UFAFANUZI KUHUSU AKINA MARIAMU WANAOTAJWA KATIKA AGANO JIPYA.
- Mch. Gasper Madumla
- Dec 10, 2018
- 2 min read

Bwana Yesu asifiwe..
Kwa ufupi.
Mara nyingi umekuwa ukisoma biblia na kukutana hasa na jina hili “Mariamu” . Hivyo jina hili si geni kwako ndivyo ninavyoamini mimi,lakini sidhani kama unajua kuwatofautisha akina Mariamu hao. Hivyo,jifunze sasa; katika agano jipya wanawake sita wana jina la Mariamu. Katika wanawake hao,wengine hawatajwi sana kwenye biblia,labda hawakuwa na habari nyingi kama wale wengine. Hivyo kwa mujibu wa agano jipya Mariamu wengine walikuwa maarufu kulingana na kile walichobeba.
Mariamu mama yake Yesu ( Mathayo 1:18). Mariamu huyu aliyemzaa Yesu ndiye aliyebarikiwa kaliko wanawake wote -( yapo mengi yakuandika kuhusu Mariamu mama wa Yesu, fuatilia mahali hapa)
Mariamu Magdalena ( Yoh.20:18,Mathayo 27:56)/ huyu alikuwa ni mfuasi wa Yesu, nae alitolewa mapepo ( Luka 8:2-3). Mariamu aliitwa Mariamu Magdalena kwa kuwa alitokea kwenye mji unaoitwa Magdala ndani ya Galilaya,na aliitwa hivyo kumtofautisha na Mariamu wengine.Lakini ukumbuke ya kwamba ni Mariamu huyu Magdalena aliyekuwa mwanamke wa kwanza kupokea na kuihubiri injili ya ufufuo pale alipofufuka Bwana.
Mariamu mama wa Yakobo na Yusufu ( alikuwa miongoni mwa wanawake waliomfuata Yesu kutoka Galilaya na kumtumikia ( Mathayo 27:56)
Mariamu yule mwanadada kule kwenye kanisa la Rumi kipindi cha Paulo ( Matendo 16:6)
Mariamu mama yake Yohana ( Matendo 12:12) – alikuwa mmoja wa wanamaombi kipindi cha Petro alipokuwa amefungwa gerezani.
Mariamu ndugu yake Martha na Lazaro. ( Yoh.11:1-2. Mariamu mwenyeji wa Bethania na huyu ndiye aliyempaka Bwana marhamu ya gharama. Lakini yeye pamoja na Martha wanatajwa pamoja. Wandugu hawa pamoja na Lazaro ni marafiki wa Yesu)
Hao ndio kina Mariamu katika agano jipya, lakini hata hivyo wanawake walikuwa hawako nyuma katika huduma ya Bwana,na ndio maana Bwana aliwatumia akina Mariamu kuonesha huduma inawahitaji sana akina mama na wanawake pia.
Ikiwa umebarikiwa na fundisho hili nifahamishe pia. Kwa maombezipia nipigie kwa namba hizi hizi + 255 683 877 900
WhatsApp ni .+255 746 446 446
Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comentários