top of page

MAOMBI.

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Neno “ maombi” limetokana na neno “ praise” lenye maana ya “ kusifu“. Katika kusifu tunaomba pia. Hivyo neno maombi humaanisha hasa namna ya mawasiliano kati ya mtu na Mungu katika kusifu,kuabudu,kushukuru,kutubu na kupeleka mahitaji binafsi. Njia za Mungu za kuwasiliana nazi ni nyingi na hazichunguziki,lakini njia za wanadamu za kuwasiliana na Mungu huanza katika maombi kama njia maalumu. Maombi ni kama mlango muhimu uliowekwa wazi kwa waaminio wenye kiu ya kuwasiliana na Mungu wao.

Hapo zamani, taratibu zilizopo zilikuwa ni tofauti na sasa,kwa maana Mungu alijichagulia watu wachache wataosimama kati yake na kusanyiko. Watu ambao watawasilisha yale tu anayoyasema,mtu kama Musa ni miongoni mwa watu wa Mungu waliosimama katika kusanyiko. Musa ndiye aliyekuwa na kibali / access ya kusikia sauti ya Mungu kisha na kuwaambia Israeli. Kwa hiyo Israeli alimsikia Mungu kupitia Musa,hakuweza kuomba moja kwa moja. Lakini kwenye agano jipya Roho Mtakatifu ameachilia kipawa hiki,kwamba kila mmoja aliyempokea Yesu,basi anakuwa na kibali / access ya kumwendea Bwana moja kwa moja. Hali hii ndio tuliyonayo hata sasa.

Baada ya anguko,watu walikuwa mbali na uso wa Mungu. Neema ya Bwana ikafunuka kwa kizazi cha Sethi mtu yule aliyesimama kwenye nafasi ya mtu mwenye haki aliyeuwawa na kaka yake,huyu ni Habili. Baada ya kizazi cha Sethi,Enoshi kizazi kipya,hapo ndipo watu walipoanza kuliitia jina la Bwana; maombi yakaanzia hapo Mwanzo 4:26.

  1. Mambo muhimu katika kanisa / nguzo tatu

“ nguzo” ni muhimili inayosimamisha jengo lote. Kanisani linasimamishwa na mambo mengi,lakini mambo yafuatayo yanalifanya kanisani la Bwana kutoteteleka;

  1. Roho mtakatifu – Matendo 2:4

  2. Neno/Kutafakari na Maombi- Matendo 1:14,2:42 na Luka 19:46

Maombi ni lazima yawe na ratiba yake maalumu – Matendo 3:1

Biblia inataja namna ambavyo Petro na Yohana waliokuwa wakikwea kwenda Hekaluni kuomba saa tisa. Biblia inapotaja muda fulani, ina maana kubwa sana. Maana kubwa ni kumfahamisha msomaji kwamba tukio hilo lilikuwa likifanywa kwa kuzingatia muda. Yaani ina maana tukio hilo halikufanywa kiholela olela,bali lilikuwa na muda maalumu. Maombi ni tukio linalohitaji muda maalumu, muda mzuri. Changamoto kwako,Je unatenga muda maalumu kwa ajili ya maombi? Au unaomba omba tu bila ya kuwa na ratiba kamili? Ukitaka kumwona Mungu, jaribu kuseti muda wako wa maombi kila siku kama akina Petro na Yohana walivyojiwekea muda wao.

Kwa nini tunaomba?

  1. Sisi tu wahitaji mbele za Mungu ( Mwanzo 25:21)

  2. Tuna imani ya kupokea tuyaombayo ( Mathayo 7:7)

  3. Bwana hujibu maombi yetu hasa kwa kipindi cha mateso ( Zab.118:5,Zab.30:2)

  4. Kushinda vita,vikwazo na majaribu mbalimbali ( Luka 22:40,Danieli 2:17,10:11-14)

  5. Kufichuliwa kwa mambo makubwa na magumu usiyoyajua ( Yeremia 33:3)

  6. Kwa ajili ya ushirika na Mungu

Ni kwa namna gani tunaomba?

  1. Kwa jina la Yesu tu – Yoh.14:13-14

  2. Katika Roho – Waefeso 6:18

  3. Sawa sawa na mapenzi ya Bwana – 1 Yoh.5:14

  4. Kwa njia ya faragha – Luka 22:41,6:12,Mathayo 14:23

  5. Kutanguliza sifa na kuabudu kabla ya kuomba

  6. Kuwa na hoja maalumu – Isaya 41:21

  7. Katika kusanyiko – Matendo 12:5

  8. Kuwaombea wengine – Matendo 12:5

  9. N.K

Matokeo mawili ya maombi ni kupata ushindi wa kiwango cha juu ( Kutoka 17:8-13), lakini pili kwa njia ya maombi macho yetu hufumbuliwa kuona yasiyoonekana kwa kawaida. Hata hivyo ikiwa mtu hataishi maisha bila maombi basi hakika vifungo mbali mbali vitakuwa ni sehemu yake. Tena shetani atafaulu kumchezea atakavyo,kwa maana shetani haogopi jina lako la kikristo,isipokuwa huogopa pale uombapo.

Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,nifahamishe. Na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga sasa +255 683 877 900

Whatsapp namba +255 746 446 446

Mch. G. Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page