top of page

PENTEKOSTE.

Pentecost-Wishes-Painting

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Neno hili ``Pentekoste” bila shaka si geni masikioni mwako. Likini unaelewa nini hasa unaposikia likitajwa? Au unaelewa nini pale mtu mmoja akajitambulisha kuwa `` mimi ni mpetekoste…” Bila shaka huna maelezo ya kina au inawezekana hujui kabisa. Na hili ndilo tatizo la walio wengi,“kutumia maneno pasipo kujua ” . Mara ya kwanza niliposikia neno hili “Pentekoste ” akili zangu zilinieleza kuwa ni pentekoste ni kuokoka tu. Sikuwa mbali sana na maana halisi ya neno hilo,lakini sikuwa na majibu ya kina. Hivyo nimeona leo nikushirikishe hili ili ikuongezee ufahamu wako.

Maana halisi ya ``pentekoste” ni hamsini (50),neno hili linatokana na tafsiri ya Kiyunani ya agano la kale.,inayoeleza kuhusu sikukuu ya Israeli ya mavuno. Sikukuu ya mavuno asili yake ni kwenye agano la kle na sio agano jipya,Kwenye agano la kale sikukuu ya mavuno ilikuwa na majine mengine kama “sikukuu ya malimbuko au sikukuu ya majuma” . Katika agano jipya maana ilipanuka na kuitwa ni sikukuu ya Pentekoste (Matendo 2;1)

Kuanzia hapo “pentekoste’‘ ikabeba maana pana sana na muhimu sana katika historia nzima ya kanisa la Bwana kwa sababu ndio siku hiyo hiyo “kanisa lilizaliwa” kwa maana Mwana-Kondoo wa Mungu kwa damu yake alilinunulia kanisa lake safi kwa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu. Ni muhimu kujua historia ya kanisa ya kwamba Mungu aliachilia Roho wake kuonesha ishara kwamba kanisa ni lazima liongozwe na Roho mtakatifu.

  1. Roho mtakatifu aliachiliwa baada ya Yesu kufufuka. (Yoh.7:37-39)

Kabla ya Yesu kufufuka,wanafunzi wa Yesu hawakuvikwa uwezo utokao juu yaani Roho mtakatifu. Watu wengi hawaelewi hili ninalokufundisha sasa,kwa maana wanajua Roho mtakatifu alikuwa amewavika. Katika sikukuu ya pentekoste,(baada ya siku hamsini) Mungu alimimina Roho wake kwa wale wanafunzi 120 waliokuwa mahali pamoja na watu 3000. Ni muhimu kujua kwamba siku ya pentekoste,Yesu alibatiza katika Roho makundi mawili;

  1. Wanafunzi pomja na mitume 120 (Matendo 2:4)

  2. Watu wa mataifa 3,000 (Matendo 2:37-42) – Na kazi ya Roho mtakatifu iliendelea hata leo.

Hivyo,neno pentekose katika agano jipya linaangazia zaidi kanisa moja la Kristo (Kanisa moja lililo katika ushirika mmoja wa Roho mtakatifu,yaani mwili wa Kristo)tunapolitumia neno hili,au tunaposema “kanisa la pentekoste” maana ni lazima ibakie pale pale kwamba ni kanisa lenye misingi ya umoja katika Roho mtakatifu.

Kwa maana kusudi la Mungu kumwachilia Roho wake ni kuwaleta watu wote kwenye mwili mmoja wa Kristo Yesu na ndio maana unaona katita pentekoste walibatizwa kwanza wanafunzi na mitume wa Yesu 120,kisha baadae kipawa kile kile cha ubatizo katika Roho kiliwafikilia wamataifa kama vile Wasamalia,watu mataifa mengine walioamini kwa lengo la kuwa na kanisa moja la kiroho.

Ikiwa umebarikiwa na fundisho hili nifahamishe pia. Kwa maombezi pia nipigie kwa namba hizi hizi + 255 683 877 900 

WhatsApp ni +255 746 446 446

Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page