top of page

UINJILISTI NI NINI?


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Neno “uinjilisti” ni neno la kiswahili limetokana na neno injili. Hivyo ni vyema kufahamu kwanza “ injili “ni nini  kisha ndipo ujifunze maana ya uinjilisti. Kwa mujibu wa biblia takatifu,injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye,kwa Myahudi kwanza na kwa Myunani pia ( Warumi 1:16). Neno“uweza wa Mungu” ni habari njema zenye kuleta wokovu. Ni lazima ujue kwamba habari njema huleta wokovu,lakini kwa yule aaminiye.

“ kwa Myahudi kwanza na kwa Myunani pia” injili inapaswa kuanzia Yerusalemu kwanza kisha iende kwa wamataifa hii ikiwa na maana kwamba injili yako kwanza ihubiriwe nyumbani kwako kwanza ili watu wa nyumbani mwako waletwe kwenye wokovu kisha ndipo uwahubirie wengine walio nje. Watu wa kwako wanapaswa wapokee uweza wa Mungu uletao wokovu kwanza,kabla ya wengine.

Unawezaje mtu wa mbali aokoke ikiwa umemuacha baba yako,hujamwambia aokoke??? Au unawezaje kutumika kupeleka uweza wa Mungu uletao wokovu kwa jirani zako ikiwa watu unaoishi ndani ya nyumba moja hujawapa uweza huo? Lakini ndivyo ufanyavyo wewe,upo tayari kuwaambia watu wageuke na kuacha maovu ya dunia hii hali mkeo unayelala naye kitanda kimoja hujawahi kumueleza ujumbe huo!!! Ukiwa unafanya hivyo,basi utambue bado hujaifahamu injili ni nini,maana injili inaanzia nyumbani mwako.

Maana ya uinjilisti ipo tofauti kidogo kwa sababu imepanuka sana kimaana. Mojawapo ya huduma zile tano alizozitoa Bwana,wainjilisti walikuwa ni miongoni mwa huduma( Waefeso 4:12) ikiwa kama wainjilisti wametajwa kama sehemu ya huduma zile tano,basi ni sawa na kusema uinjilisti ni ofisi kamili kati ya ofisi zile nne zilizobakia sawa sawa na Waefeso 4:12. Nataka kwanza ufahamu uinjilisti kama ofisi maalumu kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu,hata kazi ya huduma zote zitendeke hata mwili wa Kristo ujengwe.

 Ukianzia kuutazama“uinjilisti“kama ofisi ya Bwana wakaao watu wenye uweza wa Mungu uletao wokovu kwa yeyote aaminiye,utagundua kwamba si wote watakaoitwa kwenye ofisi;na huu ndio ukweli wenyewe,mwinjilisti ni lazima uitwe au itengwe na Bwana. Ukiona mtu kajiendea mwenyewe kwenye ofisi ya namna kama hii,bila kujisikia sauti ya Mungu,basi ujue hajui mambo kihuduma.

Pili,kwa mujibu wa biblia,uinjilisti ni mojawapo ya karama yaani ni utendaji kazi wa Roho mtakatifu ndani ya mtu ashuhudiae (mwenye kuinjilisha ) matendo makuu ya Mungu kwa leo la kuokoa roho za watu wasiingie jehanamu ya moto. Watu wa namna hii wanakuwa na mzigo kubwa kuwaeleza watu wengine habari saa za injili na uzima wa milele na kwa sababu hiyo wanachukia sana kitu kinachoitwa“dhambi”. Kwa kuwa Yesu yeye mwenyewe alizifia dhambi zetu msalabani,hivyo mwinjilisti huchukizwa kumuona mtu anayeifurahia dhambi.

Uinjilisti umebeba huruma ya Mungu juu walimwengu,na ndio maana usishangae umuonapo mwinjilisti akilia mwenyewe dhidi ya watenda dhambi! Yaani mwinjilisti anaumia kiasi kwamba analia akiona huruma juu wote ambao bado hata sasa wapo dhambini tena zaidi sana kuona watu wasiookoka kwa sababu yoyote ile. Moyo huu haupo kwa watu wote isipokuwa wale walioitwa,maana ni vigumu kumuona mtu mzima akitokwa na machozi eti kwa sababu ya mtu mwengine anafanya dhambi,tena mtu mwenyewe hata hamjui! Bila moyo huu hauwezi!

Yesu naye alikuwa akifanya kazi kwenye ofisi zote tano (ualimu,utume,unabii,uchungaji pamoja na uinjilisti). Ukiwa msomaji mzuri wa neno utagundua hilo. Katika eneo la uinjilisti Yeye mwenyewe alikubali kufa kwa ajili yetu maana alikamatwa sana na huruma ya Mungu na kusudi aibebe ghadhabu ya Mungu kwa ajili yetu sote ulimwengu ili sasa kila amwaminiye awe na uzima wa milele na kwa sababu hiyo,maana ya uinjilisti ikapanuka. 

Kila aliyeokoka sasa anakusudiwa afanye kazi hii ya injili ( ingawa bado watakuwepo wachache watakaokuwa ni wainjilisti kwa maana ya karama ) kwa watu wote. Hata wewe unapaswa uwape watu waliko karibu nawe injili ya Bwana. Angalia;unaweza ukawa si muinjilisti kwa karama lakini kitendo cha kuokoka basi hapo unatakiwa umzalie Bwana matunda kwa kazi ya uinjilisti. 

Inakuwaje hii?

Nyumbani mwako unawaambia habari za Yesu,ofisini mwako mtu mmoja mmoja unampasha habari za Yesu na kumwambia YESU ANAWEZA HIYO SHIDA,NJOO KWA YESU ATAKUPONYA hivyo tu! Au waweza kuinjilisha kwa mali zako au pesa zako ukawa patner / mtu unayesapoti injili na wainjilisti waendapo kuhubiri na hapo wala huitaji uwe na mabilioni bali unahitaji uwe na moyo wa kutoa chochote ulichonacho kwa ajili ya kazi ya injili na ukifanya hivyo utakuwa umeinjilisha kupitia mala au fedha yako. N. K

Na ukifanya hivyo,ujue Mungu ambaye anapenda watu wote waokolewe na kupata kujua kweli basi ( 1Timotheo 2:3_4),Yeye Mungu hatakuacha hivyo hivyo bali atakubariki kwa baraka zote za mbinguni na duniani. Kumbuka,kuna furaha mbinguni kwa mtu mmoja mwenye dhambi atubuye ( Luka 15:7) 

Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900

Namba ya what’s app ni +255 746 446 446

Mchungaji Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page