PASIPO MAOMBI HAKUNA MAJIBU ~ sehemu ya mwisho
- Mch. Gasper Madumla
- Aug 25, 2015
- 3 min read

Na Mchungaji Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
~Ikumbukwe kwamba,neno “majibu” huja mahali penye maswali. Ikiwa hakuna maswali,majibu ya nini? Au majibu yana kazi gani kama hakuna maswali?Leo, tuna maswali mengi kuhusu afya zetu,maswali kuhusu elimu zetu,maswali kuhusu kuonewa na nguvu za giza,N.K Maswali haya yote na mengineyo hutatuliwa kwa maombi,thus ninakuambia ya kwamba pasipo maombi hakuna majibu. Karibu tuendelee kujifunza;
Taratibu/sifa za muombaji mzuri.
02.MWOMBAJI AWE NI MSOMAJI WA NENO,MWENYE KULIISHI.
~ Mwombaji asiyekuwa na neno la Mungu kwa wingi ndani yake siku zote hukosa mafunuo kwa kile anachokiomba sababu neno la MUNGU ndilo taa ( Zab.119:105 ) yenye kuangaza mbele ili aweze kuona.
~ Ikumbukwe kuwa neno la Mungu ni kama maji bali maombi ni kama mbegu,hivyo mbegu haiwezi kukua kama imekosa maji. Mwombaji anapaswa awe ni msomaji mzuri wa neno la Mungu na awe analiishi,ambapo neno la BWANA litamuongoza aombe impasavyo.
Shida iliyopo leo,ni kwamba wengi huomba lakini ndani yao hawakuliweka neno la Bwana na hapo hujikuta wakikosa mafunuo kwa kile wakiombacho tena wengine sasa hawajui waombeje ombeje maana wamekosa muelekeo sababu ya kulikuso neno la Mungu kwamba sio wasomaji wazuri wa neno la Mungu.
03. MWOMBAJI AOMBE KWA JINA LA YESU KRISTO PEKEE.
~ Sisi sote tumepewa jina moja tu litupasalo kuokolewa kwalo,ambapo kwa jina hilo twapata wokovu (Matendo 4:12 ) tena kwa jina la Yesu Kristo aliye hai kila kilichokufa kinahuishwa tena,jina la Yesu Kristo laleta uzima,kwa maana lina uwezo,uweza,mamlaka,nguvu,utiisho N.K
Yeye mwenyewe Bwana Yesu Kristo anathibitisha akisema“ Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. ” Yoh.14:14. Mwombaji yeyote yule amuombaye MUNGU hapaswi kuomba kwa jina jingine lolote lile si jina la mtume,wala si jina la Mariamu,wala si jina la mtakatifu awaye yoyote yule,wala si jina la malaika,wala si jina la mzimu bali mwombaji aombe kwa jina moja tu,jina la Yesu Kristo Yeye aliyekufa,akafufuka,Yeye ambaye hakushikwa na uchungu wa mauti ( Matendo 2:24) naye ndie Bwana wa mabwana.
04. MWOMBAJI ATAMBUE THAMANI YA DAMU YA YESU KRISTO.
Maombi yaletayo majibu ni lazima yahusishwe na damu ya Yesu Kristo maana imo nguvu damuni mwa Yesu Kristo. Damu ikitumika katika maombi yaleta ulinzi,yaleta ushindi dhidi ya magonjwa na kila mishale ya yule adui iliyotupwa kwako. Damu ya Yesu Kristo huondoa dhambi ( Mathayo 26:28 ) maana hata katika torati vitu vyote vilisafishwa kwa damu,pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo ( Waebrania9:22 ). Mapepo hukimbia mahali penye damu ya Yesu,kamwe hawezi kupigana vita mahali pa damu ya Yesu ( Ufunuo 12:11 ) N.K Hivyo muombaji anapaswa kutambua nguvu iliyomu damuni mwa Yesu pale aombapo.
~ Hayo manne niliyokufundisha ni machache kati ya mengi yenye kuonesha sifa za muombaji yule aliyempokea BWANA Yesu. Maana zipo sifa nyingine za muombaji kama vile awe mtu msafi kiroho kwa kuzitubia dhambi zake,awe na shauku na kiu ya kumpenda Mungu.N.K
B.MAZINGIRA MAZURI YA MUOMBAJI.
▪ Kanisani.
~ Maeneo mazuri ya kufanya maombi ni kanisani kwa sababu ndani ya kanisa hakuna usumbufu wa kupata wageni,au usumbufu uletwao na watoto wachezao kama vile mazingira ya nyumbani. Kanisani ni mahali pa utulivu sana ukilinganisha na maeneo mengine. Tunapohitaji tuseme na Mungu wetu basi ni dhahili tunahitaji mahali tulivu ambapo twaweza kuisikia sauti ya BWANA.
▪ Nyumbani mahali pa faragha.
~ Hii ni sehemu ya utulivu,faragha~Mfano,wapo watu wenye kutenga kajichumba cha ndani cha maombi mahali ambapo akizama humo akiibuka amekuja na majibu. Mahali hapo si pa kucheza cheza watoto au kuingia ingia wageni na kutia story,no! Bali ni chumba special cha maombi. Chumba hiki kinafananishwa kama ikulu,au ni kama jikoni pa kupika mambo ya kiroho kwa sababu ya umuhimu wake.
▪ Milimani./Kambi
~ Sehemu hizi za milimani au kambi ni sehemu nyeti sana za maombi maalumu ambapo hata Bwana Yesu alizitumia mara nyingi huko milimani. Mathayo 14:23,Mathayo 17:1-2,Marko 6:46, Luka 9:28.
C.EPUKA MAZINGIRA MABAYA YA MAOMBI.
▪Kuomba ukiwa amelala.
~ Maombi ya namna hii pale muombaji anaomba huku akiwa amejiegesha kitandani,au katika sofa~ Sasa katika kanuni za uombaji mzuri hatushauli maombi ya namna hii kwa sababu muda wowote ule muombaji anaweza kutekewa na usingizi,kisha akalala badala ya kuomba.
▪ Kuomba simu zikiwa on.
~ Maombi mazuri yanahitaji utulivu wa kiroho wa hali ya juu sana,simu ni moja ya kwazo la kuondoa utulivu huo. Sababu simu ikiwa on zinaweza kuita na kuondoa umakini wa mawasiliano yako wewe na Mungu kisha ukaanza kufikilia mawasiliano ya kibinadamu. Mfano fikiria upo katikati ya utamu wa maombi gafla simu yako inaita,ile kuangalia unakuta anayekudai ndio anapiga na wewe ulimuahidi kumlipa siku hiyo,na kumbe hukupata pesa yake~hapo sasa!!! Ndiposa utaanza kuwaza mengine ya madeni badala ya kuomba.
▪ Maombi ya watu wenye jinsia mbili tofauti ambao si mke na mume ndani ya gheto/chumbani.
Haya ni mazingira hatarishi ya maombi,maana dakika yoyote ile waombaji hawa wanaweza kutekewa na ukimya wa geto/chumbani na kujikuta wameanguka katika matamanio,kisha…. lah!,..(.wakajamiiana ). Waombaji wowote wa namna hii,wanapaswa kuombea wakiwa kanisani au maeneo yasiyo ya faragha. Maeneo ya geto ni maeneo chochezi ya zinaa. Yatupasa kuikimbia zinaa ( 1 Wakorintho 6:18 ).
Ikiwa unahitaji msaada wowote ule wa maombi,basi usisite kunipigia kwa namba yangu hii +255 683 877 900.
What’s app number ni +255 746 446 446
Mch.Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
Comentários