top of page

SAFARI YA KIBIASHARA.

Updated: Sep 5, 2022


Na Mwl.Andrea G.Muhozya


  1.  SAFARI YAKO YA KIBIASHARA HAITAKUWA SAWA NA YA MTU MWINGINE YEYOTE

Katika kufanya kwangu biashara na ujasiriamali nimekuja kutambua kuwa safari yangu kibiashara imekuwa tofauti sana na watu niliokuwa nikiwatazama kama mfano mbele yangu.

Mwanzoni hilo lilinifrustrate kiasi na kujiona kuwa huenda mimi nakosea sana vitu. Lakini baada ya miaka zaidi ya nane ya kudumu katika biashara na ujasiriamali nimetambua kuwa uzoefu wangu katika safari ya biashara hauwezi kuwa sawa na walionitangulia. In fact haupaswi kuwa sawa.


Unaweza kufanana kidogo (being similar) lakini siyo kuwa sawa sawa (cannot be the same)

Hivyo unapoanza safari yako kibiashara tambua hilo pia kuwa alikopita Bakhresa wewe hutopita vile vile. Alikopita Shigongo na Dewji na mwingine yeyote unayemjua haitakuwa vile vile.


Maana mazingira tunatofautiana mno.Wewe na yeye mnatofautiana vitu vingi hata kama utaanza kwa umri ule ule alioanza yeye. Maisha ya wakati ule alipoanza kupita njia hiyo aliyopo sasa ni tofauti mno na maisha ya sasa. Nk.


Hata kama mmeanza pamoja huenda hata mlivyopata mitaji ni tofauti. Mwingine alipewa mwingine alikopa mwingine aliuza vitu mwingine alikusanya kupitia mishahara mwingine alifanya madili hatari ofisini nusura akamatwe mwingine hakuanza na pesa alianza na idea tu pesa ikamfata. Hamtafanana kabisa niamini mimi. So acha kutamani kuwa kama yeyote.

Cha kuzingatia tu ni kujifahamu wewe mwenyewe kwa undani.


  • Wewe ni aina gani ya mtu?

Unaongozwa na FILOSOFIA GANI katika kutafuta mafanikio? Mfano kuna watu philosophy inayoaaongoza ni kuwa lazima ujuane ba mtu serikalini ili mambo yako yaende sawa. So huyo Rushwa kwake ameweka budget kabisaa hata asipoombwa yeye ndo ataomba atoe. Mwingine personal philosophy inayomwongoza ni kuwa kazi kazi. Yani ni kupiga mzigo 24/7. Hilo tu. Mwingine anaamini ili atoke anahitaji kuwa mtu wa maombi na siyo kutegemea kupiga mzigo tu. Huyu anaweza kuwa kanisani mara 4 kwa wiki na mkesha juu kuombea biashara lakini hawezi kukesha kazini hata siku moja ili akamilishe majukumu. Hizi ni philosophies. Wewe yako ni ipi?


Maana usije ukajifananisha na mwenye LAKE OIL au ASAS kumbe philosophy zenu za mafanikio ziko tofauti. Kuna watu wanaamini mafanikio anatakiwa yaonekane mapema ndani ya miaka mitatu hivi..wengine wanaamini mafanikio ya kweli miaka 30 ijayo. Sasa unadhani mtakuwa na safari sawa? Wewe unataka kuwa milionea ndani ya miaka 7 mwingine anataka awe ndani ya miaka 17. What’s your approach to success kibiashara?


Jijue. Jichunguze.

Una uelewa upi kuhusu biashara? Una ujuzi wowote kuhusu mauzo? Una ujuzi kuhusu matangazo (marketing and publicity)? Au ndo utataka kulazimisha rafiki zako na ndugu ndo wakupe sapoti wasipokupa unakuja mitandaoni kulalamika eti watu weusi hatupendani?😂.


Una ujuzi wowote wa uongozi? Unaweza kuongoza wale utakaowaajiri kwenye biashara yako?Una maono gani? Vision. Biblia yasema pasipo maono watu huangamia. Una vision? Ipi?

Una mipango gani? Mikakati gani? Tabia zipi? Character ipi?

Fikra zipi? Personality (temperament) ipi? Wewe ni mtu wa watu… unaweza kuthamini mtu yeyote? au wewe rafiki zako na ndugu zako ndo unawathamini kuliko stranger? Hivi vitu vinasababisha uwe na safari tofauti mno kibiashara.

Jitambue. Jichunguze.

Unatokea familia inayoamini nini kuhusu pesa: kwamba pesa ni chanzo cha uovu au pesa ni msaada kwa jamii?

Una nidhamu ya pesa? Ukikopa hata tigo au voda huwa unaridisha on time au hadi wakutishie kuwa watakunyima huduma zao?My point is huwezi kufanana na mtu katika mambo hayo yote. Hivyo safari yako kibiashara itakuwa tofauti tu. Kuna vitu kwa wengine itakuwa rahisi kwako itakuwa ngumu. Tafuta maarifa. Pamoja na kumwomba Mungu kweli kweli kwa bidii lakini usisahau nafasi ya kujifunza na kufanya kazi kwa bidii.


Biashara inahitaji uwe na maarifa na ujuzi wa mambo mengi. Binafsi kwa kuona jinsi watu wengi wanavyohangaika ba kuishia kukata tamaa katika biashara… nimekuwa nikitoa mafunzo kwa wenye nia ya kujifunza. Huenda ukawa mmoja wao.Usijipe moyo tu huku huna maarifa. Itakusaidia sana!


AGM

Ikiwa umebarikiwa,tufahamishe ili tumtukuze Mungu pamoja,Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa;


Semper Fidelis,

Andrea G. Muhozya Entrepreneur & Business Trainer Dar es Salaam, Tanzania

East Africa +255 788 366 511.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page