top of page

TENDO LA NDOA NI TAKATIFU ( SEX IS HOLY IN MARRIAGE)

Updated: Sep 5, 2022

Ni kwa wanandoa tu, kama bado subiri ndugu mpaka wakati wako.


“ Tendo la ndoa ni takatifu” angalia hapo vizuri, “tendo la ndoa” maana yake ni kwa wana-ndoa tu, ni takatifu na limeruhusiwa. Je wewe ni mwana ndoa? Au je unajiandaa kuingia kwenye ndoa? Mimi sijui hilo, lakini tambua ya kwamba leo nazungumzia mambo ya ndani ya ndoa. Lengo mama la fundisho hili la leo ni kukuleta badiliko la imani uliyo nayo kwenye eneo hili la mapenzi / sex kwa sababu ninajua kanisa la leo limekuwa kimya kuzungumzia jambo hili likiwa na mtazamo mbaya.

Mtazamo mbaya wa kanisa la leo kuhusu tendo la ndoa / sex


  1. Ni dhambi,

  2. Ni la watu wa mataifa,

  3. Ni jambo la aibu,

  4. Ni jambo la siri sana, lisifundishwe kanisani

  5. Tendo hili linaondoa upako kwa mwanadoa ambaye ni mtumishi. N. K


Huo ni mtazamo wa kanisa, lakini ebu cheki na mtazamo wa dunia jinsi unavyoliangalia jambo hili la ngono /sex. Dunia inafundisha hivi ; “ huwezi kuishi bila kufanya, unapaswa kufanya, ili uwe sawa, tendo linaongeza akili kwa mtu, tendo linaondoa makunyanzi usoni, tendo linamtengeneza mwanamke akae kwenye maumbile ya mvuto, tendo linaondoa mawazo, tendo ni kwa ajili kutengeneza pesa, tendo ni kwa ajili ya kuleta furaha hivyo ukiwa huna mpenzi huwezi kuwa na furaha. N. K”


Hayo ndio mafundisho ambayo dunia inafundisha. Ebu angalia hatari inayokuja wakati kanisa limekaa kimya kuogopa kulizungumzia lakini dunia ndio mwalimu, sasa fikiria mwenyewe watu watalazimika kwenda kujifunza kwa mwalimu dunia kwa sababu kanisa halina usemi. Ebu fikiria tena, matokeo yake pale ambapo watu wa kanisa wametoka nje kujifunza tendo na hao miongi mwao ni wanandoa. Na hilo ndilo tulionalo leo, wanandoa wakikosa maarifa ya kiungu kwa habari ya tendo la ndoa wakijikuta wanapata maarifa ya dunia ambayo hupelekea mpasuko katika ndoa.


Sijajua wewe unamtazamo gani katika eneo hili!!!

Kumbuka ; leo, sikufundishi ndoa ni nini bali nakufundisha tendo lenyewe la ndoa. “Kwamba ni takatifu ” Najua kwako inawezekana ikawa ngumu kuelewa hivyo kwa sababu ikiwa umeookoka unafikiri tendo la ndoa ni baya, au ni jambo la mwilini hivi na ndio mtazamo mbaya uliopo kwa watu wengi. Yaani Mungu akusaidie na atusaidie ikiwa tunatazama hivyo, unajua sasa imefika wakati hata watumishi wa Mungu wanashindwa kutoka / kwenda out pamoja mume na mke.


Wakidhani hata kutoka na mke / mume nayo ni jambo la kidunia sio kiroho. Kha!!! Sasa wewe unafikiri jambo la kiroho ni kuomba tu! Ingelikuwa hivyo Mungu asingeweka ndoa, angeweka kuomba tu alufu uone ingekuwaje!!!!

Tendo la ndoa limewekwa na Mungu kwa wanandoa tu na si vinginevyo na ndio maana Mungu amekuumba ukiwa na sehemu za siri kwa jinsi yako. Lengo kubwa la kukupa sehemu za siri ni kufaidiana na mwanandoa mwenzako kama sehemu ya kukumbuka agano lake la ndoa. Muungano wa kimapenzi kati yako na mwenzako wa ndoa ni mkamilifu, ni jambo jema machoni pa Mungu.


Wakati wa kufunga ndoa madhabahuni, kuna maneno unayoelekezwa ukiri lakini yatoke moyoni bila shuruti / kulazimishwa, lakini maneno hayo tunayathibitisha kuwa agano katika tendo lake, ambalo ni tendo la ndoa / mapenzi na mwenzako wa ndoa

Hivyo, maneno yako uliyokiri madhabahuni pamoja na tendo / penzi / sex hutupeleka kwenye agano la ndoa. Lakini haina maana ndoa ni tendo la ndoa tu! Hapana,


ndoa sio tendo la ndoa kwa sababu unaweza ukawa na ndoa lakini tendo la ndoa lisiwepo na bado ndoa ikabaki kuwa ndoa. Utajiuliza kivipi kukawa na ndoa alafu tendo la ndoa likakosekana, inawezekana kweli! Ndio inawezekana sana tu, kwani wanandoa wote wanapata tendo la ndoa? Jiulize hilo, utagundua sio wote wapatao tendo la ndoa. Kwani hujawahi kuona mmoja katika ndoa ni mgonjwa na hawezi kushiriki tendo la ndoa? Sasa ikiwa hivyo je utasema hiyo sio ndoa kwa sababu hakuna tendo? Hapana huwezi kusema hivyo,


Hivyo ni vyema ubadili mtazamo huo. Inawezekana pakakosekana tendo kwa sababu kama hizo za kiugonjwa lakini bado ndoa itabaki kuwa ndoa. Ingawa mazingira haya si mara nyingi, lakini yapo. Jifunze hapo, ili usije ukafikiri tendo ndio kola kitu, kwa sababu ukifikiri hivyo utakuwa ukimbaka mkeo, au mtakuwa mkibakana. Maana ukikosa kujua ndoa ni zaidi ya tendo, basi ukweli utamkera mwenzako, maana kila ukirudi, unahitaji, ukimuangalia unamuhitaji sasa na yeye ni mwanadamu anachoka,


akikuambia amechoka basi ugomvi! Kwa sababu wewe hujui chochote zaidi ya tendo tu basi. Badili mtazamo ndoa sio tendo tu, ni zaidi ya tendo. Ingawa tendo ni takatifu likifanywa kwa mtazamo huu ninaokufundisha leo.

Kumbuka ; penzi / tendo ni muhuri kati ya mume na mkewe, ni kiashiria kinachoonesha kuwa watu hao waweli sasa ni mmoja ( the sign that they are one). Kila unapokutana na mwenzako katika tendo, ni ishara ya kukumbusha kile kiapo walichoapa madhabahu yaani agano. Tendo ndani ya ndoa ni huduma ya kukumbushia agano lenu mbele za Mungu ( Sex within marriage becomes a covenant renewal service).


Je unafahamu nini kuhusu meza ya Bwana, kila tunapotumia? Tunapotumia meza ya Bwana tunafanya kwa ukumbusho wa Bwana ( Luka 22:19). Na katika tendo la ndoa, wanandoa wanapokutana hukumbusha agano la Mungu katika ndoa lakini pia tendo huwaleta pamoja wanandoa, tendo pia ni ishara ya kumtangazia mwenzako kwamba wewe ni wa kwangu tu na mimi ni wako tu, hakuna mwingine, tendo la ndoa hutoa heshima kwa mwenzako n. K


lakini chonde chonde usije ukajaribu kama wewe si mwanandoa, ni dhambi. Unanisikia? Ikiwa bado huna ndoa, mpendwa tulizana kabisaa! Subira wakati wako!!!

Je tendo la ndoa limewekwa kwa madhumuni gani, kwa kuzaliana tu?


  1. Kwa kuzaliana.

  2. Kwa furaha / kufurahiana kwa wanandoa kama sehemu ya utakatifu/ kwa maana ni la ki Mungu jambo hilo.

  3. Kwa kuleta ukaribu / mume na mke kuwa mmoja ( become oneness)

  4. Je kama ni jambo takatifu kwa nini watu ambao ni wanadoa wengi wanazimaga taa? Na pili je kama ni takatifu ni ruksa kwa mwanandoa anaweza kuanza kwa maombi kabla ya tendo?


Hahahahaaa… 😀😀😀💖💖 nilikuambia leo ni mambo ya ndani, shauri yako.

Maswali hayo ni maswali ya kuchekesha lakini ni maswali makini sana. Nakumbuka, nilikuwa na rafiki yangu zamani zamani, aliniambia yeye akikutana na mke wake lazima azime taa na hawawezi kukutana mchana, wao ni usiku kwa usiku. Sasa nilimuuliza “ kwa nini, mnazima taa? Na kwa nini hamwezi za mchana mchana hivi? ” akanijubu kwamba yeye anasikia aibu sana!!! Dah!!!! Eti macho yake yanaona aibu, hahahaha…


Kwa kuwa alikuwa rafiki yangu nikamtania avae miwani myeusi 😎😎😎… Unajua huyu, jamaa alikuwa haelewi kabisa mambo haya bhana! Alikuwa mlokole fulani hivi, mshamba!! Anyway

Majibu ;


01. Hakuna haja ya kuzima taa, ikiwa tendo takatifu.


Aibu inatoka wapi kwa mumeo au mkeo? Kwani ni nini wewe usichokijua kwa mwanzako? Lakini kama umejiwekea kautaratibu kenu, sawa sio vibaya. Mchana pia muda mzuri, hakuna shida.


02. Mnaweza mkamshukuru Mungu kwa uumbaji wake kabla hamjaaza mambozii, sio dhambi kabisa!


Kuna ndugu ambao kwa kweli wanamuhitaji Mungu, lakini hata mimi na wewe tunamwitaji Mungu. Hawa ni wale ambao dk mbili tu, wapo hoi wamekwisha choka! Sasa huoni ni vyema uanze na maombi Mungu akusaidie uweze kumfikisha mwenzako!!! Ni vyema ikibidi uombe, upate nguvu zaidi ndugu, unanielewa? Lakini sio vibaya kuomba wala sio sheria kwamba uombe, pale unapoona vyema,lakini inapendeza kuomba kabla ya tendo, ukiweza fanya hivyo.


Ngoja niishie hapa bhana, najua umepata kitu fulani leo hii. Usisite kunipigia kwa jambo lolote ulilojifunza leo.


Namba zangu ni +255 683 877 900

What’s app ni +255 746 446 446


@ Mch. Gasper Madumla.

Ubarikiwe.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page