MTU USIYEMJUA MWENYE KUTEMBEA NA WASAA WA HATMA YAKO – 02.
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 15, 2020
- 5 min read
Updated: Sep 29, 2022

Na Mwl.Andrea G.Muhozya
….So ninavuta pumzi ndefu na kuishusha. Ninakuwa nimerelax zaidi. Akasema:
“Mimi naitwa kaka Aaron”
“Ninafanya kazi hapa. Hapo kwenye hilo duka. Nimekuwa nikikuona kwa siku nyingi ukija hapa unalala hapa kwenye kibenchi baadaye unaondoka. Kwa hiyo leo nimeona nije ili nikuulize mdogo wangu. Sasa umesema unakaa Nyakato kote huko mjini huwa unakuja kufanya nini na mbona huwa unalala tu sasa.”Anaongea kwa upole sana. Kwa kuwa nimeshakuwa na instinct kali ya kumwamini ghafla, ninaamua kumwambia ukweli kuwa huwa nakuja mjini kutafuta vibarua nikichoka ndo nakuja kupumzika sababu hakuna kelele hapo siku ambazo hakuna treni.
Baada ya mazungumzo mafupi ananambia:
“Sasa kuanzia kesho uwe unakuja hapa dukani umesikia? Utakuwa unatusaidia kufanya usafi na kufagia nje… nitakuwa nakupa angalau nauli na hela ya kula. Umesikia dogo?”
Mimi kimya. Namwangalia bado. Sijui cha kujibu. Ghafla anaita:
“Sporahhhhh!” “Abeee” anayeitwa anaitika “Niletee soda moja… dogo unakunywa soda gani?”
“Fanta”, ninamjibu. “Leta Fanta ya baridi Sporah! Si ya baridi dogo eti?”
“Ndiyo”. Ninamjibu machozi yakinilengalenga.
Soda inaletwa. Ninakunywa. Ananiacha peke yangu anarejea dukani kwake. Kulikuwa na duka halafu ofisi nyuma ya duka. Ananiambia nikimaliza nimpelekee dada chupa dukani. Namshukuru. Namaliza kunywa napeleka chupa. Yuko nje ya ofisi. Nashukuru tena sana. Kwa kweli soda imenipa nguvu ya breakfast na lunch hapo hapo. Namuaga!
“Shika hii hapa nauli. Nenda nyumbani kesho usichelewe saa mbili uwe umefika”
“Asante sana kaka Aaron”
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Story short nikafika kesho yake. Nikaanza kibarua. Kwangu si zali la mentali tu. Bali kuna kitu cha tofauti kabisa moyoni. Ninaona future ileeee. Kumbuka yeye ni mwajiriwa tu kwenye duka la mtu ni msimamizi.
Nimefanya kazi za usafi. Baadaye nikawa naenda nao kuwasaidia kubeba vitu wakifanya manunuzi maduka ya jumla au depot. Baadaye nikawa nimebadilika nimekuwa kama mmoja wao. Baadaye mmiliki wa duka akavutiwa na bidii niliyoonyesha akawauliza wamenitoa wapi mbona ni mdogo sana. Wakampa story yangu. Akataka kuonana na mimi. Story short akaniambia ameamua kunisomesha A LEVEL maana amesikia nilifaulu vizuri Kidato cha Nne. Nilishangaa na kufurahi sana.
Akanipa ajira kwenye behewa la chakula kwenye treni. Buffet Car. Maana yeye alikuwa ana tenda ya kutoa huduma ya chakula na vinywaji kwenye treni (catering services). Akaniambia huko Nyakato unakokaa kawaage wambie unahamia Dar maana nina nyumba ya wafanyakazi Kinondoni utakuwa huko. Keshokutwa unaanza kusafiri kwenda Dar es Salaam. Utakuwa unaishi huko Mwanza utakuwa unafika na kugeuza tu.
Ninaenda kuwapa hizo habari “masela” na yule rafiki yangu.
Wanashangaa!
Wengine wananiambia niwe makini duniani mambo mengi.
Nyumbani pia Ukerewe wanashangaa.
Ajabu kipindi hicho hicho nikapata watu mwili walikuwa tayari kunisomesha. Mmoja anataka niende LAKE SEKONDARI hapo Mwanza mwingine anataka niende TABORA BOYS. Unaweza kuchanganyikiwa na kusema nilichotaka si ndo hiki. Lakini nguvu ya ile encounter kwenye kile kibenchi na kaka Aaron ilikuwa kubwa sana ndani yangu.
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Story short ni kuwa niliachana na kila kitu na kila mtu nikaanza maisha mapya. Kaka Aaron na dada Sporah wakabaki Mwanza pale dukani. (Nina mengi ya kuongea juu ya watu hawa wazuri. Leo siyasemi.) Nikaanza kazi kwenye treni. Nikaona mengi. Nikajifunza mengi. Oh God mengi kweli kweli. Mwaka uliofuata nikaanza kutafuta shule. Wakati ulipofika nikapata Makongo kwa Mzee Kipingu. Hapo ni mwaka wa tatu tangu nimalize kidato cha nne. Nikaanza High School. Mungu mwema nikafaulu. Nikaanza Chuo Kikuu. Nikamaliza. Nikaingia kwenye ajira na baadaye ujasiriamali mpaka hivi leo unaposoma makala hii.
IMPORTANT POINT:
Destiny yangu na mambo yoyote yaliyo mbele yangu vilikuwa SHAPED kwenye kile kibenchi na ile encounter na kaka nisiyemfahamu kabisa pale Railway Station Mwanza mjini miaka mingi sasa iliyopita.
Encounter hiyo na tukio lile moja lilikuwa na NGUVU kubwa ya kunipeleka Mungu alikokusidia niende. Such a powerful encounter indeed.
Sikia: Strangers have a greater chance to shape your future than your family. Watu usiowajua wamebeba nguvu ya kubadili maisha yako kuliko ndugu zako.
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
USIPOJUA MAJIRA YA KUIJILIWA KWAKO UTAPISHANA NA KUSUDI LA KUISHI KWAKO.
Tuachane na story yangu kidogo. Nikupeleke katika historia. Safiri nami mpaka karne ya 9 kabla ya kuzaliwa Yesu. Miaka ya 900 hadi 800 na kitu BC hivi. Tutakutana na Nabii mmoja anaitwa ELIYA. Bonge la nabii. Si mchezo. Ana nguvu siyo ya kawaida. Nabii nabii kweli. Si unajua ndiye aliyeomba hadi moto ukashuka ukalamba sadaka na maji na madhabahu na kila kitu. Huyo huyo. Nabii mwenye nguvu.
Lakini muda wake ulikuwa umekaribia ukingoni. What to do.
Mungu anampa jukumu la kumwandaa mrithi wake. So Eliya anapita zake hadi alipo Elisha. Wapi?
Shambani.
Imagine. Elisha analima zake kwa kutumia ng’ombe wale wa kilimo. Na wafanyakazi wengine. Baba yake Elisha hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa mtu mwenye uwezo. Kumiliki jozi 12 za ng’ombe wa kulimia mwaka 900 kabla ya Yesu kuzaliwa si mchezo.
So Eliya anapita. Anamkuta Elisha akipiga kazi shambani. Eliya haongei kitu. Anajipitisha karibu ya Elisha. Anavua moja ya vazi alilojifunika na kumtupia Elisha!
Hebu fikiria kidogo zama za leo. Uko zako shambani bize na kazi then mtu usiyemjua kapita shambani kwenu. Uko na wengine shambani. Anapita karibu na ulipo wewe. Anavua tuseme kama vile vikoi vya kimasai watu wanajifunikaga shingoni labda. Anakutupia wewe. Halafu huyooo anaondoka!
Nini ungefanya?
Utamtukana. Utamwambia aache utoto? Utamstahi tu na kumwacha aende zake? Utakemea kwa Jina la Yesu ashindwe!
Elisha kitendo kile aliona si cha kawaida. Ndani mwake kuna kitu kilimwambia FOLLOW THIS MAN.
STOP EVERYTHING AND GO.
Kinaitwa INSTINCT.
Huyu stranger amemtupia tu vazi lakini kwa Elisha kitendo hicho kiliongea maneno zaidi ya elfu moja. Kwa sababu baada tu ya kutupiwa lile vazi Elisha aliacha kila kitu, acha ng’ombe na AKAMKIMBILIA ELIYA. (1Wafalme 19:19-20)
Kuna tofauti ya kujua destiny yako na kuikimbiza isikupite.
Eliya anamshangaa Elisha. Dogo vipi? Elisha anasema boss usishangae nipe “dakika sifuri” nakuja. (Natumia lugha ya ujana tuelewane). Elisha akarudi shambani.Kwa nini alirudi? Sababu aligundua kuna vitu siku za usoni vinaweza kumfanya arudi nyuma. So akamwambia Eliya: “WAIT A MOMENT” “NIPE DAKIKA SIFURI NAKUJA”
Kilichofuata kinatufundisha zaidi. Maana alirudi shambani akachinja wale ng’ombe aliokuwa analimia, akawapika tena kwa kutumia zile mbao wanazofungwa ili walime. Akawagawia watu ile nyama watu wakala. Halafu akamfuata Eliya. Tena akaanza kuwa mtumishi wa huyo STRANGER (kama HOUSE BOY wa Eliya yaani).
Can you imagine?
Hakuna cha kujieleza kwa ndugu. Hakuna cha kuconvince wazazi. Chinja ng’ombe. Vunja mbao pikia nyama. Gawa nyama watu wale. Tembea mbele.
Alichoma daraja kabisa. Unguza boti za kumrejesha. No turning back!
Elisha destroyed EVERY possibility of going back. Can you do that?
Huyo ndiye Elisha ambaye baadaye alikuwa na nguvu ya kurudisha shoka juu ya maji likaelea lilipotumbukia majini…Elisha aliyetabiria mifupa ya wafu ikawa hai watu wakafufuka kutoka kuwa mifupa hadi watu…
And everything in between! Nguvu yake ilikuwa imefichwa ndani ya ELIYA. So hakupaswa kumiss wasaa wa kumfuata Eliya na kuwa mentored naye. Na aliutambua ulipofika. Akautumia.Yes Elisha akawa Elisha.Elisha the Great. Greatness haiji hivi hivi my friend. You must have the INSTINCT to follow your destiny…
ITAENDELEA… !
Ikiwa umebarikiwa,tufahamishe tumtukuze Mungu pamoja,kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa;
Semper Fidelis,
Andrea G. Muhozya Entrepreneur & Business Trainer Dar es Salaam, Tanzania East Africa +255 788 366 511. Na +255 683 877 900 :::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Comentarios