top of page

UNAHESABIWA HAKI KWA IMANI TU, BILA MATENDO.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Fikiria mtu mmoja ambaye atajitoa sana kuwasaidia wahitaji kwa pesa na mali zake, tena wakati mwingine yupo tayari kumpa mhitaji maskini nguo zake nzuri na kufanya mambo mengi mazuri kwenye jamii. Lakini mtu huyo akawa mbali na kumwamini Bwana, hajaokoka. Je unadhani mtu huyu akifa, ataingia mbinguni kwa sababu ya misaada yake tu aliyekuwa akiitoa? Je misaada yake inaweza kumwokoa na ule moto wa Jehanamu ikiwa amemkataa Yesu?

Ukweli ni kwamba hawezi kuokoka kwa sababu ya kujitoa kwake. Je ni nini alichokuwa akihitaji zaidi,? Jibu ni jepesi kabisa, alikuwa akihitaji “kuokoka, kumpokea Bwana, na kumwishia Mungu ” Kumbe maana ya kuokoka hajafungiwa kwenye eneo moja la kuwasaidia wahitaji bali ni kuamwamini na kumpokea Bwana.

Leo kumezuka mafundisho ya ajabu mengi, na tumejikuta hatujui lipi la kushika na lipi si la kushika. Kwa sababu kila mmoja amejaribu kujitengenezea msimamo wake binafsi nje ya neno la Mungu. Moja kati ya msimamo uliotukumba wengi ni juu ya wokovu. Kwa jinsi gani mtu anaweza akaokoka? Hilo ndilo swali mama lililojengewa mtazamo usio sahihi kibiblia. Msimamo au mtazamo usio sahihi ni “mtu awe na imani kwa Bwana kisha lazima atende mema kama kwenda kanisani, awe mtoaji n. k kisha ndio aokoke” Lah! Si hivyo tunavyoambiwa kwenye neno!! Ngoja nijaribu kulichora wazo hilo kwenye lugha ya kihesabu / kimahesabu, na linawezekana kuwa hivi;

“ Imani + matendo / kazi = kuokoka. In English ; Faith + works / good deeds = Justification. “. Huo ndio mtazamo tulionao makanisani leo. Umenielewa? Bado, ujaelewa naona… Ni hivi, watu wengi wanajua kwamba ili uokoke basi lazima uwe na imani pia ujitahidi kuwa na matendo mema. Ukweli ni kwamba kinachotahitajika kwenye kuokoka ni “kuwa na imani tu, kisha unaokoka. Kihesabu ni sawa na kusema ; Imani + bila matendo = kuokoka Faith +nothing = Justification “. Ni kweli unahitajika kumwamini Bwana Yesu, kisha kukiri kwa kumpokea Yeye Bwana, bila kuwa na jitihada zako nyingine za kimatendo au kazi fulani, kumbuka neno hili ;

“ Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.“ Wagalatia 3:11

Matendo mema yanafaa sana, lakini sio kigezo cha kumfanya mtu ahesabiwe haki. Kwa maana tunahesabiwa haki kwa “ imani” (Waefeso 2:8). Sisemi usiwasaidie wahitaji, hapana bali nataka ujue kwamba kuwasaidia wahitaji sio ndio kuokoka. Bwana anachokihitaji kwako, ni wewe “kumwamini Yesu, awe Bwana na mwokozi wako ” bila kujali unafanya nini sasa, kwa maana imani tu yatosha. Inawezekana wewe ulihubiriwa au kufundishwa kwamba “huwezi kuokoka mpaka ufanye jambo la kwanza, la pili, la tatu na la nne, kama kanuni” hapana, kwa maana kama ingelikuwa hivyo basi ukweli ni kwamba hakuna angeliweza kuokoka hata mmoja!!! Kwani hujasoma injili ya Bwana, na namna nyaraka za mtume Paulo zinavyoelezea habari za wokovu? Ilikuwa ni kwa imani tu, hata mtu mmoja aliye dhambini kutubu na hatimaye aokoke. Unafahamu hata Petro alipokuja kwa Bwana, je alihitajika matendo mema kwanza? Biblia inasemaje? ;

“ Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.“ Mathayo 9:9.

Mathayo alikuwa mtu wa ushuru, leo hii unapoambiwa mtu wa ushuru unapata picha gani ya kwanza? Bila shaka picha ya kwanza ni “mla rushwa” yaa, ni kweli, maana tumezoea kuwaona watoza ushuru wengi wakifanya hivyo. Hii inatuonesha kwamba Mathayo hakuwa na matendo mema la, hata moja katika kazi ya ushuru kama tunavyoweza kuiona leo. Lakini mbona aliokoka na kuwa mmoja kati ya mitume wa Bwana Yesu? Je ni matendo yake yalimwokoa? Hata kama angelitenda mema je angeliokoka kwa kutenda mema? Bila shaka Bwana hakuangalia matendo ya Mathayo, bali imani iliangaliwa.

Kwa sababu baada ya Yesu kumwambia “nifuate” Mathayo hakusitasita, bali “alimfuata” maana yake alipoisikia sauti ya Bwana hakungoja, bali mara moja akayaacha yote na kumfuata Bwana. Kumbe hata wewe huwezi ukahesabiwa haki kwa matendo yako, bali kwa imani tu. Na pale unapoisikia sauti ya Bwana kwa kinywa cha mtumishi wake awe mchungaji au mtumishi yoyote, hapo usichelewe chelewe, chukua hatua mara moja na kumfuata Bwana, okoka papo hapo kwa imani.

Lakini unapookoka, unatakiwa kutenda mema sana tu, kwa maana ikiwa kweli umempokea Bwana Yesu, uwe na uhakika atakeyekuwezesha kutenda mema ni Bwana wali si wewe, ila unapaswa kumwomba Mungu akusaidie katika hili. Waooh🙏🙏🙏

Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi, nipigie sasa kwa namba zangu zilizopo hapo juu. Na ukiona simu haikupokelewa kwa wakati au haipatikaniki, basi ujue nipo kwenye huduma, hapo niandikie ujumbe mfupi nami nitauona. 

Simu ni +255 683 877 900

What’s app ni +255 746 446 446

Na Mch Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page