ROHO YA KUCHELEWESHWA
- Mch. Gasper Madumla
- Sep 6, 2018
- 2 min read
Shalom…
Kwa ufupi sana.
Kuna wakati unajiuliza umekosea wapi?, kwa maana umekua mtu wa kukwama kwenye eneo moja hilo hilo,au wakati mwingine umekuwa ukikwama kwenye maeneo mengi,yaani kila unachokigusa hakiendi!!!. Sasa ni miaka imepita, hujatoka katika eneo hilo. Si kana kwamba humpendi Mungu,la hasha! Unampenda sana, Lakini pamoja na kujitoa kwako kwa Bwana/kutumika,ila bado mambo hayaendi kabisa!
Ukiona hivyo, basi lazima ustuke kwa maana hiyo sio hali ya kawaida,yawezekana kabisa kuna roho imekushikilia ( Kwa upande fulani Mungu naye aweza akawa anakupitisha eneo hilo kwa kusudi fulani,lakini kusudi lake ni jema siku zote) Siku zote ibilisi ndiye mwenye kuchelewesha maisha yako. Na hakika kabisa kuna roho ya namna hii ya kucheleweshwa.
roho ya kucheleweshwa ni nini hasa?
Tena waweza kujiuliza,kuchelewa wapi? na waweza kuendelea kujiuliza maswali mengi ya msingi. Tunaposema roho ya kucheleweshwa,tuna maana ya nguvu inayokukwamisha katika safari yako ya maisha. Safari yako ya maisha inaweza kukwamishwa au kucheleweshwa kwa sababu nyingi.
Baadhi ya sababu hizi hutokana na hila za ibilisi juu yako,ama Mungu mwenyewe akakukawilisha kwa kusudi fulani,au wewe mwenyewe ukajichelewesha kwa sababu tu ya ujinga na upumbavu wako mwenyewe!!! ( Hivyo inategemea umecheleweshwa na nini)
Lakini mi nataka kuzungumzia sababu moja tu kati ya sababu nyingi za kukuchelewesha,sababu inayotokana na wewe mwenyewe. Nayo si nyingine ni;
01. Marafiki wasiofaa
Marafiki wana sehemu kubwa sana ya kukuchelewesha ikiwa kama umeambatana na marafiki wasiofaa kwako. Na muambatano huo utengeneza kitu kinaitwa “roho” (hivyo mnajikuta mnakuwa mkitembea katika roho moja) – 1 Samweli 18:1
1Samweli 18:1 “...roho ya Yonathani ikaambatana na roho ya Daudi...” Bila shaka hata mwenendo ama tabia ya Yonathani ilifanana na tabia ya Daudi kwa sababu ya roho zao ziliambatana. Sasa fikiria kama Yonathani ni mtu mbaya,Je Daudi hata pata ubaya huo? Ukweli ni kwamba ni rahisi sana Daudi kupata ubaya.
Ikiwa roho yako ikiambatana na roho ya mwingine basi ujue mtafanana kila kitu hata kitabia mtafanana. Hivyo marafiki wabaya wanasababisha roho ya kucheleweshwa kwa kiasi kikubwa sana. Pamoja na sababu nyingine za kucheleweshwa katika safari yako,bado marafiki wabaya ni watu wakuwaepuka kama ukoma! Kumbuka;
Tunaposema “marafiki wasiofaa/marafiki wabaya”tunamaana ya watu waovu ambao msiofanana kitabia. Watu ambao mmetofautiana katika tabia njema. Hao ni watu wenye kuachilia roho ya kucheleweshwa!
Namna ya kutoka katika mumbatano nao
Kukata mawasiliano nao. Hio ndio njia moja muhimu ya kuepuka urafiki na watu wasiofaa. Kuomba ni muhimu sana,lakini baada ya kuomba sasa chukua hatua ya kukubali kuwapoteza kabisa,ili kusudi ufungue lango la marafiki wakufaao watakaoachilia roho ya wepesi ili usonge mbele!
Kwa maombezi na ushauri + 255 683 877 900
Na Mch. Gasper Madumla.
What’s app ni +255 746 446 446
UBARIKIWE.
Comentários