top of page

UKO WAPI ?

Updated: Sep 29, 2022



Uko wapo ? /Where are you?


Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? ” Mwanzo 3:9. Hili ndilo swali la kwanza katika biblia yote,kwa mara ya kwanza Bwana Mungu anaanza kumwuuliza mwanadamu “uko wapo?”.  Baada ya Adamu na mkewe kutenda dhambi ya kuasi,waliona vyema wajifiche kati ya miti ya bustani,ili Mungu asiwaone. Hakika walijidanganya,kwa maana hakuna yeyote awezaye kujificha mbele za Mungu,Yeye Mungu anajua yote (Zab.139:1-5,Yeremia 23:23-24). Akili za mtu mwovu ni kujificha mbele za Mungu,kwamba Mungu asimwone;Lakini ni kujidanganya tu,kwa maana huwezi kumficha kitu Mungu. Bwana Mungu hali akijua mahali walipojificha Adamu na mkewe,na hapo amwuuliza Adamu “uko wapo?”

  • Je ni kweli,Adamu alikuwa hajui uwezo wa Mungu kwa Yeye hafichwi ni kitu?

Biblia hajasema kama Adamu alikuwa anajua kwamba hata kama akijificha ataonekana au la! Lakini ukweli ni kwamba Adamu alikuwa akijua uwezo wa Mungu,kwa maana wote wawili walikuwa na ushirika mzuri. Lakini sasa kwa nini alijificha hata akaulizwa ? Ndani ya Adamu aliyeanguka dhambini,kulikuwa na nguvu mbaya ya kiroho iliyoanza kutenda kazi pale alipoanguka dhambini,nguvu hiyo ndiyo iliyomsukuma Adamu na mkewe hata wakashauriana kujificha. Swali hili “uko wapi” linaulizwa kwa mtu aliyepotelea dhambini. Bwana anamtaka Adamu ajue kwamba sehemu alipo si sehemu yake anayostahili kuwepo.

Adamu alikuwa mbali na nafasi yake ya kiroho,yaani alitoka nje ya nafasi yake ya kiroho. Mungu anajaribu kumpa nafasi ya pili ya kurejea kwenye nafasi yake halisi. Swali analoanza nalo Mungu,limejawa na pendo pamoja na huruma kuu. Kwa jitihada zote alizonazo Mungu kwa watu wake waliopotea,Lakini bado yeye aliyepotea haelewi kama kapotea? badala ya kutafakari kujua yu wapi,bali aliyepotea anaanza kujitetea kwamba yeye hajapotea,isipokuwa mwenzake ndiye chanzo na ndiye mkosaji!!!!

Kigezo cha kujua upo wapi

  1. Ili ujue uko wapi sasa,itakulazimu kujua ulikuwa wapi?

  2. Itakulazimu kujua kwa nini upo hapo ulipo /Ni sababu gani zimekufanya umefikia hapo ulipo.

Tafakari hali yako ya kiroho na kiuchumi uko wapi?,

Inawezekana ukawa ni mtu wa Mungu kwa sasa,lakini ukijaribu kutafari miaka michache nyuma utagundua kwamba kuna mahali kiroho ulikuwepo,lakini sasa umesogea nje mstari huo wa kiroho. Wengi watakaotafakari kule walikukuwepo kiroho watagundua kwamba kwa sasa hawapo hapo tena,wachache wameongezeka,lakini wengi wameshuka kiroho. Sasa leo Mungu anakuuliza “uko wapi?”


Kwa lengo la kukutaka urejee kwenye nafasi yako ya kiroho. Tafakari sasa,uko wapi kiroho?. Ikiwa umegundua kwamba umeshuka sana kiroho,basi ujue Bwana anasema na wewe leo . Katika uchumi,wengine walikuwa wameshamiri lakini sasa wamepotea kutoka katika sehemu yako ya kwanza,Je unafikiri kwa nini upo hivyo ulivyo sasa? Mbona wenzako mliokuwa nao leo,wameshamiri kiuchumi? Upo wapi?


Swali ili,“uko wapi” linalenga sana katika nafasi yako ya kiroho. Ikiwa upo mbali na Yesu,hujaokoka basi ujue Bwana anakuhitaji akikuuliza uko wapi?. Inaoyesha wazi kabisa kwamba uinjilisti ulianzia kwa Mungu mwenyewe kwa maana ni Yeye ndiye mwanzilishi wa kutafuta waliopotea. Moyo huu,wa kutafuta waliopotea dhambini,ni moyo wa Mungu ambaye Yeye hafurahii kufa kwake mwenye dhambi (Ezekieli 18:23),


bali yeye hufarahia kuona kila mtu anaifikiria toba (2 Petro 3:9). Anza kujihoji kuhusu uhusiano wako na Mungu,uko wapi? Kisha waweza kunipigia kwa simu ili tushauriane na kuomba pamoja.


Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900


Na.Mch. G.Madumla


Whatsapp namba +255 746 446 446


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page