KWA JINSI GANI MUNGU ANAWASILIANA NASI?
- Mch. Gasper Madumla
- Nov 10, 2018
- 3 min read
Updated: Sep 30, 2022

How does God communicate to us?
Shalom…
Kwa ufupi sana.
Tangu hapo awali ilikuwa ni utaratibu wa Mungu kuwasiliana na watu wake. Biblia inatuambia Mungu alikuwa akishuka kuwasiliana na Adam ( Mwanzo 3:8). Bila shaka kulikuwa na mawasiliano ya karibu sana kati ya Mungu na Adamu. Kumbe suala la mawasiliano lilikuwepo sana. Lakini je hata leo Mungu anawasiliana nasi? Hilo ndilo swali muhimu kujiuliza.
Bila shaka Mungu anawasiliana nasi hata leo akitumia njia nyingi na mbali mbali. Lakini ni kwa njia ipi hata tunawasiliana na Mungu au ni njia ipi tunaweza kuwa na mawasiliano? Katika hili jifunze kwanza,Mawasiliano bado yapo. Moja kati ya njia muhimu ambayo Mungu ameiweka ya kuwasiliana naye ni njia ya maombi.
• Kwa njia ya maombi.
Njia hii ni sisi ndio tunanyenyekea kwake na kuwasiliana, hivyo Kwa kuwa maombi ndio njia muhimu na ya kipekee ya kuwasiliana naye ( Isaya 43:26). Katika maombi tunapata namna ya kuwasiliana naye na ndio maana yatupasa kuwa rohoni ( kuwa watu wa rohoni) ili tuwasiliane vyema na kuelewa nini Mungu anasema.
Ni sawa na kusema kwamba kama usipokuwa rohoni utashindwa kuelewa kile asemacho Mungu kwa sababu Yeye ni Roho ( Yoh.4:24). Kuna gharama ya kuwa mtu wa rohoni. Kama ndio kwamba ipo gharama,basi pia ipo gharama ya kuisikia sauti ya Mungu na kuielewa kwa kigezo hicho hicho cha kuwa mtu wa rohoni.
• Kwa njia ya neno lake. Lakini pia namna nyingi hata nyingine hazichunguziki. Ila kuna namna ambayo Mungu pia hutumia kama namna ya kumtambua. Nataka nikutambulishe njia nyingine muhimu sana. Ambayo kwa njia hiyo tunanaweza kutambua;
Uwepo wake.
Kusikia nini anawasiliana nasi.
Hivyo Mungu hutumia ;
Ufunuo ( Revelation)
Ufunuo ni kufichua kitu / kukifanya kitu kilijulikana kile kilichokuwa hakijulikani ( Revelation is to uncover something which was covered or to make known what is unknown ). Hapa ni muhimu kutambua kwamba Mungu ni Mungu wa ufunuo,Ni Yeye ambaye hujifunua kwetu ili sisi kwa ufahamu na akili zetu za kibinadamu tupate kutambua uwepo wake na kujifunza siri za ufalme wake.
Aina kuu mbili za ufunuo kama njia ya mawasiliano kati ya Mungu na wanadamu;
Ufunuo wa ujumla ( general revelation)
Ufunuo binafsi ( special revelation)
01. Ufunuo wa ujumla ( general revelation)
Hapa Mungu utamia uumbaji wake na matendo makuu aliyoyafanya. Vile unavyoweza kuona mbingu ilivyosimama bila nguzo,hapo unatambua ya kwamba Mungu yupo. Biblia inasema ;“Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.” Zab.19:1 . Hivyo “ kila mtu ” anatambua uwepo wa Mungu kwa kuyatazama maajabu ya Mungu. Na ndio maana huitwa ni general revelation. N.K
02.Ufunuo binafsi ( specific revelation )
Njia hii ya ufunuo hupata watu wachache. (This is supernatural method where by few persons have it) . Ufunuo wa namna hii ni kama vile kupitia ndoto,maono,kwa njia ya biblia,kuokoka ( maana neema),kwa njia ya karama n.k. Mungu anaweza kutumia njia ya maono kusema na watu wake. Sasa si wote watakaopata maono isipokuwa ni wachache,ebu cheki mifano ukianzia kwa Daniel alikuwa akipata maono. Au Mungu anaweza kutumia neema ya wokovu,kwa wale walimkubali Kristo Yesu,ili aseme nao mambo siri ya ufalme wake. Sasa ukiangalia pia katika hili utagundua kwamba si wote wameokoka.
Wakati mwingine muujiza na ishara hutumika kama special revelation. Kwa mfano unaweza ukamwona Mungu katika ugonjwa fulani na kupitia huo Bwana Mungu akajifunua. Ni Muhimu kujua Yeye ni Mungu asiyekuwa na mipaka wala hazuiliwi na chochote. Hivyo uponyaji katika ugonjwa ni moja ya ufunuo binafsi. Je hujawai kuona mtu hakuweza kuwasiliana tena wala kuisikia sauti ya Mungu mpaka pale alipopitishwa kwenye ugonjwa fulani? Ndio yapo mazingira mengi tu kama hayo.
Je umeona uwepo wa Mungu?
Bila shaka jibu ni ndio kwa maana katika “ufunuo binafsi” utagundua Mungu yupo kwa kuangalia tu vilivyoumbwa ( when you see the several creatures, you will come to say that there is must a God who is Almighty). Huitaji kufundishwa kama Mungu yupo. Lakini kwenye “ufunuo bifsi” ni wachache tu. Sasa uombe neema ya Mungu ili katika hao wachache nawe uwemo.
Ikiwa kama umejifunza kitu katika ujumbe huu leo,basi naomba kujua kutoka kwako.
Pia ikiwa unahitaji huduma ya maombi basi usisite kwa kunipigia kwa + 255 683 877 900
WhatsApp in .+255 746 446 446
Much. Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
Comments