top of page

ROHO YA PASHURI.

Mch.Madumla

Na Mch.G.Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Pashuri mwana wa Imeri alikuwa ni adui wa Yeremia tena alikuwa kuhani na msimamizi mkuu wa nyumba ya Bwana,lakini cha ajabu alikuwa ni adui wa mtu wa Mungu Yeremia. Uadui wake haukua wa kawaida bali ni roho mbaya iliyokuwa ikimsumbua kwa sababu haiwezekani mtu kuhani kuwa adui na mtumishi wa Mungu kwa maana nyote mnafanya kazi ya moja ya Mungu.

Kama afisa mkuu wa hekalu la Bwana,Pashuri alikuwa msimamizi wa askari waliokuwa na wajibu wa kusimamia shughuri zote za utulivu katika ukumbi wa hekalu ( Yeremia 29:26). Hivyo aliamuru Yeremia apigwe na kumtia katika mkatale; 

Basi Pashuri, mwana wa Imeri, kuhani, aliyekuwa msimamizi mkuu katika nyumba ya BWANA, alimsikia Yeremia alipokuwa akitabiri maneno hayo.2 Ndipo Pashuri akampiga Yeremia, nabii, akamtia katika mkatale, uliokuwa pale penye lango la juu la Benyamini, lililokuwa katika nyumba ya BWANA.” Yeremia 20:1-2 

Na hilo ndilo andiko letu la msingi tunapojifunza roho ya Pashuri. Na kupitia andiko hili,ndilo andiko la kipekee la kwanza kwa Yeremia kupigwa hadhalani. Lakini baadae tunamuona Yeremia mtu wa Mungu akipitia katika adha ya kupigwa ( Somo Yeremia 26:7-11,36:26,37:11-16 n.k)

Pashuri alikuwa ni kuhani mwenye kutoa nabii za uongo (Yeremia 20:6). Na kwa sababu hiyo alitabiriwa kuwa ataangamia yeye na rafiki zake , Nabii huyu ni sawa na kusema kulikuwa na roho ya uongo na huyo baba wa uongo (shetani) ndani yake. Kumbe ukiwa unatoa nabii za uongo na kujifanya unatoa za kweli,kuna siku chache zijazo utaangamia na huo unabii wako wa uongo.

Hivyo roho ya Pashuri ni moja ya roho mbaya sana inayowatafuna watu wengi leo. Tazama Pashuri alikuwa kuhani katika nyumba ya Bwana ingawa alikuwa kinyume na neno la Bwana. Na hii ndio roho inayotesa wengi leo.

roho ya Pashuri ni roho ya kupinga neno la Mungu la kweli kwa neno la uongo. Pashuri aliposikia unabii wa kweli kwa kinywa cha Yeremia,tazama alimpiga Yeremia ( kwa sababu zake binafsi kwa maana nuru na giza haviwezi kuchangamana). Leo tunaona baadhi ya watu wanaotumika makanisani wakipinga unabii wa kweli pale ambapo Bwana anapotumia kinywa cha mtumishi wake.

Ukiona mtumishi wa hekaluni akimpinga mtu wa Mungu mwenzake kwa namna yoyote ile,hususani akiupinga unabii wa kweli wa Mungu ujue ndani yake ana roho ya Pashuri na inawezekana huyo apingaye ni adui wa neno la Mungu.

Leo,wakristo hatukubaliani,bali vita imejaa makanisani maana utakuta mchungaji wa kanisa fulani akigombana na mchungaji wa kanisa fulani. Ukiona hivyo basi ujue kuna mmoja hapo hayupo sawa au wote waweza wakawa hawapo sawa wametawaliwa na roho ya Pashuri ambayo roho hii ni kukataa kweli ya Mungu.

Mimi kinachonishangaza kwa huyu Pashuri kitendo  cha kumpiga Yeremia,kwa maana ilikuwa hakuna sababu ya kupigwa kwa Yeremia kwa maana Yeremia hakutoa unabii wa kwake mwenyewe bali unabii ulikuwa wa Bwana. Laiti ningekuwa mimi ndio Yeremia labda ningelimuuliza huyu Pashuri,kwa nini unanipiga ? kwani mimi nimetunga haya maneno ? Je hayo ni maneno yangu au ni ya Bwana ?

Roho ya Pashuri ni roho kinzani kwa sababu yenyewe haina kweli ndani yake. Na ndivyo watu wenye roho hii wameikosa njia ya Bwana,na hawana kweli ndani yao bali watu hao utawaona wakikaa tayari kuleta ukinzani. Lakini uzuri ni kwamba Pashuri aliangamia na roho yake mbaya ya kishetani na ndivyo ilivyo kwako;wataangamia wale wote waipingao kweli ya Mungu ndani yako,wataangamia na roho zao.

Pashuri alitamani kusikia nabii ya kumpendeza yeye,yaani nabii ya kiuongo uongo ili afurahie lakini ilikuwa ni bahati mbaya kwake kwa maana alichokitarajia hakukipata badala yake akakutana na neno la Mungu halisi. Jambo moja kubwa tunalojifunza pia,ni kwamba hata kama kutakuwepo akina ma-Pashuri kwenye huduma yako/mahali ulipo wewe usinene unabii kwa kuwafurahisha wao bali linene neno la BWANA kama lilivyo,kama kuwachoma liwachome tu na hapo ndipo watakuinukia kwa maana umenena kweli ya Mungu; lakini usiogope Bwana atakulinda katika hayo yote kama alivyomlinda Yeremia mtumishi wake.

Mch.G.Madumla.

Kwa maombezi piga sasa +255 683 877 900

What’s app number ni +255 746 446 446

UBARIKIWE.

コメント


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page