SHETANI NA MAPEPO.
- Nov 22, 2018
- 3 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Je ni vyema kujifunza somo kuhusu shetani na mapepo yake? Je ukijifunza kuhusu shetani na mapepo utafaidika nini? Je ni kweli unahitaji kujua au kupata maarifa kuhusu shetani? Utapata matokeo gani ukijifunza kuhusu ufahamu wa namna ? N.K Unaweza ukajiuliza hivyo. Lakini watu wengi hawaoni sababu ya kujifunza maarifa ya namna hii.
Kama mtumishi wa Mungu unapaswa kuyajua haya,ili yakusaidie. Kuna mambo mengi sana ya kujua ili uongezeke kiroho. Na itakusaidia utakapojua siri iliyopo katika mapepo ili kusudi usije ukatishwa au ukatumikishwa hali wewe umekwisha okoka! Mapepo si sehemu yako katika jina la Yesu. Sema amen.
Mambo muhimu kujua.
01. shetani alikuwa malaika,aliumbwa pia.
Moja kati ya malaika walioumbwa, alikuwa ni Lusifa,yeye alikuwa ni mkubwa wa malaika wengine akiongoza sifa kwa Mungu. Aliitwa nyota ya asubuhi / morning star ( Isaya 14:12). Hivyo utagundua ya kwamba hakuumbwa ili awe shetani, hakuumbwa ili aasi,wala hakuumbwa ili awe mwuaji,mwizi au baba wa uongo. Bali amekuwa hivyo kwa sababu alipenda “kiburi” akataka apokee sifa za Mungu,hapo ndipo alipoharibu. Na hapo ndipo shida ilipoanza!!! Kiburi ndio shida!
Ndio maana ugopa mtu mwenye kiburi, maana kiburi ni chukizo kwa Mungu. Kwa sababu hiyo ya kiburi shetani na baadhi ya malaika walioasi ( mapepo) walifukuzwa kutoka kwenye uwepo wa Mungu. ( Because of pride, satan and other Angeles, rebelled against God and they were sent away from God’s presence) – 2 Petro 2:4,Yuda 1:6. Bila shaka shetani amechukua robo / moja ya tatu ya malaika pamoja naye ( Ufunuo 12:4)
02. shetani hana sehemu ikiwa umeokoka.
Wengi hawafahamu kile kinachofanyika hakika kwa mtu aliyeokoka. Lakini endapo kama utatambua wewe ni nani,wewe uliyeokoka basi shetani hatakuweza hata mara moja. Maneno haya sio polojo tu,bali kuna namna ya ajabu kwa yule aliyeokoka. Ebu leo tafakari neno hili;
“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.“ Marko 16:17-18
Wale wanaozungumziwa hapa sio wachungaji,au mitume bali yeyote atakaye weka imani yake kwa Kristo,mtu huyo atatoa pepo. Hivyo utagundua kwamba ikiwa mtu atatoa pepo basi iko nguvu ya ziada yenye kutoa pepo. Huyo si mwingine bali ni Yesu ndani yake,Yeye Yesu yu hai. Hivyo ni vyema kutambua ya kwamba shetani,mapepo,majini na roho zozote hazina nguvu ya kumshinda mtu aliyekaa vizuri ndani ya Yesu.
03. Mapepo wapo wengi na wamekosa mwili.
Ukweli ni kwamba mapepo wapo wakutosha tu kwa maana ni roho zilizoasi. Tunaweza kuliona hili pale tunapoangalia yule mtu aliyepagawa na mapepo kule kwenye ng’ambo ya Wagerasi. Yesu alipomwuuliza yule aliyepagawa kwamba jina lake nani? Naye akajibu ni “Legioni” ( Marko 5:9) . Maana yake ni “jeshi” hivyo mapepo yalikuwa ni kama jeshi. Wengi tu. Na hii ndio hali iliyokuwepo hata sasa. Lakini ukweli ni kwamba hizi ni roho,zimenyimwa miili. Kwa sababu hiyo,mapepo huingia ndani ya mtu kwa lengo la kumsumbua hata kumwangusha hata kufa.
Kuna watu ambao kwa kweli wanasumbuliwa kweli kweli na mapepo, mavibwengo n.k Na bahati mbaya wengine wanapoteswa na kusumbuliwa hukimbilia kwa waganga pasipo kujua ya kwamba hakuna mganga anayetoa pepo hata mmoja. Habari njema ni kwamba Yesu yupo hai,kwa jina lake hakuna pepo hata mmoja atakayesalia ndani ya mtu. Hivyo ukiona unateswa na roho mbaya za namna hii,basi kimbilia kwa Yesu,mtafute mchungaji,naye atakuonesha njia sahihi ya kuwatandika hayo mapepo
04. Hakuna mapepo mazuri,ili mladi ni pepo ni baya tu siku zote.
Hujawahi kusikia watu wakisema “ kuna mapepo ya heri na kuna ya shari” hao wote wasemao hivyo hawajui wanachokiongea kwa kweli. Siku zote roho chafu (impure spirit),ni mbaya tu. Kwa maana mapepo yote ni roho chafu ni mabaya siku zote.
ITAENDELEA…
Natamani leo tuwasiliane pamoja na maombi. Lakini ikiwa umebarikiwa na fundisho hili nifahamishe pia. Kwa maombezi pia nipigie kwa namba hizi hizi + 255 683 877 900
WhatsApp ni .+255 746 446 446
UBARIKIWE.
Comments