top of page

UWEZA WA JINA LA YESU.

Updated: Aug 29, 2022



Neno “Yesu” limetokana na neno la  Kiebrania “Yeshua/Yoshua” lenye maana ya “Mungu aokoaye”. Ni jina la Mungu wenyewe. Kwa kuwa ni jina la Mungu mwenyewe,basi ni jina la pekee,lililobora kuliko vyote na bora kuliko malaika ,naye Mungu alipenda kumrithisha mwanaye wa pekee jina hilo. Hivyo ni jina la kurithi – Waebrania 1:4


Ndani ya jina hili kuna kuna “uweza” wa ajabu. Tafsiri ya neno “uweza” inatofautiana na neno “uwezo” ingawa yote mawili yanazungumzia kuhusu nguvu. Tofauti yake ni kwamba “uweza” ni nguvu ya pekee amilikayo ya Mungu tu. Kwa nguvu hiyo,Mungu huwa Mungu. Bali “uwezo” ni nguvu ya kawaida inayomilikiwa na viumbe vyote kuanzia


mwanadamu,shetani,mapepo,majini,na viumbe vingine. Mfano Mungu ana uweza wa kuumba,au kurudisha uhai ndani ya kilichokufa, huo uitwa uweza,bali viumbe vingine havina nguvu ya kuumba au kurudisha uhai ndani ya aliyekufa.


  • Sifa za Jina la Yesu


Jina la Yesu limebeba uungu wote wa kufanya mambo ambayo hakuna awezaye kufanya isipokuwa Mungu tu. Hivyo limebeba sifa lukuki ambazo hakuna awezaye kuzieleza zote,maana ni nyingi mno hata kupita akili ya mwanadamu. Lakini hizi zifuatazo ni chache mno,

  1. Jina la Yesu ni tamu (lina radha,lapendeza)

  2. Huondoa hamu ya dhambi/linakata kiu ya dhambi

  3. Linaponya roho,mwili na nafsi

  4. Ni chakula cha uzima

  5. Ni msingi / Jiwe kuu la pembeni

  6. Ni ngome,ngao,mwamba

  7. N.k

Pamoja na sifa zote hizo,uweza wa jina la Yesu tunaona likidhihirika kwenye maeneo mengi. Nami nimechagua maeneo mawili tu,nayo ni;


1. Ulinzi wa kiroho na kimwili.(Yoh.17:12)


ENDELEA KUBAKI MAHALI HAPA, FUNDISHO HILI LINAENDELEA KUCHAPWA….

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page