top of page

NANI ANAYESTAHILI MSAMAHA?

Updated: Sep 30, 2022


Je unastahili msamaha? Unafikirije? Ikiwa ndio,ni kwa nini? La kama sio ni kwa nini basi? Ni kweli kabisa ukatambua jambo hili ili liwe msaada kwako na kwa wengine. Nimegundua kwamba maswali tunayoyadhania kuwa ni mepesi au marahisi ndio maswali msheria. sana kuliko tunavyodhania.


Mwalimu alituuliza “ni nani anayestahili msamaha” nami nikaona swali jepesi mno kabla sijajibu mtu mmoja akajibu,akasema “ kila mtu anastahili msamaha” jibu hili ndilo nililokuwa nalo,lakini pia wengi tulifikiri hivyo. Mwalimu akasema mmekosea! Hivyo nataka nikushirikishe tafakari hii pamoja nawe,kujibu swali hili muhimu. Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayestahili msamaha,kwa sababu;


  • Tulistahili mauti. ( Warumi 6:23)


Wanadamu wote tumefanya dhambi,na mauti kama malipo yetu,imetufikiria sote ( Warumi 5:12),hivyo kwa sababu ya dhambi tunastahili adhabu ya mauti na wala si msamaha. Ebu fikiri hivi; ikiwa umekosa katika jambo fulani, labda umevunja sheria za nchi. Hapo kitakachokustahili ni kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Ndio maana mtunga Zaburi akajiandikia, “BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu,Ee Bwana, nani angesimama?“


Zab.130:3 maana katika kufikiri,akaona hakuna aliyekosa kutenda dhambi pamoja na wewe. Neno la Mungu limeweka wazi kwamba hatukustahili msamaha bali adhabu kwa maana sote tumetenda dhambi ( Warumi 3:23). Hivyo,kwa kuwa tumezaliwa sote kwenye asili ya dhambi, kwa kosa lake mmoja,kila mmoja alistahili hukumu tu! Ukihisi kama ulikuwa unastahili kusamehewa ni lazima ujiulize,kwa lipi ulilolifanya jema,kwa haki gani uliyokuwa nayo hata ukastahili kusamehewa? Ukitafakari hilo,utagundua kwamba hakuna chochote kitakachokupa uhalali wa kustahili kusamehewa!!!


Lakini je ukiwa na mtoto aliyekukosa,anastahili kuonywa / kuadhibiwa?

Ebu fikiria hilo,je utamwadhibu mtoto wako aliyekukosa? Au utamsamehe? Bila shaka unaweza ukampa mapigo au ukamsamehe tu! Yote mawili yanawezekana. Lakini ni kipi alichokuwa anastahili kukipata kama matokeo ya kosa lake ikiwa ulikwisha mwambia mapema kwamba ikiwa kama utafanya hivi nitakuchapa? Bila shaka alistahili kuchapwa,lakini ikiwa kama utamsamehe kumchampa hapo ni lazima mtoto huyo afahamu ya kwamba msamaha aliyopewa hakustahili kupewa lakini kwa pendo,huruma ya mzazi wake,hakumchapa.


  • Neema tu ya Kristo imetuokoa ( Waefeso 2:8)


Neema ya Bwana imezidi sana kwetu hata tupo mbali na adhabu yetu tuliyoistahili ( Warumi 8:1). Neema ya Bwana ni ya ajabu sana,yashangaza mno! Kwa neema hiyo,tumejikuta tumejisahau sana hata kufikiri kwamba msamaha ni stahili yetu na kumbe sivyo!!! Hujawahi kuona mtu anatenda dhambi hali akijua ya kwamba baade ataomba msamaha kwa Mungu kisha anayendelea kutenda dhambi ile ile huku akipanga kuomba msamaha?


Hali hii inaonesha mtu huyo labda hajui afanyalo au ameizoelea neema ya Bwana na kuona anastahili kuishi hivyo! Mimi huwa ninatafakari sana katika eneo hili,na kuona kama isingelikuwa ni neema hiyo,hivi leo hii tungelikuwa wapi? Sijui kwa kweli.


Neno “kustahili / deserve” lina maana ya haki unayopaswa kupewa. Ikiwa kama unafanya kazi “unastahili” kulipwa sawa sawa na makubaliano mliyowekeana. Ikiwa kama unafanya kazi halafu hukulipwa,basi unayo haki ya kushtaki ili ulipwe kile unachostahili.


Tunapozungumzia kustahili katika eneo la msamaha,tuna maana ya “haki au uhalali wa kusamehewa” sasa ukicheki kuzaliwa kwako hata hapo ulipo utagundua yale uyapatayo,kwa kweli ni kwa neema tu wala hustahili hata huo msamaha.


Kwa msaada zaidi pamoja na maombi piga kwa +255 683 877 900


Whatsapp numba +255 746 446 446


Na Mch.G.Madumla


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page