top of page

SIKUKUU YA PASAKA NDANI YA RUNGWE (MBEYA),KATIKA TAMASHA LA INJILI


DSCN0985

Mch. Gasper Madumla akihubiri ndani ya Masukulu


Bwana Yesu asifiwe…

Mwacheni Mungu aitwe Mungu jamani. Mungu hakika anaishi yu hai halisi kabisa.

Haya ninayokujuza sasa ni machache kati ya mengi aliyotenda Bwana Mungu katika mkutano wa injili huko Rungwe~Mbeya. Awali ya yote nimshukuru yeye Bwana wa mabwana,sababu alitusafilisha toka Dar mpaka Rungwe,tukiwa salama kabisa.

Watu wa Rungwe waliheshimishwa mno kwa kutembelewa na watumishi wa Mungu,ambao walifanyika baraka kubwa kwa wakazi wote wa maeneo mengi huko Rungwe. Unajua injili inapohubiriwa ni Yesu mwenyewe anahubiriwa,hivyo siku hizo 6 za mkutano wa injili zilikuwa ni siku za matendo makuu ya Bwana.

Tulienda kula sikukuu ya Pasaka na wakazi wa Rungwe,kwa kweli inapendeza kula sikukuu nyumbani,hivyo tukafanya na tamasha kubwa la injili katika miji ya Rungwe sehemu za Masukulu,Ushirika katika shule ya msingi,viwanja vya CCM KKK,na katika kiwanja cha Itokela pamoja na sehemu iitwayo Ikuti.N.K ( Kuanzia tar.03,04,05,06,07na 08 April 2015)

Ndiposa nikalikumbuka neno la Bwana katika kitabu cha injili ya Marko 16:20,Neno linasema;

“Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.] “

Mitume walipotoka ndipo Bwana akatenda kazi pamoja nao,Biblia inasema kwamba mitume walihubiri kote kote hii ikiwa na maana kuwa hawakuchagua maeneo ya kuhubiri bali Roho ndie aliyewachagulia maeneo na kuwapeleka.

Mitume,walipohubiri tunaona ishara kuu na matendo ya ajabu yakifuatana nayo kama ilivyokuwa katika mkutano huu wa injili maana Bwana alitenda kazi pamoja nasi. Bwana aliwaponya wote wenye kuelemewa na nguvu za giza.

Tazama,


IMG-20150411-WA0009

Mtumishi Gasper Madumla akihudumu.


Palikuwepo na kijana mmoja aliyekuwa akianguka mara kwa mara kwa kifafa. Wazazi wake wakampeleka kwa waganga na wakaambiwa kwamba mtoto wao kachezewa kwa madawa na mtu ndugu yao,waganga hawakuweza kumponya kabisa! Hali ya kijana ikawa mbaya zaidi.

Hali ile ilimkosesha raha yule kijana,lakini ashukuliwe Mungu wa miungu maana alimponya kijana katika mkutano huu. Akalejeshewa furaha iliyokuwa imepotea miaka mingi, hakika Mungu anaishi.

Mama mmoja pia aliponywa na Yesu Kristo. Mama huyu alikuwa amekematwa na nguvu za giza kweli kweli,akawa anakula chakula kingi sanaa ( chakula kama cha familia,yeye hula mwenyewe ),mapepo yalikuwa yanamtesa mno,Lakini watumishi walipoingia hapo wakafanya maombi kwa jina la Yesu Kristo,na hatimaye akafunguliwa.

Jambo moja nililojifunza katika mkutano huu wa injili ni hili;

▪ UNYENYEKEVU NI NGAZI YA MAFANIKIO.

~Najua kwamba kila mtu hupenda kufanikiwa kitika nyaja tofauti tofauti. Lakini mimi nakuambia ukitaka upande kimafanikio ya kiroho hata kimwili basi uwe mnyenyekevu. Ukitaka Mungu akuinue katika huduma yako,basi huna budi kujishusha mbele yake. Matendo makuu ya Mungu Baba yanapatikana katika unyenyekevu. Mara nyingi tunajizuilia ishara za Mungu katika mikutano ya injili kwa sababu tumekosa unyenyekevu.

Naliliona jambo hili,nikajishusha mimi pamoja na wenzangu,kisha tukamuona Mungu akifanya Yeye mwenyewe.

Haleluya…


DSCN0961

Mtumishi wa Mungu Mh.Richard Kasesela akiimba na Edson Mwasabwite ” ni kwa neema tu..”



IMG-20150411-WA0007

Mch. Adam Mwakipiki na mwinjilisti Musa Gwau wakihudumu katika eneo la Ikuti huku mvua ikinyesha



IMG-20150411-WA0017-1

Watu wakimchezea Mungu wao,katika viwanja vya KKK CCM.



kuhani

Waimbaji wakimtukuza Mungu katika nyimbo ya sifa ikiongozwa na Filemoni Kuhani.


Waimbaji mbali mbali walikuwepo kumtukuza Mungu aliye hai.Ilikuwa ni furaha sana maana mbali na uimbaji tuliweza kupokea mahubiri mazuri kutoka kwa Mch. Gasper Madumla,Mch.Adam Mwakipiki,mwinjilisti Musa Gwau & mwinjilisti Ibra. Ndipo lile neno likatimia la umoja katika kazi ya Bwana maana tuliagizwa tuwe wamoja.

Hivi unajua katika umoja pana nguvu sana,ndio maana Yesu alisisitiza sana tuwe na umoja  hata Petro alipokutana na yule kiwete aliyewekwa katika mlango wa mzuri.Petro akamwambia yule kiwete ” tutizame sisi ” (Matendo 3:4) Lile neno ” sisi ” linawakilisha umoja katika kazi ya Bwana,Petro alitambua hilo.


ITOKELA

Tamasha hili lilikuwa na vijimambo,hapa ni msanii na mwimbaji wa nyimbo za injili akifanya vitu vyake katika viwanja vya Itokela-Rungwe



port port

Wasiomjua port port ndio huyo hapo wa kati kati akicheza ” kipiki piki”



masukulu-2

Watu wakifuatilia mahubiri-Masukulu.



DSCN0988

Mtumishi Gasper Madumla akihubiri.



IMG-20150411-WA0011

Kipenzi cha watu wa Rungwe yaani ni mwimbaji mwenye kuzikonga mioyo ya watu wengi Rungwe,anaitwa Simon Mwamweja



DSCN0922

Mwinjilisti wa kimataifa ,Ibra akihudumu



DSCN0940

Mratibu wa tamasha ndugu Elias Kalinga (wa kulia mwenye suti nyeusi) pamoja mh.port port wa kati kati,na Mch.Gasper Mdumla wa kushoto.



IMG-20150419-WA0006

Mratibu MC.Mtumishi Ibra,akienda sawa kumalizia tamasha zima.


UBARIKIWE.

コメント


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page