top of page

ROHO YA HEKIMA NA MAFUNUO – 02

Updated: Aug 30, 2022



Paulo mtume ni mmoja wa watu waliokuwa na “roho ya hekima na mafunuo” Biblia inamwelezea kuwa alikuwa ni mtu aliyekirimiwa mafunuo (2 Wakorintho 12:7). Uwezo huo aliokuwa nao ulimwezesha kuifanya kazi ya umisheni kwa wepesi katika mazingira magumu,kwa maana hakuwa yeye kama yeye bali kulikuwa na roho ya hekima na mafunuo iliyofanya kazi ndani yake.


Katika safari yake ya tatu ya umisheni alipofika Efeso na kuliona kanisa la Bwana likisonga mbele,aliwaombea wapokee roho ya hekima na mafunuo, “Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; ” Wafeso 1:17. Paulo anaona umuhimu wa mkristo kuwa na roho ya kusikia na kuona,ili aweze kusonga mbele kiufanisi zaidi.

Ni matamanio ya Bwana kwamba watu wake wavikwe uwezo wa kiroho wa kusikia na kuona ili wapambanapo washinde,kwa sababu moja ya kigezo kikubwa cha ushindi dhidi ya adui yako ni kumwona alivyo na kuweza kumsikia katika ulimwengu wa roho,(Kuona uwezo wake) ili ujue unampigaje. Unanielewa lakini? Kanisa la Bwana limepitia kwenye vipindi tofauti tofauti,katika vikwazo vingi,lakini hata hivyo bado linashinda zaidi ya kushinda.


Paulo alitamani kanisa la Efeso liwe macho wakati wote,na ndio hayo hayo matamanio ya Bwana kwako wewe ambaye ni kanisa la leo.

Ebu mtazame Paulo tena,alipoingia Filipi mji wa Makedonia (Filipi ulikuwa mji mkuu katika jimbo la Makedonia). Paulo na watendakazi wenzake walipokuwa hapo,walitafuta mahali pa kuomba,na walipopata,wakafunga hapo na ibada ikaanza.


Gafla kulikuwa na binti /kijakazi mmjoa mwenye pepo la utambuzi/pepo la uaguzi. Kijakazi huyu,alipiga kelele na kusema “… Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. ” Matendo 16:17. Kijakazi huyo,alisema kweli kabisa,kwa maana ndivyo akina Paulo wanachokifanya. Lakini sauti ile haikuwa ya kawaida,bali pepo mchafu aliwatambua akina Paulo.


Na kwa kuwa Paulo alikuwa na roho ya hekima na mafunuo,Paulo aliona nyuma ya ile sauti kuna nini,na hapo ndipo akamkemea huyo pepo amtoke huyo binti. Sasa kama ungelikuwa mmoja katika kundi hilo,labda ungelishangaa kwamba kwa nini Paulo amkemee mtu ambaye amenena vyema kabisa,? Paulo alipoona alimkemea yule pepo atoke! bila kujali nini kisemwacho!!!! Sasa fikiria kama Paulo asingelikuwa na roho ya mafunuo (kuona na kusikia rohoni),Je asingemfurahia binti huyo? Je angelimkemea?


Bila shaka angeweza kufurahia,kwa sababu kijakazi alikuwa “akiwafagilia” akina Paulo. Kuna wakati mwengine mtu anaweza akakusifia juu ya huduma yako uifanyao,lakini ndani yake kuna njama/hila fulani ambapo anakuvuta kwa sifa akupazo ili uingie kwenye 18 zake/mtego wake,na ikiwa kama huna macho ya rohoni,nakwambia utanaswa na kupigwa.Kumbuka ; Si kila anayekusifia anakupenda,bali wengine ni mapepo tu,yenye njama katika sifa hizo ili uanguke.

Leo kuna changamoto kubwa sana katika huduma kwenye eneo hili. Kwa maana wengi hawasikii wala hawaoni kiroho hali ni watumishi wa Bwana. Sasa mimi najiuliza,unawezaje kufanyakazi ya Bwana bila uwezo huo? Kwa maana hata adui yako yeye anaona ulivyo. Fikilia kijakazi tu,alikuwa anauwezo wa kuona kwa maana pepo la kuagua lilikuwa ndani yake. Ikiwa kijakazi/binti mmoja hivi anaweza kuona mambo yako


,je akiamua kukupiga si anakupiga kabisa! Ukweli ni kwamba unahitaji sana kusikia na kuona kiroho ili kusudi uone yanayotendeka kwenye kazi yako /huduma yako. Jipange sawa sawa kwa maana kazi ya utumishi si lelemama,kwa maana usipoona kiroho ujue watakuona wewe kiroho!…


ITAENDELEA…


Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Na kwa huduma ya MAOMBI ushauri na msaada zaidi,piga sasa +255 683 877 900


What’s app namba +255 746 446 446.


Na Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page