top of page

TUNAMWITAJI FARAO?

question-mark-1019993_1280

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Je tunamwitaji Farao katika safari yetu ya wokovu?,Bila shaka tunaweza kusema ndiyo tunamwitaji ili atusukume tusonge mbele zaidi,na pia tunaweza kusema kwamba hatumwitaji Farao tena,kwa maana tutasonga mbele sisi wenyewe. Lakini tukitafakari safari ya ukombozi wa Israeli kutoka utumwani Misri tutapata jibu zuri zaidi.Maisha yetu ya wokovu ya sasa hayana tofauti kabisa na safari nzima ya Israeli kutoka Misri kwenye mikono ya mtesi wao Farao. Ingawa Bwana aliwakomboa,lakini bado Bwana aliwapitisha katika njia ndefu,kwa sababu Bwana alikuwa anawajua vyema watu wake kwamba wanaweza kurejea nyuma (Misri)watakapokutana na vita. Hii inatuonesha kwamba,ingawa walikombolewa lakini bado walikuwa ni watumwa wa fikra,walihitaji wawekwe huru katika fikra zao.

Lakini Bwana alimwacha Farao awafuatie nyuma,na biblia inasema wazi kwamba Farao aliwafuatia na jeshi lake,kiasi kwamba iliwabidi kutaharakisha safari yao kwa haraka kwa maana walijua kwamba ikiwa kama wahawatatoka kwa haraka,Farao atawaangamiza ingawa mbele yao kulikuwa na bahari. Kilichowasukuma haraka kuvuka bahari ilikuwa ni utisho wa Farao na jeshi lake. Kwa hiyo kwa namna fulani safari yao ya kutoka ilisukumwa na Farao,ingawa walikuwa hawamwitaji.

Leo pia safari yetu ya kusonga mbele na Bwana,inasukumwa sana na ibilisi ambaye ni kana kwamba ni Farao wa leo. Hakuna anayemwitaji ibilisi/shetani,lakini katika uwepo wake unatufanya kuwa hodari na washupavu katika wokovu wetu. Hujawahi kufikiri kwamba,maisha ya wokovu tuliyonayo yangelikuwaje pasipo ibilisi na majeshi yake? Mimi nafikiri labda watu tungebweteka mno,na tungejisahau sana. Sasa,shetani/ibilisi/farao sio mtumishi wa Bwana lakini,Bwana amemwacha aendelee kuwepo,kwa nini aendelee kuwepo? Hivyo Farao katika picha ya ibilisi,hatumtaki kabisa,na pia hatumwitaji katika wokovu wetu,lakini katika uhalisia wake ni kana kwamba tunamwitaji kwa maana katika kumpiga,ndio tunaposhinda na kuimarika katika safari yetu.

Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,basi nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja. Lakini inawezekana labda unahitaji MAOMBI kwa maana nawe unapitia changamoto hii,Basi kwa yote nipigie sasa kwa + 255 683 877 900

What’s app namba ni+255 746 446 446  (Jiunge pia na kundi la UJUMBE WA LEO kwa kutuma neno NIUNGE katika what’s app kwa namba hiyo hiyo)

Na Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Kommentare


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page