top of page

LAANA YA WAZAZI.

Updated: Aug 26, 2022

“Maana wakati mwana wa Yese akiwa hai juu ya nchi, wewe hutafanikiwa, wala ufalme wako. Basi, sasa peleka, ukamlete kwangu, maana hakika yake atakufa huyu.” 1 Samweli 20:31

Sauli kama baba mzazi wa Yonathani ( 1 Samweli 19:1) amemkasilikia mwanae na anajikuta akishindwa kuzua hasira zake ,kinywa kimeshindwa kujistili,anajikuta sasa akimtukana matusi makubwa ya “nguoni” mwanae tena anamtukana hadharani,akimwainisha,utafikiri huyo kijana siye mwanaye wa kuzaa. Lakini Sauli anaendelea kumwaibisha mwanaye,sasa anajikuta “akimlaanai mwanae ” maana Sauli anamwambia mwanae “hutafanikiwa wala ufalme wako hautafanikiwa” .


Kwa maneno hayo, Sauli anabomoa mafanikio ya mwanae na hiyo ndio furaha yake,amesahau kwamba kushindwa kwa mwanae ni kushindwa kwake na kufanikiwa kwa mwanae ni kufanikiwa kwake ( maana kama mtoto atafanikiwa basi mzazi amefanikiwa na kama mtoto wako akifeli,ujue wewe pia umefeli)


Angalia vile mzazi asemavyo kwa mwanae“hutafanikiwa,wala ufalme wako” Maneno hayo yana nguvu ya kuleta athari katika maisha ya Yonathani. Maana yametoka kwenye kinywa cha mzazi anayejitambua nini anatamka pamoja na kwamba mzee huyu (Sauli) alikuwa akisumbuliwa na mapepo.Hivyo,


kumbuka ;


Lengo la huyu mzee kumtamkia mwanae maneno mazito kama hayo,lilikuwa ni “kumlaani mwanae” asiambatane na Daudi. Hasira ya mzee Sauli ilisababishwa na roho mbaya ya mauti maana alimtafuta Daudi mara nyingi amwangamize,lakini hakufanikiwa kwa sababu Daudi mwenye haki alikuwa akilindwa na Bwana,hivyo mzee anamgeukia mwanaye Yonathani na kumlaani.


Nataka uone vile wazee kama Sauli wanavyochangia kuwakwamisha vijana wao kwa “laana ya maneno “ wakidhani wanawakomoa vijana wao lakini hawajui wanajikomoa wao wenyewe kwa maana mtu kama Sauli yeye mwenyewe anahitaji msaada kutoka kwa mwanae Lakini huyo mwanae ndiye anayemlaani asifanikiwe,Sasa atasaidiwa na nani ikiwa mtu anayemtegemea ndiye anayemlaani ?

Leo pia tunao wazee kama Sauli ambao kwanza wameshachoka,umri umekwenda sana na kwa kweli ni watu wanaohitaji msaada wa vijana wao,lakini kwa bahati mbaya vijana hao wanatamkiwa laana kila siku na wazee hao hao,sasa watasaidiwa na nani? Unajua wezee wengine wanazingua sana!!


Kwa maana hawaishi kuwalaani vijana wao ambao ndio wanaowategemea. Sauli badala ya kumtamkia mwanae baraka za kufanikiwa yeye “anaachilia laana”. Hivi ndivyo akina Sauli wa leo wakifanya kwa vijana wao.


  • Namna ya kuikwepa laana ya mzazi kama Sauli


1.Kunyamaza na kuondoka ikiwezekana.


Jifunze kwa Yonathani,babaye alipomtukana na kumwaibisha mbele za watu. Yonathani hakujibizana na baba yake bali aliona ni vyema kuondoka,hiyo ndio ilikuwa pona yake . Lakini laiti kama Yonathani kijana angelijibizana na baba yake, matokeo yake yangelikuwa mabaya kwa maana baba yake Sauli labda angempiga,au wangepigana. “kunyamaza kimya na ikiwezekana kuondoka” ni njia mojawapo kubwa ya kutumia tu utashi wako kukwepa laana ya mzazi wako kama Sauli.


2.Maombi.


Lakini pia kumwombea Sauli wako ambaye naye anasumbuliwa na roho mbaya / mapepo. Kwa sababu tunaamini katika nguvu ya maombi usikome kuomba,kuna siku usiyodhani Bwana aweza kumgeuza. Pia kumbuka nguvu ya maombi inadhohofisha laana ya mzazi wako,kwa hiyo ajapotamka maneno mengi kiasi gani,kama unaomba,basi hayo maneno yatabaki kama makapi yasiyo na nguvu ya kuwa halisi.

Kwa msaada zaidi,nipigie kwa simu pia ukiwa umebarikiwa nifahamishe,namba ni +255 683 877 900.


What’s app number ni +255 746 446 446.


Na Mch. Gasper Madumla.


UBARIKIWE.

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page