USHAURI WA MEMUKANI ~ 01.
- Mch. Gasper Madumla
- Nov 18, 2019
- 3 min read
“Ushauri” ni maoni au mapendekezo ya nini kifanyike katika njia nzuri. Ushauri usimama kama dira katika maisha ya kawaida ya mwanadamu. Hii ni sawa na kusema mwanadamu anahitaji ushauri juu ya nini afanye au asifanye.
“Ushauri ni zao la ufunuo ” hii ina maana, mtu upata kwanza ufunuo juu ya kitu au jambo fulani kisha maarifa ya nini kifanyike huja,na hapo ndipo mtu utoa “ ushauri ” ( au neno la maarifa). Ukichunguza maisha ya kila siku ya watu,utagundua kila siku watu wanahitaji “ kutoa au kupokea ushauri” na ndio maana ushauri ni moja ya kipawa. Ebu tazama,ukiwa mfanya biashara utahitaji ushauri wa namna ya kuendesha biashara yako,kwamba nini usifanye na nini ufanye.
Au ukiwa ni mtumishi wa Mungu, bado utahitaji ushauri nini ufanye na kitu gani usifanye. Kwa hiyo “ ushauri” ni mapendekezo au maelekezo yatolewayo na mtu. Nataka uuone ushauri kama “maelekezo” ya nini ufanye,ili twende pamoja.
Kwa ufupi,
Ushauri ni kama taa za barabarani.
Nilikuwa najiuliza kwa nini madereva wanaongozwa na taa za barabarani au trafiki polisi hali wamesoma sheria za barabarani na ni watu wazima? Nini hasa kinachowafanya kuongozwa kama watoto wasio na maarifa? Nikagundua kwamba ingawa mwanadamu amesoma lakini bado hawezi kujiongoza mwenyewe.,
Ingawa mtu ni mwenye akili lakini bado hawezi kutumia akili zake kujiongoza! Hapo ndio utaona kwamba kila mmoja anahitaji kuongozwa,hata kama mtu awe wa namna gani lakini bado atahitaji msaada wa kuongozwa,ikiwa ndivyo ilivyo basi“ushauri ” ni kiongozi cha mtu.
Kwa hiyo utaona madereva wanaendesha wakiziangaria taa za barabarani, ikiwa taa zitawazuia basi hapo dereva hana budi kutulia,na endapo taa zitamruhusu,basi atakwenda. Au endapo taa zitamwelekeza akate kushoto,basi dereva hana budi kukata kushoto. Ingawa maamuzi ya kukata kushoto yametolewa lakini dereva anaweza akakataa kukata kushoto na kuamua kunyoosha au kukata kulia.
Na hapo ndipo uharibifu utakapompata,kwa maana amekataa kufuata maelekezo sahihi yaliyotolewa bali dereva kaamua mwenyewe kufuata taratibu zake mwenyewe, hakika atahangamia. “ Neno la Mungu ” ndio elekezo kuu,kukuonesha ni nini unapaswa kufanya,ni wapi utaelekea!.
Lakini ushauri unapotolewa vibaya,hupotosha mwelekeo mzuri. Ushauri mbaya huleta uharibifu mkubwa sana. Fikiria taa za barabarani zikidanganya / kuelekeza vibaya,vipi dereva akiyafuata maelekezo hayo,ataishia wapi? Hakika atapotelea mbaya kwa kufuata maelekezo/mapendekezo mabaya! Endapo dereva akigundua maelekezo anayopewa si sahihi,ana uwezo wa kuyakataa na hiyo ndiyo itakayokuwa ndio salama yake.
Kuna watu wanaushauri mbaya siku zote kama “ Memukani“. Memukani alikuwa mmoja wa maakida saba wa Uajemi na Umedi katika kipindi cha Esta. Huyu,alikuwa mmoja kati ya watu waliokaa karibu na mfalme,waliweza kuuona uso wa mfalme kwa ukaribu. Kupitia kitabu cha Esta katika sura yake ya kwanza,
biblia inatoa simulizi ya kiroho iliyobeba wahusika katika mwili ili kusudi yeye asomaye apate kuelewa kwa haraka. Simulizi inatuambia namna ya sherehe kubwa ya namna yake aliyoifanya mfalme. Kwenye biblia nzima hakuna sherehe / party bab’kubwa kama hii,biblia hajarekodi sherehe kubwa kama hii,isipokuwa ile tu ya mbinguni.
Sasa mambo yalipoenda vibaya pale malkia Vashti alipokataa kuja kujionesha mbele ya mfalme,hapo ndipo Memukani alipoingilia kati jambo hili,wala yeye Memukani hakuwa mfalme lakini kwa kuwa alikuwa na kibali,akashikia kidedea jambo hili,katika ushauri.
Ushauri wake ulimwondoa malkia Vashti kwenye enzi yake,ushauri wake ulileta utata mkubwa kiasi kwamba hasira ya mfalme ikaongezeka. Memukani hakuwa mshauri mzuri,lakini alikuwa ni mtu mwenye nafasi na kibali kwa mfalme. Ni hatari kama nini ukiwa na mtu kama Memukani katika ofisi yako,
Au Memukani akiwa hapo nyumbani kwenu maana kwa sababu ya kuwa na kibali na boss wako,au mtu wa juu yako,aweza kushauri chochote kile na hatimaye maamuzi yakafanyika. Ushauri wa Memukani una hila ndani yake,si ushauri wa kujenga.
Hatari kubwa ipo juu ya ushauri wake kwa yule mwenye mamlaka juu yako. Kuna watu ambao wana ushawishi mkubwa na wanasikilizwa sana na kiongozi wako,watu wa namna hii wanasikilizwa sana katika ushauri wao. Hata kama wakishauri ujinga,ujinga huo mbele za boss /kiongozi wako sio ujinga,utakuta boss haoni kabisa kama ni ushauri mbovu,lakini cha ajabu kile alichosema Memukani kinafanyiwa kazi mara moja bila kuajali matokeo yake yatakuwaje. Biblia inamtaja Memukani kama mtu yule anayewakilisha kutoa ushauri / maelekezo yasiyofaa,mashauri yaliyojawa na matakwa yake binafsi ( personal interest)….
ITAENDELEA…
Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900
Na.Mch. G.Madumla
Whatsapp namba +255 746 446 446
UBARIKIWE.
Comments