USHINDI KABLA YA MWAKA MPYA.
- Mch. Gasper Madumla
- Dec 31, 2019
- 2 min read
Updated: Aug 30, 2022

Kwa ufupi,
Katika mbio za riadha za mita ndefu,wakimbiaji huanza kukimbia taratibu kwa staili ya “kuvuta pumzi ” huku kila mmoja akitaraji kushida taji,lakini hata hivyo si wote washindao ingawa wote wamejitia machezoni.Lakini gafla mwendo wao hubadilika na kuongezeka zaidi pale wanapobakiza umbali mdogo wa kumaliza.
Mkimbiaji huangalia sana anamalizaje na si anaanzaje,na ndio maana katika kuanza yupo tayari wengine wamtangulie lakini si kwenye kumalizia. Hivyo,ipo maana kubwa ya kuwa na kasi zaidi kwenye kumaliza jambo lolote kuliko kuanza,hata kipindi hiki cha kumaliza mwaka kasi zaidi inahitajika na wale wenye kujua mbinu za wanariadha utawakuta sasa wakikaza zaidi kwenye kumaliza. Kwa muda mfupi uliobaki,Bwana aweza kukushangaza,na hatimaye ukauona ushindi wako. Lakini ongeza spidi!
Usiku wa kutoka Israeli utumwani.
Ebu cheki taifa la Israeli lililokuwa utumwani Misri kwa miaka mingi 430 hivi. Na hatimaye muda ulipowadia wa kutoka utumwani,kwa usiku mmoja tu,kila kitu kilibadilika. Hata tarehe zilibadilika,kwa maana walianza mwaka mpya ( Kutoka 13:1). Safari zao zikabadilika,walikuwa mahali pamoja sasa wanatakiwa watembee mbele.“ Kwa usiku mmoja tu“,mambo yote yalibadilika,hata historia nzima ya maisha yao ilibadirika! .
Miaka mingi ya kuteseka,lakini kwa usiku mmoja tu Ukombozi ulifanyika. Kumbe, hata muda wa usiku mmoja tu,mambo yako yaweza kubadilika,ukawa wa tofauti na ushindi ukawa ni sehemu yako. Kwa Mungu dakika moja tu yatosha kubadili mambo yote,kwa maana hakuna lisilowezekana kwake!
Fanya kiume,fanya haraka ni muda wa kutoka.
Katika usiku mmoja Mungu akawahimiza Israeli wafanye kiume / wakaze,tena wafanye mambo yao kwa haraka. Hii ni sawa na Mungu anajaribu kuwaambia sasa mnakaribia kumaliza mbio huku Misri sasa,ongeza kasi usiku huu. Kasi ilihitajika kwa maana ni muda wa kutoka. Ikiwa imebaki muda mfupi kumaliza mwaka,“kasi ya maombi”,inahitajika mno kwa maana ni wakati wa kutoka kwako. Ikiwa utapunguza mwendo,ujue hutaweza kwenda na mwendo autakao Mungu mwaka ujao. Kuna mambo lazima uyasukume kiume/ kinguvu ili uingie mwaka kwa nguvu zote. Mfano,mwaka mpya lazima ukabidhiwe kwa Mungu kikamilifu,hii ni kupiga kasi zaidi!
Una malengo gani mwaka mpya / Umeupa neno gani mwaka mpya?
Kuna umuhimu mkubwa wa kuubatiza mwaka mpya,kwa kile unachokitazamia wewe. Jiulize maswali haya; Je mwaka mpya ni mwaka wa nini kwako? Je Bwana anataka ufanye nini mwakani? Una malengo gani? Kuna nguvu ya majina,unapouita mwaka mpya kwa jina zuri,ndivyo itakavyokuwa. Wengine wanaelewa ni nini ninazungumza hapa. Mfano wengine wanaweza kuuita ni mwaka wa ushindi,mwaka wa kuinuliwa,kupenya,mwaka wa neema,mwaka wa kihuduma n.k!
Wewe je unauhitaje mwaka mpya,fikiria sasa,na umwombe Mungu akuoneshe ni mwaka wa namna gani kwako. Usiwe kama yule bwana mjinga fulani aliyeuita mwaka fulani,kuwa ni mwaka wa shida! Unaambiwa huyo jamaa aliambatana na shida kipindi chote cha mwaka huo kwa maana majina yana mata sana.
Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.
Kwa msaada zaidi na MAOMBI piga +255 683 877 900
What’s namba + 255 746 446 446
Na Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
コメント