top of page

USIKATE TAMAA/USIVUNJIKE MOYO -YOUR RAINY SEASON IS COMING!

Updated: Sep 5, 2022



Na Samuel Nathanael Sasali.


Bwana Yesu asifiwe… 


Nilipokuwa mdogo nilikuwa namuona MAMA akichambua maharage, alikuwa anaweka *maharage mazima* kwenye sufuria ya kupikia, na *maharage mabovu* alikuwa anayatoa kisha anayatupa mbali jalalani.!

Chakushangaza.. mvua ikinyesha maharage yale yale mabovu ndio yanakuwa ya kwanza kuota na kuchipua..

Yalitupwa yakiwa mabovu yasiyofaa.. lakini yanaota.. kisha yanatoa maharage mengine mazima na bora zaidi kuliko yalivyotupwa mwanzo yakiwa mabovu! “

Hii imenifanya nijifunze kuwa ni muda/wakati tu utakao amua hatma yako.. Pia jinsi Mungu anavyokuona ni tofauti kabisa na watu wanavyokuona.. Inawezekana ukaonwa/ukajiona kama maharage mabovu leo.. lakini hakika *mvua ya Mungu* ikikunyeshea UTAOTA na kuwa wa thamani na KUZAA/KUTENGENEZA WATU WENGINE BORA ZAIDI YA WEWE..


Inahitaji wakati tuu Uvumilivu.. Na kujua kusudi la Mungu na mawazo ya Mungu ni tofauti na ya binadamu….

USIKATE TAMAA WALA USIVUNJIKE MOYO YOUR RAINY SEASON IS COMING

Wewe ni bora na unafaa sana.! Kila jambo chini ya jua lina wakati wake haijalishi jinsi ulivyo leo.


Wasiliana nami Kwa +255 683 877 900

What’s app ni +255 746 446 446


Mungu awabariki na nawatakia siku njema

BARIKIWA.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page