top of page

AHADI YA ROHO MTAKATIFU.

Updated: Aug 29, 2022

Bwana Yesu asifiwe..

Kwa ufupi,


Bwana Mungu alitanguliza ahadi ya kumwaga Roho wake mtakatifu tangu kipindi cha manabii. Nabii Yoeli alitabiri juu ya Roho mtakatifu atakayemiminwa juu ya wote wenye mwili Kisha akasema kumiminwa kutaambatana na kutabiri,kuona maono,kuota ndoto pia Bwana atafunua mambo ya ajabu katika mbingu na dunia ( Yoeli 2:28-30).


Yesu Kristo ndiye aliyebeba ahadi hiyo,alianza kuwavuvia Roho mtakatifu wanafunzi wake kabla ya kuteswa kwake, kufa,na kifufuka . Alipowaangalia wanafunzi wake aliona kuna kitu kimepungua ndani yao ndipo akawaambia “ pokeeni Roho mtakatifu ” Yoh.20:22 .


Tendo hili halikuwa utimilifu wa ahadi ya Roho mtakatifu kwa wanafunzi wake.Bali Yesu aliwafanya upya wanafunzi wake / kuwafanya viumbe vipya ndani yake Kristo akiwapa uzima wa kiroho,ambao ni sawa kabisa na kuzaliwa mara ya pili kwa wanafunzi.


  • Hivyo ahadi ya Roho mtakatifu ni ubatizo katika Roho mtakatifu uliofanywa na Yesu mwenyewe siku ya sikukuu kubwa ya mavuno ya Kiyahudi iitwayo Pentekoste ambapo siku hiyo,Wayahudi walileta mazao ya nafaka na kutolewa kama malimbuko Kwa Mungu. Ahadi ya Roho mtakatifu ikatukia siku hiyo hiyo kueleza kiashiria cha uamsho mpya wa kanisa na mavuno mapya ya Mungu


Utimilifu wa ahadi ya Baba, unaeleza uaminifu wa Mungu kupitia unabii uliotolewa na Yoeli ( Yoeli 2:28), Yohana mbatizaji ( Mathayo 3:11),Yesu Kristo ( Matendo 1:5). Kristo Yesu ndiye abatizaye kwa Roho na moto. Hivyo,ukumbuke ; ahadi ya Roho mtakatifu ni tofauti kidogo na kuvuviwa Roho mtakatifu siku unapookoka,ahadi ya Roho mtakatifu ni kubatizwa katika Roho mtakatifu.


Pamoja na hayo, mwinjilisti Luka anaandika Neno fulani muhimu sana kuhusu Roho mtakatifu. Neno ambalo ni muhimu sana kutafakari ili kusudi ufahamu zaidi kuhusu ahadi ya Roho mtakatifu katika maisha yako binafsi ( kwa maana ahadi hii si ahadi ya makundi makundi bali ni mtu binafsi kama mwili wa Kristo),anase anasema ;


“ Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” Luka 11:13


Neno hili linaelezea kuhusu ahadi ile ile ya Roho mtakatifu lakini si kwa watu wote Bali kwa wale tu “ wamwombao Mungu ” kuonesha wazi wazi kabisa kwamba kuna kipengele cha “ kuomba “. Kawaida ya mtu anayeomba ni yule mwenye uhitaji,kama mtu hana uhitaji kamwe hawezi kuomba,na akiomba atakuwa anaigiza tu.


Hivyo ni sawa na kusema yule mwenye kuhitaji ahadi ya Roho mtakatifu kwake anapaswa aombe ili Baba wa mbinguni amkirimie,ammiminie Roho mtakatifu. Hii pia ni sawa na kusema “ hakuna maombi,hakuna ujazo wa Roho mtakatifu “


Pamoja na kwamba ahadi hii ni kwa watu wote,bado kuna mkazo wa kuomba kupokea ahadi hiyo. Kwa sababu hiyo,pasiwepo mtu anayekaa vivi hivi bila kuomba na kutegemea kupokea ahadi hiyo!!! Ataisikia Kwa wengine tu wenye kuomba! Mkazo wa Luka,upo katika eneo la “kuomba” Kwa maana Neno Hilo limeanzia na kuonesha uaminifu wa Mungu kwa Kila aombaye atamjaza. Kipengele cha kuomba kinategemea kitu kinachoitwa “shauku,kiu” au “njaa ya ndani”


ukiwa na mambo hayo,waweza kuomba vyema na kujikuta unajazwa Kwa namna ya kufurikishwa. Hivyo ni vyema kutengeneza shauku na njaa ya kuhitaji ahadi hiyo ya Roho mtakatifu katika huduma yako/ maisha yako binafsi na uombe kwa kumaanisha ukihitaji kupokea ahadi ya Roho mtakatifu.


Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.


Na Kwa msaada zaidi unipigie simu Kwa+255 683 877 900


What’s app number +255 746 446 446


Na Mch. Gasper Madumla.


UBARIKIWE

Commentaires


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page