top of page

USILIPE KISASI,KISASI NI KAZI YA BWANA.

Shalom…

Kwa ufupi.

Ilikuwa ni miaka ya vita na mapambano dhidi ya adui wa Daudi na watu wake. Daudi alifanikiwa kulinda mali yote ya mtu mmoja ambaye alikuwa mkuu kwa sababu ya utajiri aliokuwa nao,mtu huyo tajiri alikuwa akiitwa Nabali. Ukweli ni kwamba Nabali alikuwa mwenye mali nyingi kwa maana alikuwa na kondoo elfu tatu na mbuzi elfu zake,lakini bahati mbaya alikuwa ni mtu aliyekosa adabu,mkorofi,mwovu katika matendo yake yote.

Mke wake Nabali alikuwa mzuri,na mwenye akili na jina lake aliitwa Abigaili. Baada ya miaka ile ya shida aliyotumia Daudi huko nyikani akilinda mali ya Nabali pamoja na wachungaji wake huku akitafutwa na hasimu wake mkubwa Sauli,mtu mwenye wivu na mbaya,ilifika wakati ambapo hari ikawa shwari kidogo.

Siku moja ambayo Nabali na watu wake wakawa wakiwakata kondoo manyoya,bila shaka ilikuwa ni maandalizi ya shughuli ya kula na kunywa. Siku hiyo hiyo,Daudi akatuma vijana wake kumi waende kwa Nabali ili wamsalimie. Sasa wewe unajua kabisa,kama ikiwa ndio kuna sherehe nyumbani kwako,alafu ndugu yako au rafiki yako anakuja siku hiyo hiyo,kuja kukusalimia,hapo utajua tu “kwamba jamaa kaja kula” kwa sababu kwa nini asije siku nyingine aje leo kwenye sherehe.

Katika hili,Daudi aliweka wazi akituma vijana,na kuwaambia wamsalimie Nabali lakini “ Nabali awafikirie chochote atakakachokuwa nacho awape ” kwa kuwa Nabali alikuwa mtu mbaya asiyekumbuka fadhila za Daudi kumlindia mali yake,badi Nabali akawatukana wale vijana na akawanyima ( yaani kawatoa mikono mitupu,hali yeye yuko na utajiri mwingi). Sasa,hapo ndipo Daudi akaona huu ni ujinga,akachukua upanga wake,pamoja na vijana mia nne wengi wenye panga,na kuelekea kwa Nabali kwenda kuangamiza.

Kitu gani Daudi anafanya?

Daudi alipopokea taarifa mbaya kutoka kwa Nabali kwamba Nabali kawatukana vijana wake,Yeye akaamua kwenda kurudisha mashambulizi“ yaani kulipa kisasi“. Ilikuwa hakuna haja ya kulipa kisasi kwa Nabali, lakini Daudi akaenda. Ashukuriwe Mungu,Abigaili akasawazisha mabaya haya. (Soma habari kamili 1 Samweli 25:1-44)

Lakini hata hivyo,Mungu alimzuia Daudi katika ubaya wake alioupanga. Mungu alimtumia Abigaili mke wa Nabali kusimama katikati ya kusudi baya,ili Mungu aonekane yeye mwenye kulipa kisasi. Wakati mwingi Mungu anawatumia watu wazuie kile kibaya ulichopanga juu wengine. Ebu tazama jinsi alivyomtumia Abigaili kumnyamazisha Daudi. Laiti kama Daudi asingelikubali shauli la Abigaili, basi Daudi angeliangamia kwa kisasi alichopanga. Ebu jiulize;

Ni mara ngapi Mungu amekuinulia mtu ili akutulize na hayo mabaya uliyoyapanga lakini,wewe umempuuzia kisha ukafanya mabaya? Je kwa nini humsikilizi huyo mtu anayekujia na kukushauli tofauti na mtazamo wako mbaya. Labda anaweza akawa ni mke au mume wako,kwamba nakushauri ugeuke katika kisasi ulichopanga lakini hutaki kumsikiliza. Shauri yako,utapigwa na Mungu ikiwa kama hutaweza kumsikiliza.Tunaona baadaye Mungu mwenyewe alimpiga Nabali. Na hapo ndipo Daudi akasema :

“ …,Na ahimidiwe BWANA ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumwa wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali BWANA amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe….” 1 Samweli 25:39

Daudi hakuyajua haya yote kwamba, alitakiwa amwachie BWANA alipaye kisasi tena bila upendeleo wowote. Ebu fikiri kama Daudi akelipa kisasi,angelikuwaje mbele za Bwana? Jambo hilo hilo,fikiria kwako pia kwamba, kama utalipa kisasi leo kwa aliyekukosea,hivi utakuwaje mbele za Bwana. Je hautakuwa na hatia mbele za Mungu. Bila shaka utakuwa na hatia kwa sababu hukutakiwa kumrudishia yule aliyekukosa. Biblia inazidi kusema kwamba “ Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.” Warumi 12:19

Ujue jambo hili; ikiwa utalipa kisasi katika kosa au jambo lolote lile,basi utakuwa umefanya dhambi. Kwa maana unaingilia kazi ya Mungu. Lakini fikiria kwamba,kama na wewe ungelipiwa kisasi ungelikuwa wapi? Je wewe hukutenda makosa namna hiyo,? Tena hukutena makosa zaidi ya hilo? Je mbona uliachwa salama! Iweje leo unataka ulipe??? Ukumbuke chochote utakachopanda utavuna. !! Maana kama leo unapanda kulipa kisasi kwa mtu huyo,ujue nawe utapigwa siku moja hata kama sio wewe labda mpenzi wako,au mtoto wako atalipwa baya litakalokufanya ulie huku ukiwa unakumbuka ya kwamba na wewe ulimfanyia mtu fulani.

Kwani hujawahi kuona,mtu/ mwanaume aliyekuwa akiwaharibu wanafunzi kwa kuwachezea chezea hata kuwakosesha masomo. Alafu baadae angalia kinachotokea. Watoto wake wakuzaa kabisa, na wenyewe wanakuwa hawatulii,wakichezewa na mtu mwingine kipindi hicho yeye kashaacha. Sasa weee!! Si kulia huko!!!! Usilipe kisasi,kisasi ni kazi ya Bwana.

Ikiwa umebarikiwa na fundisho hili nifahamishe pia. Kwa maombezipia nipigie kwa namba hizi hizi + 255 683 877 900 

WhatsApp ni +255 746 446 446

Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page