top of page

UINJILISTI NI KAZI YAKO,USIIKWEPE !.

Updated: Sep 5, 2022

Injili lazima ihubiriwe.


 Shalom…

Kwa ufupi


Lengo la fundisho hili ni kukumbusha wajibu wako wewe mkristo,kwamba hukuitwa uwe mkristo alafu basi uishie hapo hapo bali umeitwa ili uwashuhudie wengine waliopotea dhambini. Kumbe unayo kazi ya kufanya. Kazi hii ya kumuhubiri Yesu haiangalii jinsia yako,umri wako,rangi yako,uzuri / urembo wako,kabila lako Bali kinachoangaliwa ni kimoja tu,Je umeokoka? Ikiwa ndio,basi na ujihesabu hivi,“wewe ni mtumishi wa Mungu na ni muhubiri injili”.


Ni kweli wapo watu walioitwa kuwa wainjilisti rasmi katika“ wito mkuu / special call “,watu hao waendelee kwenye kazi zao. Lakini kumbuka namna ya kuokoka tu,huo nao ni wito “ a general call” ambapo unapaswa kumshuhudia Yesu Kristo kwa mataifa yote. Je hivi unajua kuna watu hawajasikia injili mpaka sasa? Je unajua kuna watu wanahitaji kuokoka lakini wamekosa mtu mmoja atakayesimama na kuwaendea? Ni nani mtu huyo?


Ni wewe mpendwa! Ebu fikiria mpaka leo mama yako hajaokoka,ni nani amwendee kama si wewe!! baba yako je,mbona hajaokoka wala hujawai kusema nae ? dada yako mkubwa,au ebu mwangalie mjomba wako ambaye mpaka sasa amekuwa ni mlevi wa kupindukia,… Wewe utadaiwa damu zao watu hao,usipochukua hatua sasa!

Nimeogopa kama nini niliposoma Ezekieli 3:18 ,biblia inasema


“ Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.” Hivi unaposomaga biblia yako,huyaoni kweli haya maandiko? Au unapita tu na kuyapuuzia??? Ukweli ni kwamba damu ya ndugu zako itakulilia kwa sababu hukuwapa maonyo wayaache maovu yao.


Na huu ndio ukweli, kwamba nyumbani mwako,wapo watu ambao Bwana amewaandaa waokoke kupitia wewe baada ya kusema nao. Lakini ukikaa kimya labda kwa kuwaogopa,ujue utawapoteza. Ni vyema useme nao kama wakikataa hiyo ni juu yao,wewe kwa sehemu yako umenawa. Najua kwamba wengi huwaogopa ndugu zao hususani wale ndugu ambao wana mali “akina baba / mama fulani wenye pesa,maboss” lakini leo,sikia neno la Bwana ,Bwana anakukumbusha wajibu wako kwao,wewe ni bora kuliko pesa,mali wala chochote kile,nenda,nenda,nenda sasa…. Usiogope Bwana yu pamoja nawe ( Yoshua 1:9)


Ngoja nikwambie;

Siku moja nilikuwa na rafiki yangu mwinjilisti mmoja hivi. Tulikuwa tunaelekea uwanja wa taifa,kwenye mkutano wa injili. Umoja wa makanisa ya kipentekoste mkoa wa Dar TZ, walishirikiana kuundaa pamoja na wainjilisti kutoka marekani,ulikuwa ni mkutano wa mmoja wa mtoto wa R. Bonnke. Tukiwa kwenye daladala kuelekea uwanjani,daladala ilikuwa imejaa sana. Na kama kawaida ya wainjilisti hupenda kuona watu,ili wahubiri “ naipendaga sana hiyo“


Tulipowaangalia watu,tukasita. Mwenzangu ndiye haswa mwinjilisti kweli kweli,gafla akaanzisha “ Bwana Yesu asifiweeee,abiria wenzangu…” kwa kushangilia abiria wote wakaitikia “ ameeen mtumishi wa Bwana…. Piga injili baba…” kha! Kumbe daladala zima lilikuwa limekodiwa nalo lilikuwa linaelekea uwanjani taifa kwenye mkutano,kumbe walikuwa walokole wenzetu bhana. Basi tukachekaaaa. Tukanza nyimbo hadi uwanjani. Sasa nini nataka nikuoneshe hapo;


Wakati mwingine unafikiria umwanzaje mtu kumsemesha habari za Yesu,na kumbe mtu huyo ni wa Yesu tayari. Kumbe hutakiwi kusita sita,Kwa maana Bwana amekwisha kuwaandaa watu wake kwa ajili ya kupokea neno la Mungu kwa kinywa chako. Kwani nani alijua kuwa wale abiria walikuwa walokole wenzetu kama tusingelianzisha. ?Hata huko kwa ndugu zako,wapo watu ambao Mungu amekwisha waandaa,ni wewe tu unayesubiriwa kwenda ili kusudi la Mungu likamilike. Ni lazima waokoke hao kwa Jina la Yesu.?? Umeona hapo

Kwani uinjilisti ni nini hasa?


• Kwa lugha nyepesi kabisa ya kiswahili ;uinjilisti ni “ mawasiliano / mazungumzo ya habari njema za wokovu. Kusudi kuu la uinjilisti ni kutoa nafasi maalumu kwa watu wote wampokee Yesu Kristo. Uinjilisti una lengo kuu moja tu,la kuwatangazia watu habari njema za Yesu ili waokoke na kumtumikia Yeye Yesu ndani ya ushirika. “ Kwa lugha ya kiingereza ningesema


Evangelism is the communication of the good news.The purpose is to give individuals the valid opportunity to accept Jesus Christ. And the main goal is to persuade men and women to accept Jesus Christ as the Lord and savior and to serve Him in the fellowship in His church.


  1. Kumbuka mambo nane muhimu kujua kwa kila mwinjilisti.( Mambo haya,ni mfumo kamili wa kila injili,ukiyasoma na kuyaelewa,hakika utaweza kuinjilisha na utakuwa mwinjilisti mkubwa sana. Nimeandika kwa ufupi kukupa mwanga tu,waweza kunipigia nikueleze kwa marefu ikiwa kama una kiu ya injili.)

  2. Mungu / God “ Mungu anakupenda / God loves you ” Yoh.3:16

  3. Sote / All “sote tumefanya dhambi / All we’ve sinned ” Warumi 3:23

  4. Yesu / Jesus “Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu /Jesus died for our sin” Warumi 5:8

  5. Alizikwa / Buried “ Yesu alizikwa / Jesus was buried ” 1 Wakorintho 15:3b-4

  6. Kufufuka / Raised “ Yesu alifufuka / Jesus was raised ” 1 Wakorintho 15:3b-4

  7. Njia moja / One way “>Yesu ndiye njia pekee ya kwenda kwa Baba / Jesus is the only one way to God ” Yohn.14:6

  8. Imani / Faith “ Weka imani yako kwa Yesu / You must put you’re faith to Jesus ” Waefeso 2:8-9

  9. Maombi / prayers “ ungependa umpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi waa maisha yako? /Would like to received Jesus as the you’re Lord and savior? “Warumi 10:9, 1 Yoh.1:9.


Hayo mambo nane ni muhimu sana katika injili yako kuyahubiri. Kabla ya kumwalika mtu aje aokoke,yakupasa umwelezee kwamba Mungu anampenda mtu huyo,Tena kwamba sote tulitenda dhambi na Yesu alikufa kwa ajili yake pia alizikwa,akafufuka naye yu hai .Mtu huyo aweze kumwamini Yesu na hatimaye aweze kumpokea ili Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yake. Waaahooo!!!!


Ikiwa kama umepata kitu wakati ulipokuwa ukijifunza,tafadhali nifahamishe kwa namba zangu zilizopo hapo juu.


Na kwa maombezi vivyo hivyo piga kwa namba hizo hizo. 

Kwa mawasiliano piga sasa +255 683 877 900


Na Mch. Gasper Madumla.


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page