MTU AKIONA KIU,NA AJE KWANGU ANYWE ~ Yoh.7:37
- Mch. Gasper Madumla
- Sep 2, 2017
- 2 min read

Na mch.G.Madumla.
Bwana Yesu asifiwe….
Imeandikwa “ Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.” Yoh.7:37
Kwa kawaida maana ya kiu katika maana nyepesi ni ile hali ya uhitaji wa kunywa kimiminika ( maji au juisi,n.k wakati mwingine hata vilevi). Ukiwa na kiu ya kunywa maji basi utajitahidi kwa hali na mali kutafuta mahali ambapo maji yanapatikana. Kiu inapelekesha mtu kiasi kwamba haivumiliwi!
Ukipelekwa kulala katika moja ya nyumba ya kijijini ambayo mitungi ya maji huwekwa ndani lakini kwenye kijumba kingine nawe unalala katika kijumba kingine. Ukiwa umelala kwenye nyumba ya namna hiyo,na gafula ukastuka usiku na kusikia kiu ya maji lakini ukipiga hesabu unagundua kwamba mtungi wa maji upo ndani ya kibada cha pili na muda huo ni usiku wa manane.
Nataka nikuambie kwa sababu ya kiu, utakwenda mwenyewe kutafuta maji kwenye kibanda cha pili na ingawa ni usiku wa manane lakini hutojali,bali ili mradi ukate kiu yako.
Jaribu kupata picha ukiwa jangwani mahali ambapo pana ukame pasipo maji,angalia hapo jinsi utakavyokuwa na kiu kiasi kwamba ukisikia kuna mahali maji yapo basi ujue utakwenda mbio tena waweza hata ukajisahau kuangalia usalama wako kule uendako.
Kumbe kiu inaweza kumpelekesha mtu hata asisikie maneno ya watu bali kiu kwanza akaitimize. Na ndio maana unaweza ukamuuzia maji ya chupa ndogo tu kwa yule mwenye kiu,ukamuuzia kwa gharama ya juu naye akanunua bila lawama,lakini kiu ikiisha ndipo lawama huja. Sasa hiyo ni kiu ya vinywaji. Kama ni hivyo,maana ya kiu inaweza kuwa kubwa sana. Yaani mbali na kiu ya maji,mtu anaweza akawa na kiu ya sigara,pombe,zinaa n.k
Sasa,kiu inayozungumziwa katika Yoh.7:37 si kiu ya maji tunayokunywa,wala sio kiu ya soda au juisi. Bali kiu inayozungumziwa hapo ni ile hali ya kupelekeshwa katika matendo ya mwili kama vile kupelekeshwa katika sigara,zinaa,pombe,madawa ya kulevya n.k vyote hivyo ni kiu inayowapelekesha watu wengi.
Bwana amefungua mlango wa kumuendea ikiwa kama una kiu,ili yeye aikate kiu hiyo. Wengi tuliomwendea Bwana tulikuwa na kiu zetu nyingi zilizokuwa ni mbaya,lakini hakika Bwana ameziondoa kiu hizo zote,na hatimaye sasa tu watumishi wake.
Kuna watu wamekamatwa na kiu ya zinaa,miili yao inawawaka na hawatulii kabisa kama vile wenye kiu ya maji wanavyoangaika kutafuta maji. Yesu anasema kwa mtu kama huyo na kwako pia,kama unakiu fulani inayokusumbua na kukupelekesha,basi uende kwake Yesu,na Atakupa maji yakatayo kiu milele ( Yoh.4:13-14).
Maji akupayo Bwana ni Roho mtakatifu yeye ambaye akiingia ndani yako hukata hiyo kiu ya dhambi milele. Kwa Yesu kuna maji ya uzima yakatayo kiu ya kila namna.
Jiulize sasa,ni kiu ya namna gani inayokupelekesha hata kukosa Mungu? Je ni pombe? Je ni wanawake? Je ni wanaume? Je ni kiua ya kusema uongo? Je ni sigala? Je ni kiu usagaji na ushoga? Je ni kiu ya namna gani hiyo?
Ukiwa na kiu hizo zote,kamwe hutatulia na utaona kiu muda wote lakini ukija kwa Yesu na kunywa hutaona kiu tena. Hivyo kiu inaondolewa kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako,kisha kuendea kukaza kwake hatimaye Roho mtakatifu akufulikishe aondoe kiu hizo tu
Naomba niombe na wewe leo,wewe ambaye unasema unasumbuliwa na kiu za namna nyingi na zinazokupelekesha kumkosa Mungu. Nipigie sasa kwa maombezi +255 683 877 900
What’s app number ni +255 746 446 446
Na Mch. G. Madumla
UBARIKIWE.
Comentários