ATHARI YA DHAMBI YA MMOJA KATIKA KUNDI.
- Mch. Gasper Madumla
- Jun 23, 2022
- 2 min read
Updated: Aug 29, 2022

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Kuna namna ambavyo mtu mmoja aliyetenda dhambi anavyoweza kuleta majanga au athari mbaya katika kundi hata kama wengine katika kundi ni watakatifu lakini kile kitendo cha mwenye dhambik akiwa katikati ya kundi basi uwe na uhakika ninyi wengine hamtabaki salama.
Ni kweli Mungu atamuhukumu mtenda dhambi tu ( Ezekiel 18:20).Lakini pamoja na hukumu yake binafsi ninyi wengine ni lazima mtaathirika Kwa namna moja ama nyingine. Ukisoma biblia tunakutana na kisa kimoja kinachoeleza athari zilizoletwa na mtu mmoja aliyetenda dhambi.
Ebu cheki mtu huyu“ Miriamu ” dada yake Musa ambaye huyo Miriamu pamoja na Haruni walimnenea vibaya Musa kwa kuoa mwanamke mkushi.
Kitendo cha Miriamu kuinena/kuisemea vibaya ndoa ya Musa nabii wa Bwana,kilihesabika ni dhambi na makosa sana kiasi cha Miriamu kupata ukoma kama moja ya kushikishwa adabu!!! Lakini Musa akamsihi Bwana amponye Miriamu,lakini uponyaji wake ulimlazimu kwanza kukaa karantini muda wa siku saba, Imeandikwa ;
“ Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena..” Hesabu 12:15 ( KJV)
Angalia hapo,tunaona dhambi ya Miriamu imeathiri kusanyiko lote,angalia athari hizi;
01. Watu hawakusafiri muda wa wiki nzima.
Ebu fikiria kusanyiko lote limelazimika kukwama eneo moja kwa muda wa wiki nzima kwa sababu tu ya mkosaji mmoja. Hii ni athari kubwa Saba ya “kusitishwa safari ” Kwa muda wa siku 7.
Pata picha kama upo kwenye kikundi kinachosafiri Lakini kwa bahati mbaya mmoja wenu akakorofisha kwa Mungu halafu Mungu akazuia safari nzima kwa kumzuia huyo mmoja wenu kwa maana hamwezi kusafiri na kumwacha mwenzenu kambini. Leo makundi mengi ya maombi yamekwama kwa sababu ya mtu mmoja aliyetupwa kambini.
02. Kuwapa kisogo adui zenu.
Kama mkiwa katika umoja wa kiagano na mmoja wenu akavunja agano Kwa namna yoyote ile,basi uwe na uhakika Kwa ukengeufu wa mtu mmoja kundi zima litafedheheshwa na adui zao hata kama wengine wapo sawa.
Soma habari ya “Akani ” yule aloyewakosesha Israeli kwa kupigwa na adui zao watu wa Ai baada ya Akani tu kupoteza ( soma Yoshua 7:1-26)
Fikiria kama mmepatana katika maombi ya kufunga kwa siku kadhaa,halafu mmoja wenu akajificha kwa siri huku akawa anakula lakini katika kundi akijifanya amefunga na hatimaye mpo katika maombi ya pamoja kana kwamba nyote mmefunga na mnatembea pamoja. Kwa kufanya hivyo,ujue mtaanguka kama ukuta uangukavyo wote kwa ghafla.
Mambo ya kikundi hutegemea sana uaminifu wa kila mmoja ili kusudi mfikie malengo. Lakini kumbuka,mapatano si lazima yawe katika kikundi isipokuwa yanaweza kufanyika kwako na mume au mkee.
Hivyo; epuka katika agano hilo na kutenda dhambi japo kwa siri kiasi kwamba ninyi wengine hamjui.
Ikiwa kama umebarikiwa nifahamishe;
Na Kwa msaada zaidi piga +255 683 877 900
What’s app number +255 746 446 446
Na Mch. Gasper Madumla.
UBARIKIWE
Commenti