top of page

THE REASON WHY YOU WILL NOT BE VERY SUCCESSFUL! (MAANDALIZI… SABABU ITAKAYOKUNYIMA MAFANIKIO)

Updated: Sep 29, 2022

youth

Na Mwl.Andrea G.Muhozya



PREPARATION….! 


Watu wengi saaana duniani wanawaza kufanikiwa. Tena siyo kufanikiwa tu kufanikiwa sana! Kitu kimoja nimejifunza kuhusu kufanikiwa sana ni kwamba huwezi kufanikiwa #sana kama hujajiandaa kufanikiwa #sana


Mafanikio makubwa hayaji kwa maandalizi madogo! Mafanikio makubwa yanakuja kwa maandalizi makubwa tena ya muda mrefu.

Sasa unataka kuwa muhubiri mkubwa, international evangelist, mfanyabiashara mkubwa, mjasiriamali mkubwa, mwekezaji mkubwa, mwandishi mkubwa, motivational speaker mkubwa duniani, kwa maandalizi yapi labda? Twambie. Look at yourself and the things you desire! Halafu uone kama wewe unastahili mafanikio makubwa! Kutaka siyo ishu ishu ni je unastahili?


Bill Gates ‘kila mtu’ anamjua. Huyu Bwana ni mfano wa watu wanaojua hii kitu preparation. Baada ya kuingia ubia na IBM uliompa hela nyingi sana huyu jamaa aliona sasa nataka niwe tajiri mkubwa duniani. Na sehemu ya kutemgeneza pesa nyingi kwa kutumia software ni China! What he did aliamua kwenda course maalumu ya kujifunza kichina. Chinese language and culture. Alijua kuwa ili akanegotiate vizuri na wachina anapaswa kujua lugha yao na culture yao.


Alipoona yuko vizuri akaifata government of China akawapa offer ya kuwasambazia computer kwa ajili ya shule zote na computer zitakuwa na Microsoft iliyo katika lugha ya kichina. Wachina wakaona bonge la idea. (Wakati huo walikuwa na plan ya kuweka computer mashuleni kama hii ya Kagame hapo Rwanda) Wachina wakampa dili. The rest is history.! Ni wachache wanajua Bill Gates alianza kujiandaa akiwa 14 years old! Nilijifunza kitu kwa huyu ambacho kinanisaidia katika ndoto za kwangu mimi. 


Sasa wewe tuje kwako, hutaki hata kusoma vitabu vya ujasiriamali kila siku unaviona Ubungo mataa we kazi yako kununua ubuyu na ice cream. Vitabu eti ooh sina muda wa kusoma! DVD za mambo ya biashara hata ukipewa bure hutaki. Za muvi za Nollywood una Part I mpaka III. Muda huo unao. Hayo ndo maandalizi sahihi ya mafanikio makubwa? Ukialikwa semina ya ujasiriamali oooh imegongana na kitchen pati ya best yangu yaani I wish.. You wish what? Kitchen party ngapi ushaenda? Unacheka tu watu wanavyokatika viuno huko.


Sikia. You only get what you prepare for!


Maandalizi yako kama yanatosha kuingiza laki 5 Itakuwa hiyo hiyo all your life. Maandalizi yako kama yanatosha kuingiza 4 million I tell you utagota hapo. Maandalizi yako kama yanatosha kuingiza 100M utazipata! Maandalizi yako kama yanafaa kukupa 1Billion itakuja. You get what you prepare for. Kama MAANDALIZI yako ni madogo utapata matokeo madogo tu kama wanariadha wa Tanzania kwenye olimpiki! Moto mdogo huleta joto dogo. We unataka kushinda Gold Medal ya swimming kwenye olympics wakati hata humjui MICHAEL PHELPHS anaishije?


Kuna mpaka diet yake daktari wake, personal coach na team coach. Wewe ukiugua unaenda dispensary kupanga foleni. Mlo wako supu ya pweza. Kwani unaenda mashindano ya kuongelea au ya nguvu za kiume yakhe? Mazoezi yako hata hayaeleweki. Unataka kuwa the best footballer unajua what it takes?


Unajiandaaje? Kwani wangapi walitaka? Wangapi wameishia njiani.

Jiulize kwa maandalizi uliyonayo hapo ulipo sasa hivi miaka minne ijayo (2020) itakukuta unaingiza sh ngapi kwa mwezi kati ya hizi: 

Tshs 500,000/-, 

Tshs 5,000,000/- 

Tshs 50,000,000/- au 

Tshs 500,000,000/- kwa mwezi?. 


I’m telling you unaweza kujua hilo vizuri kabisa kama ukikagua maandalizi yako ya sasa. Usiseme Mungu atafanya. Mungu siyo houseboy wako. Mungu ashakupa hewa na uhai na watu na opportunity nyingi tu. It is up to you.


Huwezi kuwa muhubiri wa kimataifa wakati hata passport unasubiri mpaka utabiriwe kanisani ndo uende uhamiaji. Kwanza hiyo inaonyesha huamini ndoto yako! Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa na ndoto. Nikaamua kutafuta passport nikiwa namaliza chuo. Mwanafunzi tu. Coz nilisema I will travel a lot in future. Ndo kwanza safari zinakaribia kunoga leo. Passport yangu ilitumika mara ya kwanza three years later. Preparation. 


Huwezi kuwa Mwalimu wa kimataifa wakati hutaki kusoma vitabu kupata maarifa mpya kujifunza lugha za kimataifa. Binafsi 2012 nilisoma French course Alliance Française ikiwa ni Mara ya kwanza maishani mwangu, mwaka 2013 nikasoma Introduction to Chinese (mandarin) hapo UDSM Confucius Institute. Sasa hivi nasoma upya kiingereza ili niwe bora zaidi. Then nitaenda tena nextbstage ya French na Chinese. Na bado German, Spanish, and Russian. Coz I have MY BIG dreams. Ni mfano tu I am not bragging about anything. Nakupa mfano binafsi ili uelewe. Huenda haya yakawa msaada kwako.


Mi najiandaa! So don’t be confused with my lifestyle. 

Huwezi kuwa mjasiriamali na kiongozi wa kimataifa wakati  toka amekuja ROBIN SHARMA na kuondoka hata hujui, kina AZIM JAMAL na BRIAN TRACY wamekuja na kuondoka hata hujui. JOHN MAXWELL hujui hata ni nani? MYLES MUNROE alikuja na kuondoka ukaja kumjua siku kafariki! Unainbox watu: hivi huyo “munorowe” ndo nani? Seriously? Au usikute hata humjui. Watu wangapi walitaka kuwa unachokitaka wewe na wakakipata? Walifanya maandalizi gani na kwa muda gani? Usifikiri ni suala la kuombewa tu na kutabiriwa na kuwekewa mikono.


Preparation my friend. Kama unataka kufika mbali anza maandalizi ya kwenda mbali! Safari ya kwenda Mlimani City hupangi mwezi mzima. Lakini safari ya kwenda kijijini mtu huipanga miezi hata miwili kabla! Okay safari ya kwenda kazini kwako unaipanga muda gani? Si unaamka tu unaenda? Sasa unadhani na umilionea ndo hivyo? Ukitaka kupanda mlima Kilimanjaro unaamka tu unaenda? 

See?


Mungu hawezi kukupa mafanikio ambayo huna maandalizi nayo. Yatakuangamiza bure. Mungu anajua. Prepare yourself! Kuna mpaka kuiandaa mindset yako kuwa kama ya watu wanaoishi hicho unachotaka. Mawazo yako yanakua au yanadumaa? Unaambatana na watu gani? (Hili nitaliongelea kesho kwa Neema ya Mungu)


Usikae tu na FALSE HOPES eti one day yes! Acha hizo habari unataka kuwa superstar kama LIONEL MESSI amka alfajiri kafanye mazoezi, acha sigara na bangi acha uhuni nk. Otherwise mwisho wako ni Mtibwa Sugar au Mji Mpwapwa. Michael Jordan alikuwa anarusha mipira (shots) 1000 everyday. Ndo anaridhika. Kwa wanaojua basketball wanaelewa mikono inakuwaje ukirusha shots 1000 tena from the 3 points line! Legend!

You want to be a LEGEND? 

Prepare!


If you QUIT, you were never meant to be a LEGEND!

Utakapofika mwisho wa maisha yako utakuwa umeishi ndoto yako? That depends on your preparations. Mimi namwamini Mungu mno kuhusu hilo. Na najiandaa sana sana sana. Coz I’m going very far!

YOU ONLY GET IN THIS LIFE WHAT YOU PREPARE FOR

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya

Dar es Salaam, Tanzania

East Africa.

WhatsApp        #o788366511

SMS and Calls #o752366511

Blog                  www.andreamuhozya.blogspot.com


UBARIKIWE.

コメント


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page