ninapomuangalia.
ebu angalia; mtoto wake alipokuwa akiumwa kichwa kwa maumivu makali sana,huku akiwa na babae. Baba hakuwa na majibu ya uponyaji wa mwanae na akamwitaji mkewe ndiye aweze kushughulikia ugonjwa huo ( 2 Wafalme 4:18-20). Kumbe wanawake ndio hasa wajuao kuwatibu watoto kuliko hata wanaume. Angalia hata kwenye familia tu,unapoona mtoto akiumwa basi ni mama ndie atakayemuangaikia kwa kweli. baba huwa wanasema ”mpelekeni mtoto kwa mama yake” ; wamama ndio madaktari wazuri wa watoto,na huu ndio ukweli. Lakini tunjifunza nini kwa mwanamke mshunami katika semi hii ”Usinipunguzie mwendo,nisipokuambia” ?
Unapochukua hatua ya imani juu ya jambo lolote usikubali mtu / watu kukupunguzia mwendo wako. Kwa namna yoyote usikubali kupunguziwa kasi yako ya imani kwa sababu hawajui ni mzigo kiasi gani uliopo ndani yako. Unajua yule mwendesha punda,hakuwa na mzigo wowote bali kazi yake ni kuendesha tu,lakini mwanamke Mshunami ndie alikuwa mwenye mzigo na ndie alikuwa akijua thamani ya kumwendea mtumishi wa Mungu. Laiti mwanamke Mshunami angelikubali kupunguziwa mwendo,asingelifaulu mpango wake. Unapoiendea hatma yako hakikisha pasiwepo na mtu awaye yote atakayekupunguzia mwendo wako,ni muhimu sana hili. Mara nyingi ukiruhusu mwendo kupunguzwa basi ujue utafeli yale unayoyaendea !
Inawezekana kipunguza mwendo ni mwenzi wako wa ndoa,lakini ni vyema kumwambia asikupunguzie mwendo wa hatua yako ya imani ulikwisha ichukua. Mfano; mtoto kweli anaumwa na hali yake si nzuri na wewe unataka umpeleke kwenye maombi akaombewe kama hatua yako ya imani. Kisha ni kama vile unapanga kwamba pakipambazuka tu,basi utampeleka kwa mchungaji aombewe,lakini mwezako anakuambia ”haina haja,utampeleka Jumapili wiki ijayo” Sasa huku ndiko ”kupunguziwa mwendo kwenyewe” kwa maana wewe una kasi ya kumwahi mtumishi akaombewe lakini mwenzako haoni umuhimu wowote,na cha ajabu anakuambia umpeleke wiki ijayo! Jiulize akizidiwa je? Au chukulia biashara yako ipo katika hali mbaya ya kufa au kuanguka kabisa,nawe ndani yako kumekuwa na mzigo wa kufunga na kuomba kwa ajili ya biashara yako,lakini mwenzako anakwambia ” usihofu,itakaa sawa yenyewe,ipe muda”
Mshunami alitambua kwamba uzima upo kwa Bwana maana ni Bwana ndiye aliyempatia muujiza basi ni Yeye ndiye atakayeweza kuleta uponyaji katika huo muujiza. Alipoazimu kuendea uzima katika muujiza wake,hakutaka mtu aweye yoyote amsimamishe maana alitaka kujua Bwana atafanya nini kwanza. Jifunze katika hili,pale unapokimbilia kwa Mungu,hakikisha pasiwepo yeyote wa kukurudisha nyuma tena maanisha ili kama yupo wa kukurudisha nyuma basi aone kwamba umemaanisha hutaki kurudishwa nyuma!. Shida ni kwamba wengine hawawezi kuelewa ni mzigo wa kiasi gani ulionao,ni namna gani unataka Bwana akujibu,ni namna gani unataka ukutane na Mungu,Hawaelewi hilo!!! Sasa wewe mwenye kuelewa hilo,waambie wasikupunguzie mwendo usipowaambia!
mtu mmoja anaona akiponywa na Bwana hata kuchukua hatua ya kimaombi zaidi,lakini mwenzake anamwambia ”haina haja,acha tu” Lakini mtu huyo anafikiri kama atakubali kurudi nyuma kwa kasi aliyokuaameianza,Je atafainikiwa lengo lake? Ni kweli kuna gharama lakini mtu huyo amekubali kulipa gharama zote ila asipunguziwe mwendo. Na hatimaye mwishoe anafanikiwa lengo lake ; Mimi sijui hata kama unanielewa hapa,maana hata wewe ukikubali kwa namna yoyote kurudi nyuma katika hatua ya kasi uliyoanza nayo basi ujue hutafikia hilo lengo. Ni afadhali ufike ukiwa umechoka kuliko kutofika kwa kupunguziwa mwendo.
Mwanamke Mshunami hakumwendea Elisha kwenye mwandamo wa mwezi wala haikuwa sabato kama ilivyokuwa kawaida. Hakuona shida kwa sababu jambo lililokuwa moyoni mwake halikuhitaji protoko za kawaida. Agenda yake ilikuwa ni moja tu,ilikuwa ni kuapata uzima wa mwanaye basi!. Kumbe,ukifuata mambo ya protoko / hitifaki katika mambo ya kiungu utafeli! bali katika mambo ya kiungu itifaki ni kwa Roho mtakatifu tu,na kisha kuziba masikio,usisikie ya watu wengine ambao kwa kweli lengo lao ni kukupunguzia mwendo. Wale wote waliokubali kutembea kwenye kasi yao pamoja na Roho mtakatifu walifanikiwa sana. Jiulize wewe sasa,ni nini kinachokupunguzia mwendo usipokiambia? Je ni mume ? je ni mke? Je ni boss wako? Je ni baba au mama yako? Je ni mchumba wako? Usikubali mtu akupunguzie mwendo wa hatua yako ya imani.
Ikiwa kuna kipunguza mwendo wako kilichongangania kiasi kwamba umejaribu kukipinga lakini unaona hujafanikiwa vizuri,ebu nishirikishe kwa kunipigia simu ili tuombe pamoja. Ikiwa pia kama umebarikiwa na ujumbe huu kwenye kazi,biashara,maisha yako,au imani yako kwamba umejifunza kitu basi naomba unitumie ujumbe nijue. Sasa piga simu na kwa maombezi pia,kwa
+255 683 877 900
Namba ya What’sapp ni .+255 746 446 446
Mch. Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
コメント